Ongeza thamani na fedha zitakufuata. Fedha huvutwa kwa kutoa thamani na kujua sayansi ya utoaji inavyofanya kazi.

Fedha ni hitaji la muhimu sana kwa zama tunazoishi. Mtu anayekwambia fedha si muhimu basi huenda anazo tele. Fedha ni muhimu mno kwa mifano mingi ambayo wewe mwenyewe umekuwa shahidi pale ambapo hitaji lako lingeweza au linaweza kujibiwa dakika chache tu kama ungekuwa na fedha.

Fedha ni alama ya thamani ya kitu au bidhaa au huduma ambayo imetokea ya kufanya mambo mawili makubwa. Jambo la kwanza ni kutoa thamani ya kukidhi mahitaji na la pili ni utatuzi wa changamoto. Mtu anayeweza kupata fedha wakati wowote basi lazima ajue sayansi hii ya kutengeneza fedha kwa njia ya kutoa thamani.

Utoaji ni kipengele muhimu sana katika kuvuta fedha kwa namna ya ajabu sana. Unapojua utoaji kwanza ndio msingi wa utokeaji wa vitu vingi basi fedha ni mojawapo ya matunda ya watu wanaojua sayansi ya kutoa na vipi inachangia kuvuta fedha na utajiri maishani.

Malenga wa Ubena

raymondpoet@yahoo.com

Leave a comment

Design a site like this with WordPress.com
Get started