Rafiki wako wa kweli wa mafanikio – “Soma vitabu sasa”

Wakati naanza vitabu nikiwa bado kijana mdogo sikuweza kuona nguvu yake. Ila kadri muda ulivyoenda ndivyo nilivyoanza kuona vitabu ni rafiki wa kweli wa Maisha ya mafanikio. Kila nilipopitia changamoto nyingi katika maisha, vitabu vimekuwa njia kubwa ya kujifunza, kuona mwanga na kunisaidia kuvuka vikwazo. Rafiki wa kweli huyu amekuwa ni rafiki wa faida karibu …

Kila hatua unayochukua ina mchango kule unakotaka kufika

Hatua ndogo ndogo tunazoendelea kuchukua katika maisha yetu zina mchango mkubwa wa matokeo ambayo tunayapata maishani. Matokeo yoyote makubwa ni matokeo ya mkusanyiko wa hatua ndogo ndogo, machaguzi au maamuzi ya mambo anayofanya mtu kila siku. Usijekudharau hatua yoyote ile iwe kwa udogo au kwa ukubwa ukidhani haina mchango wowote kule unakotaka kufika. Kinachotuchelewesha kufanikiwa …

Kila kinachokutokea kinakuimarisha – “Mambo hutokea yatakavyo”

Naheshimu kila siku nayopata ya kuona, kutembea, kujifunza na kujiboresha nikiwa naamini haya ni mambo muhimu kwa mtu anayeheshimu zawadi ya maisha. Maisha yanatusaidie tuone, tutembee, tujiboreshe, tujifunze na katika hayo yote tupate kukua. Ukuaji wetu wa fikara na hisia ni ukuaji muhimu katika kumsaidia mtu awe mtu mkomavu. Ingawa mambo haya ni mazuri ila …

Jitolee kwanza kabla hujapata fursa unayoitaka

Kujitolea kunaeleweka pengine tofauti tofauti na watu mbalimbali. Wengine wanaona kujitolea ni kudidimizwa na kutumiwa bila faida na wengine wanaona kujitolea ni msingi na ngazi ya kwanza kuweka mguu kupanda kule wanakotamani kufika. Leo tugusie eneo la pili namna kujitolea kulivyo na manufaa kabla hujapata kile ulichokuwa unakitafuta maishani. Ujuzi na uzoefu ni mahitaji makubwa …

Kazi zote bora hutokeaje tokeaje ?

Utakuwa umewahi kupitia hali fulani ya kuzipongeza kazi zote za zamani kuwa zilikuwa bora kuliko sasa utakuta kuna msemo uitwao “Old is Gold” kwa maana ya “kale ni dhahabu”. Huenda hicho kitu ni muziki fulani umesikia basi unasema ama kweli watu wa zamani walifaidi sana. Nyimbo, picha, maisha ya kale, watu mashuhuri wa zamani utaona …

Safari ya Maisha ni ya pekee na Kila mtu hupitia mambo kwa majira yake – “Kila Mtu na Wakati wake”

Si kweli wakati ambao unapitia magumu wewe basi ndivyo kwa kila mtu wakati huo anapitia magumu. Wakati ambao wengine wanalia au kupitia changamoto za maisha wengine wanaendelea kufurahia maisha na kufanikiwa zaidi. Hili ni funzo kubwa la maisha kuwa kila mtu ana safari ya pekee na hupaswi kuidharau safari yako kwa kujilinganisha na watu wengine. …

Wakati unapongoja mambo yabadilike, hayabadiliki hadi uwajibike.

Maisha ni wajibu mkuu wa kila mtu aliye mtashi kukubaliana na ukweli kuwa “maisha ni matokeo ya uwajibikaji wetu kwa namna fulani”. Wajibu huu unatupa kutualika kwa kila matokeo ambayo tunakutana nayo maishani basi kwa sehemu tumechangia kuwa hivyo iwe twajua ama hatujui. Mambo hayabadiliki hadi pale sisi tunapobadilika kuyaona yalivyo. Himizo la kubadilika kwanza …

Ulivyonavyo anza kushukuru mbali na usivyonavyo.

Katika darasa la maisha huwa tunasahau kuona ni utajiri upi mkubwa ambao tunao pale ambapo tunasahau tulivyonavyo na kuhangaika na tusivyonavyo. Tunasahau namna ni rasimali ngapi tulizonazo ambazo zingeweza kutusaidia kuvuka hatua fulani kubwa maishani. Wiki hii nilifanya zoezi la kuangalia au kushukuru mambo ambayo ninayo kuliko yale nisiyonayo. Zoezi hili nilifanya kwa kuchukua notibuku …

Kufundisha ni kuivusha jamii – “Asante mwalimu wangu, Wewe ni Daraja”

Leo ni siku ya walimu Duniani kote. Siku hii ni kutambua na kufanya tafakari ya kina ni kwa vipi uwepo wa walimu umeleta matokeo chanya na kuisaidia Dunia kustawi vizazi hadi vizazi. Nafasi ya walimu ni kubwa sana unapokuja kuelezea maendeleo ya mtu mmoja mmoja hadi jamii nzima. Majitoleo yao ya muda, maarifa na maisha …

Matokeo ya malengo hayaji mpaka pale unapoweka kazi kubwa na maarifa sahihi.

Kuna mambo mawili ambayo mtu anaweza kulalamika kuwa mbona sipati matokeo ninayoyataka katika nipangayo?. Moja utakuta mtu huyo hakuweka kazi ya kutosha au juhudi za kutosha katika anachokitaka. Pili ni maarifa sahihi katika kile anachokipigania. Haya mambo mawili yanaathiri mno katika matokeo ya jambo lolote lile. Huwezi kupata kitu bila kufanya kazi fulani na kama …

Design a site like this with WordPress.com
Get started