Featured

Makala; Nguvu ya 100, mambo 100 na kama fedha, mtandao wa kutosha wa watu unavyoweza kuisaidia jamii miaka 100 ijayo.

Makala hii ni moja ya zoezi ambalo nimejipa mwenyewe katika kutii ushauri wa mwandishi Brian Tracy namna fedha ni muhimu ikiwa utapata namna bora ya kuitumia kuisaidia jamii. Hivyo akawa kapendekeza kuandika mambo 100 unayoweza kufanya kwa kutumia fedha, mtandao wa watu kuisaidia jamii ikapiga hatua za juu. Name sikuchelea kuandika yale ambayo nimeona yanaweza [...]

Ngozi ngumu; Wakatishaji tamaa ni wengi

Marcus Aurelius anasema “Kila siku unayoamka jua unaenda kukutana na watu wasumbufu, wakorofi, wasio na shukrani, wakatishaji tamaa, wasiojua kupongeza, wasiojua mazuri na wenye chuki na hatua unazopiga siku hadi siku”. Ukija kwa kina wanaokukatisha tamaa kuna mambo mawili au matatu yanawasumbua. Moja ni wao kushindwa kufanya kitu unachokifanya hivyo wanajilinganisha na wanaona wewe mbona [...]

Ongeza thamani na fedha zitakufuata. Fedha huvutwa kwa kutoa thamani na kujua sayansi ya utoaji inavyofanya kazi.

Fedha ni hitaji la muhimu sana kwa zama tunazoishi. Mtu anayekwambia fedha si muhimu basi huenda anazo tele. Fedha ni muhimu mno kwa mifano mingi ambayo wewe mwenyewe umekuwa shahidi pale ambapo hitaji lako lingeweza au linaweza kujibiwa dakika chache tu kama ungekuwa na fedha. Fedha ni alama ya thamani ya kitu au bidhaa au [...]

Usisubiri hadi mwaka mpya upange malengo. Kila asubuhi ni siku mpya katika maisha na hujui yatakayozaliwa siku ijayo.

Ni mtu kipofu yule asiyeweza kuona alichonacho na kuhangaika na asichonacho. Hili linatokea pale mtu anaposubiri kuanza maisha mapya kila ifikapo mwaka mpya na siku nyingine 300 zinaenda tu pasipo kuziishi kitoshelevu. Maisha ni sasa na asubuhi ifikapo ni maisha mengine mapya huendelea nayo huendelea kuwa sasa. Iwe ni mwaka mpya bado itakuja kuwa sasa. [...]

Unachokiona kigumu sasa ni sababu u mgeni kufanya kitu hicho. Jipe muda utajua kama wanavyojua wengine.

Maisha ni ngazi. Ngazi ina sehemu ya chini na sehemu ya juu. Huwezi rukia juu pasipo kuanza chini hatua hadi hatua. Hili lipo katika safari ya kujifunza mambo mapya maishani. Hatua za mwanzo za kujifunza kitu huwa kinaonekana kigumu kweli ila muda unapopita kama utajitoa kujifunza basi ule ugumu wa awali huanza kupotea siku hadi [...]

Kuchukua hatua mapema kunazuia gharama kubwa baadaye.

Kughairisha mambo ni tatizo kubwa linalonyima fursa nyingi kufunguka kwa watu wengi. Pale unapoghairisha vitu au kufanya jambo kwa kufikiri huenda baadaye utafanikiwa kulifanya kumesababisha majuto makubwa siku zijazo. Imekuwa kawaida kughairisha mambo kwa kufanya siku moja na baadaye kughairisha inakuwa tabia inayosababisha mambo mengi yasiwezekane kutokea. Hili linaonekana dhahiri pale ambapo mwaka mpya unapoanza [...]

Somo la maisha yangu yalopita- LEO NI NYEPESI ILA SIO KESHO

Napenda kuandika, najisikia utoshelevu kuandika, sitaacha kuandika. Kuandika kunanirudisha katika kina cha mawazo, kunanipa nguvu nisiyoweza kuelezea. Uandishi ni alama ambayo itabaki na kunipita miaka mingi kuishi zama hadi zama. Vile tusomavyo leo maandishi ya watu waloishi miaka zaidi ya 2000 basi ndivyo ilivyo alama ya uandishi hudumu vizazi hadi vizazi. Nami nashukuru kuwa katika [...]

Makala ya uchambuzi wa kitabu; Embracing Life After Loss by Allen Klein (Maisha baada ya kuondokewa)

Maisha ni zawadi pale ambapo watu huendelea kuishi. Ila wanapoondoka na kuwa mbali nasi kwa njia ya kifo na kutokuwa na matumaini ya kuwaona tena ndipo maisha hugeuka na kuonekana ni mateso na maumivu yasoweza kuelezeka. Ila kupoteza watu wetu wa karibu ni jambo lisiloweza kukwepeka maishani. Maana hata sisi siku moja tutaondoka na kuwaacha [...]

Mahojiano; Sam Vidambu kutoka Kenya

Karibu tujifunze pamoja rafiki, Dunia inakua haraka tofauti na miaka 500 ilopita. Uwepo wa ukuaji wa mitandao ya kijamii kumeleta manufaa makubwa ya kujenga mtandao wa marafiki, walimu, menta kupitia mitandao ya kijamii hasa majukwaa ya mtandaoni kama “Whatsapp”. Mwaka huu nilikutana na ndugu Sam Vidambu kwa kuunganishwa na rafiki yangu Deviano ambaye naye tulionana [...]

Create your website at WordPress.com
Get started