MAMBO 20 YA KUJIFUNZA KATIKA KITABU CHA “MY JOURNEY” Journey to the Land of Knowing Yourself na Mwandishi, Mhamasishaji na Mkurugenzi wa Kijani Kibichi Tanzania Adam Ngamange
Kama zilivyo safari nyingine za kutoka eneo moja kwenda eneo lingine, vivyo vivyo kunayo safari ya kusafiri ndani yako kujua uwezo ulionao, vipaji au kipaji, majibu, vipawa na ujuzi. Hii ni safari huenda inasafiriwa na watu wachache lakini ni safari ya muhimu kwa maisha yenye maana na ya thamani kwa mtu. Ungana nami kujifunza na kushirikishana mambo haya
Twende pamoja kusafiri na kujua mambo haya 20 katika kitabu hiki yatakayokusaidia kusafiri safari yako ya ndani. Karibu twende pamoja
1. Maisha yanaanza kwa kujiuliza maswali muhimu na kuyapatia majibu sahihi, katika safari ya kusafiri kujijua ndani wewe ni nani?, kwanini upo hapa?, umetokea wapi?, naelekea wapi?, na namna gani kufika kule?
2. Usijifananishe na mtu yoyote maishani kufanya hivyo ni kujidharau na kujishusha thamani yako, wewe una upekee wa ajabu, jikubali
3. Uwezo wa kufanya makubwa na kuishi ndoto yako ni akili ambayo Mungu kakupa, waisraeli wanasema majibu na mafanikio yapo chini ya fuvu.
4. Na mtu huwa kwa kadri kile anachokifiri, ni matokeo ya akifikiricho muda wote.
5. Kipaji ni uwezo na eneo unaloweza kulifanya kirahisi na kwa ubora, na wengi wamedharau uwezo huu ( kipaji).
6. Ukipendacho kina nguvu ya kukufanya kwa namna yoyote ukipate, na vivyo nguvu ya kipaji, au ndoto ina nguvu kuliko hata nguvu ya bomu.
7. Zungukwa na watu watakaokuwa na hamasa yakukupa ya kufanya makubwa na watakupa njia ya hatua kubwa zaidi.
8. Je ni wazo gani wapenda kulifikiri, ni maarifa gani wapenda na hii itakupa majibu ya maswali mengi
9. Fanya unachokipenda maana ndipo iliko furaha yako, na kwa namna hii hutengeneza furaha kwa wengine.
10. Namna matumizi ya siku zetu, ni jinsi ilivyo matokeo ya maisha yetu
11. Kipaji ni kama umeme, haueleweki ila tunautumia, haya ni maneno ya nguli mshairi Maya Angelou.
12. Jitengenezee kifungu cha maneno cha kwanini upo?, kusudi la uwepo wako, unataka nini?, katika maisha na wapi unataka kuelekea au kuwa?
13.Maisha ni Mchezo, gundua uwezo ulionao yatumike kama mabawa kukupeleka hatua ya zaidi.
14. Ukuu wetu ni zawadi katika dunia, na jinsi itakavyosaidia uwepo wako kuwa na mchango na kufanya ulimwengu sehemu salama.
15. Ni muhimu kujua lugha ya umbo au ya picha kama mwonekano, sauti, mavazi, umbali, rangi, muda na mguso.
16. Uwezo wa kuzungumza ni ujuzi ambao kila mmoja ana deni la kujifunza kujua namna gani ya kuzungumza na kila mmoja.
17. Saikolojia ya rangi ina athari katika tabia za mtu, rangi ni lugha mama kwa akili, na hii huifanya akili kushika sana na kukumbuka picha kuliko maneno.
18. Rangi ina uwezo wa kuongea zaidi kuliko maneno, mfano mdogo nyeusi huogopwa na watu, na pia rangi kama nyekundu hutumika kama ishara ya upendo.
19. Ni rahisi kubomoa kuliko muda wa kujenga
20. Kujifunza ni sura ya kwanza ya mlango wa afya bora, utajiri na kukua kiroho
21. Maisha ni hadithi nzuri iliyoandikwa na Mungu, haijalishi changamoto au magumu gani, endelea kuwa mtu wa shukrani na kwayo yote ni sura mpya bora kwa hatua nyingine. Kumbuka Mungu anakupenda mara zote usivunjike moyo
Asante kutenga muda wako, kujifunza ni kuwekeza kuliko na faida, kuipata hii kopi kwa kujifunza zaidi wasiliana na mwandishi ujifunze zaidi
Adam Ngamange 0656143785
Imeandaliwa na
Raymond Mgeni © 2017