Habari mfuatiliaji wa blogu hii kila siku nikupe pongezi kujitoa kwako kila siku kujifunza na kupata kitu kipya cha kukusaidia katika maisha, maisha ni mtihani mkubwa unahitaji maarifa mengi ili kuyaelewa na kuishi katika kanuni ili kufika ngazi ya mafanikio yenye furaha na amani. Mungu ni mwema kutupa siku hii kuitunza na kuieheshimu maana ikipita imepita haitakuja kurudi hata kwa gharama yoyote ile.
Nikukaribishe tushirikishane mambo machache ya kukuweka kitu kipya kwako kichwani, moja ya jambo linalotia sana moyo ni kuwa muda huenda na hakuna kinachodumu kwa maana ya kizuri au kibaya kina ukomo wa muda wake, hivyo hii ni habari njema kabisa kuisikia, muda ni adui wa mambo mengi na pia ni rafiki kwa wanaothamini. Tuendelee kujikumbusha habari hii kila siku huwa inapita.

Kama unaendelea kupambana na kitu unachokifanya iwe ni kazi, ndoto, jukumu, kipaji na lolote lile lenye manufaa basi unazidi kusogea kila siku katika unachokitamani kufika, maana siku hadi siku huwa, haina haja ya kuishia njiani sababu unakaribia kufikia endapo kila siku unafanya kama ni uandishi endelea kuandika, kama ni kipaji endelea kukinoa mpaka kiwe na makali ya kukata, siku hadi siku huwa.
Endelea na juhudi na imani kuwa haba na haba hujaza kibaba, zawadi tuliyonayo kwa wote ni MUDA. Na kila kitu kinawezekana katika kujua siri zilizopo katika muda, muda una nguvu, mafanikio yamefichwa katika muda, siku hadi siku huwa, endelea utafikia pale unatamani kufika. Ondoka na falsafa hii siku hadi siku huwa
Niishie hapa rafiki, msomaji na mfuatiliaji wangu unayefuatilia blogu hii kila, nikutakie mafanikio makubwa katika ufanyalo usisahau kuondoka na falsafa hii kuwa kwa lolote lile umeliwekea juhudi jua siku hadi siku huwa. Endelea mbele maana macho yapo mbele tusonge mbele tu
Na Malenga wa Ubena
Raymond Mgeni ©2017
Mgeniraymond©yahoo.com
0676559211
Jukumu ni lako, Chukua hatua