159: MAMBO 29 NILIYOJIFUNZA KITABU CHA ELIMU YA KUJITEGEMEA Na Mwalimu Julius K. Nyerere

Habari za asubuhi, U hali gani ?  Msomaji na mfuatiliaji wa blogu hii kila siku, karibu katika uchambuzi wa kitabu na mambo niliyojifunza kupitia kitabu hiki. Kama ilivyozoeleka katika taifa lolote lile duniani elimu ndio himizo linalopewa kipaumbele katika kumkomboa mtu kifkra na akawaza kitofauti na akawa tayari kukabiliana na changamoto na haishii tu hapo …

157: Jiwekee Nidhamu hii Kama Kiungo Katika Kufanikiwa

Habari mfuatiliaji wa blogu hii kila siku. Bila shaka unaendelea vizuri na mipangilio yako na ratiba zako kila siku. Nafasi ya kuwa na pumzi ni nafasi ya pekee sana kukupa fursa ya kujiendeleza na kujipanga kwa ubora zaidi. Na muda ndio kipimo cha mchango wa mtu duniani kila siku. Endelea kutumia vizuri fursa hizi mbili …

156: Jambo Moja la Muhimu Kabla Ya Kuanza Wiki Nyingine Mpya

Bila shaka u mzima wa afya na nguvu na unaendelea vizuri na ratiba na kutumia kwa uzuri nafasi ya Pumzi na Muda wako. Na nikupongeze kwa kujitoa kwako kujiwekeza katika maarifa na kujifunza kila siku. Wikendi yako bila shaka kuna kitu ukikaa ulijifunza na ambacho ukitumia wiki ijayo kitakusogeza hatua zaidi. Karibu nikushirikishe kitu uzidi …

155: Hizi ndizo Siku 3 Zinazokumwamisha au Kukuimarisha Maishani

Habari mfuatiliaji wa blogu hii kila siku. Bila shaka ifikapo jioni ni wakati mzuri sana wa kuangalia siku yako ilikwendaje ?, ni wakati wa kujipongeza pale ulipoweza na pia ni wakati wa kujikagua pale ulikosea. Kila siku kama utakua makini kutaka kujifunza hubeba mambo mengi sana ya kukusaidia kujifunza. Usisahau thamani ya mtu ni pumzi …

154: UTUMWA WA TUMBO USIZIDI WA UBONGO

Shairi: Utumwa wa tumbo usizidi wa Ubongo Karibu Pishi hili kulighani na Ujikumbushe na Kujifunza zaidi, Karibia na umalize kula pishi hili. Kiandae Chakula cha Tumbo Ubongo usipige kikumbo Lijaze kwa milo lako tumbo Usilishe Ubongo makombo Utumwa wa tumbo usizidi wa Ubongo. Andaa maakuli mezani Sisahau vitabu kichwani Kawashe nao moto jikoni Sipuze bongo …

153: Sababu 2 Kwanini? Ujifunze kwa Waliokutangulia

Habari mfuatiliaji wa blogu hii kila siku, bila shaka kiu ya kusonga mbele zaidi ya jana ipo. Na ndio jukumu na kusudio kwa kila mmoja kuona hatua kwa hatua zikisogea. Nafasi ya kuwa na Pumzi ni ya pekee sana kuendelea kutoa mchango wa kimawazo kwa ajili ya kuboresha na kukuza jamii zetu, zizidi kupiga hatua …

152: Hii Ndio Fedha Unayomiliki Yenye Kukupa Uwezo Wa Kununua Chochote

Habari mfuatiliaji wa Blogu hii Kila Siku. Ni jambo la pekee sana kila siku unapopata nafasi ya pumzi na afya ya kupambana na kuendelea na Mipangilio mbalimbali ya kimaisha. Nafasi ya pumzi ni ya kuipa uzito mkubwa maana ndio thamani katika mwili wa mtu na viumbe wengine wote. Niendelee kukupongeza wewe unayeendelea na safari ya …

151: Hii Ndio Zawadi ya Kuipa Heshima Sana

Habari mfuatiliaji wa blogu hii kila siku. Leo ni siku ya pekee tena kumshukuru Mungu aliyetupa nafasi tena baada ya kulala na kuweza tena kuamka kwa tarehe 12/09 ili kuendelea na majukumu ya kila siku. Nafasi hii ni ya pekee sana kujiboresha, kujifunza na kuanza mambo ya kusema kesho kesho. Leo ndio jana uliisema kesho. …

150: SHAIRI – JIONI HUTUFIKA WOTE

JIONI WOTE HUTUFIKA U hali gani na siku, kwangu likuwa Salama Vipi mebaki shauku, ya Asubuhi Mapema? Karibu figani huku, Ninalo jambo kusema Jioni mwisho wa Siku, Jipe kujitafakari Kuifikia Jioni, giza huja hufunika Ulipotokea ndani, kazi zende kufanyika Na shuka la kitandani, Ilibidi kuachika Jioni mwisho wa Siku,Jipe Kujitafakari. Masaa mepukutika, jioni ikishafika Ulopanga …

Design a site like this with WordPress.com
Get started