Habari mfuatiliaji wa blogu hii kila siku, kila siku ni Zawadi nzuri sana ya kuitunza kwa kuheshimu muda na nafasi ya pumzi ambayo Mungu ametujalia kufika hapa ili siku ya leo tuendelee kujiboresha zaidi ya jana. Kujifunza ndio njia pekee ya kutufanya kuwa bora kila siku kwa kujifunza mambo ambayo jana tulikosea ila leo ni nafasi ya kurekebisha na kufanya kwa ubora zaidi. Karibu katika Shairi ujifunze na Uchukue Hatua.

Si pekee kwalo tumbo
Ila akili nayo ina mlo
Mpaka nayo izue jambo
Haja taarifa ziwe za kilo
Akili ina Mdomo, Chunga unachotafuna
Ina uwazi wa kuingia
Mlo wake nao kachangia
Zile Ovyo itadidimia
Na hapo giza litaingia
Akili ina mdomo, Chunga unachotafuna
Kiingiacho ndo kitokacho
Iwe sikio au kwa macho
Mlo leo huzaa kijacho
Hata kama mlo wa kificho
Akili ina mdomo, Chunga unachotafuna
Mdomo
Wake Kimo
We Yaliyomo
Yakuchangiamo
Changizo la kipimo
Kipimo chake egamo, Egamo kuwa mdomo
Kipi ndani kingiamo?, Ndicho huleta tetemo
Hujaza na yaliyomo, akili yenye ukomo
Shida likua mdomo, Ndani akili ya shimo
Hicho Unachofatuna
Kinacho sana maana
Ndani paka changamana
Juu au kwenda kina
© Raymond Mgeni 2017