367; Mambo 31 niliyojifunza Mwezi wa Tano, na Safari ya Kwenda Nusu Mwaka na Shamrashamra za Kombe la Dunia.

Habari ya siku ya 151 toka mwaka huu uanze. Ni nafasi ya pekee sana ya uhai kufika mpaka hapa tulipofika leo, tumshukuru Mungu kwa nafasi hii. Kuna mengi yamepita na katika kipindi hiki chote toka ilipoanza mosi ya Januari na sasa siku ya 151 kuelekea nusu mwaka na kisha mwaka kuisha ifikapo mwezi wa 12. …

366; Safari ya Siku 365 toka nianze kuandika Figa la Ushairi, nilipo na ninakoelekea na Mambo 10 nilofunzwa na uandishi pamoja na Kiapo cha uandishi hadi kufa.

Awali ya yote, nimshukuru Mungu aliyenipa nafasi ya uzima na afya mpaka kufikia siku hii ya leo siku ya 365 toka nianze kuandika katika figa la ushairi. Si kazi nyepesi kuandika karibu mwaka mzima, hivyo nawiwa kumshukuru sana Mungu kwa nafasi hii, pili wazazi wangu Baba na Mama kwa kuona nina jambo kiduchu la kuchangia …

365; Siku ya Kuaga na thamani ya wakati kilikuwepo na Kukumbushwa jambo kubwa la KUSHUKURU

Habari Rafiki, bila shaka umeamka salama kabisa na upo tayari kwenda kufanya makubwa siku ya leo. Kuwa hai na kuwa na nafasi hii ya uzima ni jambo la pekee sana na kumshukuru sana Mungu kwa nafasi hii. Hivyo kuitumia vizuri na kuanza yale ambayo jana tulisema tutafanya kesho, basi kesho hiyo ni leo na sasa …

364; Siku 3 Zimebakia za Zawadi na Vifurushi Vya Maarifa Mwanzo wa Nusu Mwaka ( Mwezi wa Sita ~ Mwezi wa 12 )

Habari Rafiki, hongera kwa safari nzima ya kujitoa kwako katika kuwa mtu bora siku hadi siku unapokuwa wajifunza, wachukua hatua na pia kupata matokeo. Nafasi hii ya sisi kuwa wazima tumshukuru Mungu na si ya bure, ni ya maana kubwa sana tukifahamu pia hatunayo wakati wote. Hivyo kujifunza na kuchukua hatua ni mambo yanayotakiwa kwenda …

363; Kifurushi Cha Maarifa 02

Kuna mahali umewahi kufika ukakwama na pengine ukaona hakuna jinsi ya kutoka. Ukikaa na kufanya tafakari ukarejea wakati ule ambao ulikwama basi kukwama kule kuna mapungufu fulani ya maarifa yalikuwepo. Maarifa sahihi ni sawa na mwanga katika giza nene katika kutofahamu kwetu kwa mambo. Kwa kuwa wakati mwingine hatuweki juhudi kubwa kutafuta maarifa basi kuna …

362; Uchambuzi wa kitabu, Blessed in the Darkness, How All things Are Working For Your Good by Joel Osteen ( Kubarikiwa nyakati ngumu, Namna Mambo yafanyikavyo kwa uzuri )

Tunapofikiria kwa habari ya baraka, mara zote huwa tunafikiri juu ya mambo mazuri yanayotokea katika maisha yetu ya kila siku. Pengine ni kupandishwa cheo, kupata kazi nzuri, kufaulu masomo, kupata mke au mume, au kupata watoto. Hizi nyakati ni nzuri sana na hapo ndipo tunapoona kuwa baraka huenda sambamba na mambo mazuri yanayotutokea au tunayoyapata …

361; Duka la Maarifa, Hujachelewa kuanza kusoma vitabu

Habari Rafiki, bila shaka waendelea vizuri kabisa katika safari ya kuchukua hatua. Maisha yafaa kwenda hatua kwa hatua na hapa ndipo maisha tuonavyo yakibadilika siku hadi siku. Hata kama maisha yatakuwa vile ambavyo hukutegemea yawe bado ukiwa na nafasi ya kuwa hai una nafasi ya kuwa bora na kujifunza na kuchukua hatua kisha ukapiga hatua. …

360; Kifurushi Cha Maarifa.

Dunia inaenda kwa kasi sana, mambo yanabadilika kila kukicha, maarifa ya miaka michache ilopita leo yanaweza kuwa yashapitwa na wakati. Hivi ndivyo kasi ya dunia iendavyo zaidi ya vile jitihada za watu wanazofanya nao wabadili namna ya kufikiri. Kwa mtu aliye mwonaji na mfuatiliaji wa mambo yaendavyo ataoana ni kwa kiasi gani twahitaji juhudi kubwa …

359; The thank them now exercise ( Washukuru sasa, wakati ni huu)

Habari ya siku mpya. Bila shaka ni siku mpya kwako na kama umepata nafasi ya kusoma huu ujumbe basi shukuru kwa nafasi ya kuwa hai mpaka sasa kwa Muumba. Hii ni nafasi ya kipekee sana kuishi katika kusudi kubwa ambalo ndilo jambo kubwa la uwepo wetu duniani. Nafasi ya kazi hizi tatu ni muhimu sana …

358;The Protective Filter Exercise ( Chuja Habari Katika Siku yako )

Habari Rafiki, bila shaka siku imeanza na wakati mwingine tena wa kutumia nafasi hii ya kipekee ya uzima. Nafasi hii ya uhai ni kubwa sana na ya kuitumia vizuri sana katika safari ya kuwa mtu bora na kuchukua hatua kila siku, huenda ikawa ni kazi katika kuchukua hatua lakini hakuna namna ya kufanya kama si …

Design a site like this with WordPress.com
Get started