421; KURUNZI ya MAARIFA, Somo kubwa la kiroho kuhusu fedha na nishati tano ulizonazo za kufanya ufikie MAONO yako makubwa na HATUA ya KUCHUKUA.

Kitabu nilichosoma; THE ENERGY OF MONEY, A Spiritual guide to financial and personal fulfillment by Maria Nemeth, PhD ( NISHATI ya FEDHA, Mwongozo wa kiroho wa utoshelevu wa kiuchumi na maisha binafsi ) Rafiki karibu tena katika safari yetu ya maarifa na kujifunza kila siku. Kwanza kabisa tumshukuru Mungu kwa nafasi ya uzima na mpaka …

420: ACHA ALAMA; Fanya mambo madogo madogo tu kila siku ya kuleta ubora katika Dunia.

Maisha ni muunganiko wa mambo madogo ambayo yakiunganishwa ndio huleta thamani ya maisha au kitu husika. Na katika kila udogo wa kitu au jambo ndipo ulipo ukuu na ukubwa huzaliwa hapo. Unapomwona mzee kuna siku ambazo alikuwa ni mtoto mdogo, ukiona mavuno ya mazao ujue kuna siku ambazo kulikuwa mbegu peke yake. Na hata ukiona …

419; Faida ya kuchukua hatua; Mawazo huru 5 kutokana na zoezi la kuandika mawazo 10 kila siku ( Idea machine, idea muscle and idea rule )

Habari ya jioni, je wajua kuwa kwa siku karibu zaidi ya mawazo yasiyo pungufu ya 100 huwa yanatujia lakini kwa kukosa kuandika basi tunapoteza huu mtaji ambao tukifanyia mchakato basi kuna hatua ya kimaisha tutasogea zaidi. Katika zoezi hili la kuandika mawazo 10 kila siku kwa mwezi yanakuwa mawazo 280 na kwa mwaka yanakuwa mawazo …

418; Mbinu za Uchambuzi Vitabu, KITABU ~ WHAT MAKES THE GREAT GREAT, Strategies for Extraordinary Achievement by Dennis P. Kimbro PhD

Mambo 10 niliyojifunza kutoka katika kitabu hiki chenye tafsiri ya KITU GANI KINAWAFANYA WAKUU WAWE WAKUU na Mwandishi Dennis P Kimbro kikigusa mikakati imara ya kukufanya ufanikiwe zaidi kuelekea kufanya mambo makubwa katika maisha na kuacha alama nzuri ya maisha yako. Zawadi ya kwanza kabisa katika maisha ni kuwa na UHAI na katika kuwa HAI …

417; Ukiona watu wamefika mbali na wako juu usisahau kuwa wametoka mbali na siku walikuwa chini

Leo ni zawadi, zawadi ya siku na zawadi ya uhai ya kumshukuru Mungu, leo ni siku ya ushindi na umezaliwa kushinda, leo ni siku mpya ya kufanya kitu isipite bure, usiipoteze na kuacha ipite tena kwa kughairisha jambo la kuanza, kuchukua hatua na kuzalisha matokeo. Ni leo pekee ambayo unayo katika umiliki wako, jana imekwisha …

416; Tafakuri ya siku, Fikiri kuwa hata wewe yanaweza kukupata

Habari ya siku mpya, masaa mapya na siku ya ruhusa ya wewe kwenda kufanya makubwa au uache ipite tu hujafanya kitu au kuchagua sababu na visingizio. Leo ni siku ya ushindi na umezaliwa kuwa mshindi, wewe ni shujaa na ajabu kubwa kuwa Mungu kaweka nguvu kubwa ndani yako, ndio kuna uwezo ndani yako umelala ni …

415; HATUA ya KUSHITUKA; Kama utashindwa kuyarekebisha haya maeneo 5 kwa chochote kile ufanyacho iwe ni biashara, kipaji, maono makubwa ulonayo jitabirie anguko kubwa siku zijazo.

There is no business that fails overnight; it always takes time and go through a process ~ Olumide Emmanuel ( Book, The School of Money, 346 page ) Habari rafiki, kila siku mambo yanabadilika hii ni habari njema sana kwa suala zima la maendeleo na wakati huo huo tena ni habari mbaya pale ambapo watu …

414; HATUA ya KUSHITUKA, upanga unapewa sifa ya ubaya sababu ya aliyeshika upanga. Huyu ndiye anayekuzuia usifanikiwe na usitake kushituka kuanza

A sword never kills anybody; it is a tool in the killer’s hand ~ Epictetus Rafiki tujikumbushe tu maisha ni darasa na kila siku linatupa nafasi ya kujifunza kama tutajitoa kweli kujifunza. Leo utakutana na hili na kesho lile na hivyo ndivyo maisha huenda na hii ndio sababu kuwa unahimizwa sana uwe unapata maarifa kila …

Design a site like this with WordPress.com
Get started