Rafiki leo ni makala yangu ya 500 toka nimeanza kuandika na kuwa na utaratibu mzuri wa kuandika. Asante kuwa rafiki yangu maana wewe ndiwe umenipa sababu ya kuandika na nisiache kuandika hadi siku utakaposikia sipo. Kuandika ni kazi ngumu lakini huwa nyepesi ikiwa wafanya kama sehemu ya maisha yako na siku utakapoondoka waje wafaidike wengine …
Monthly Archives: December 2018
499; Jamii 100, Tabia pekee ambayo unaweza kuijenga kwa mwaka 2019 itakayokupa hatua kubwa basi ni USOMAJI VITABU na kufanyia kazi.
Rejea ya kitabu; WISDOM by Elijah Mwape ( HEKIMA ) Habari Rafiki naamini siku yako imekuwa bora na mwaka ndio waishia hivyo na ikiwa nafasi nyingine itatokea basi kuamka kwa siku nyingine basi itakuwa ni mwaka 2019 na si huu mwaka tena. Kuwa hai ni fursa maana ukitazama nyuma ni wengi hawapo ila wewe upo …
498; NJIA ya KUTOKA, Kama unamiliki simu janja una kila sababu ya kupiga hatua labda kama huoni fursa.
Maandishi haya ni muktadha wa nchi yetu zaidi ( sisitizo ) Habari Rafiki ikiwa katika siku chache kabisa za kumaliza mwaka ni wasaa mzuri sana wa kuangalia ulikuwa wapi na upo wapi na wapi uendako. Maisha yanaenda kwa kasi sana na vile unasema kesho utafanya unakuta mwaka umeisha kama hivi. Kama u hai bado nafasi …
497; Falsafa 100, Ustahimilivu wa akili na mwili kama silaha katika nyakati ngumu za maisha na kuyaendea mafanikio.
Kila siku maisha yanatupa nafasi mbalimbali za kujifunza katika sisi wenyewe, mazingira na hata wengine. Kama si ugumu ambao tunapitia sisi basi kuna wengine wanapitia magumu na kupitia wao tunaweza kujifunza mengi kabla kuwa zamu yetu kama wao. Ustahimilivu ni silaha katika maisha ambayo tunaishi iwe katika nyumba, jamii, taifa hadi Dunia kwa ujumla wake. …
496; Falsafa 100, Maisha yetu katika sura ya MKOPO na Maarifa yatakuwa ngao kwako katika siku za kuishi kwako Duniani.
Rejea ya kitabu; STOICISM, Ultimate Handbook to Stoic Philosophy, Wisdom and Way of Life by Thomas Beckett. ( USTOA, Kitabu cha Falsafa ya Kistoa, Hekima na Njia ya Maisha ) Uwepo wetu wa kuishi Duniani ni wa muda mchache kuliko urefu wa asili iliopo ambayo imekuwa tangu kale. Asili na vilivyomo vimekuwa na urefu wa …
495; ZAMA TUISHIZO,Teknolojia ni fursa ya kukuza uchumi kwa muda mfupi ikiwa kila mmoja ataona hivyo. Rejea ya kitabu
Rejea ya kitabu; THE ENTREPRENEUR MIND by Kelvin Johnson ( FIKRA za MJASIRIAMALI ) Teknolojia hasa ya mawasiliano imefanya maisha yawe rahisi zaidi kuliko zama nyingine zote ambazo binadamu kawahi kupitia na huenda zikawa zama pekee ambazo zitafanya biashara nyingine zikue haraka na nyingine zife kabisa. Mbali na nguvu ya teknolojia ya mawasiliano ilivyo katika …
494; TAFAKURI ya MAISHA, Kila wakati tunahimizwa kufanya mambo kama ndio nafasi pekee ikipita hatutapata tena kuifanya.
Habari Rafiki yangu, siku zinaenda na kama majira ya saa ni saa zaenda dakika lala salama. Mwaka unaishia na wakati huo huo nayo maisha yanapungua na kuongezeka kila siku. Nguvu zetu za miaka ya nyuma huenda zisiwe sawa na huko tuendako na hivyo hitaji la kutunza nguvu na muda ni la msingi sana kwa maisha …
493; DUKA la MAARIFA, ONGEZA IDADI ya WATEJA WAPYA KWA NJIA 22 na TUMIA NJIA HIZI KUKUA KIBIASHARA MWAKA 2019. Rejea ya kitabu INSTANT CASHFLOW by Bradley J. Sugars Biashara bila kuwa na wateja ni anguko l
Biashara bila kuwa na wateja ni anguko la kibiashara. Wateja ni sehemu ya uhai wa biashara yako mbali na maeneo mengine makubwa mawili ambayo ni faida na mapato. Ili biashara yako iwe na uhai lazima mambo 3 haya yawepo vizuri kuwa lazima pawe na wateja, faida na mapato ya biashara. Kila mmoja kwa wakati tofauti …
492; DUKA LA MAARIFA; Siku 20 katika makundi 5 ya vitabu muhimu kuanza navyo kwa mwaka 2019
Habari Rafiki yangu, Tukiwa katika kumaliza mwaka na kutegemea panapo nafasi basi mwaka 2019 ubishe hodi katika maisha yetu. Nimekuandalia programu ya maarifa kwa faida ya pamoja kuona wapi twapaswa kufika. Muda unaenda na siku zinaenda kila siku. Pale utakapokuwa umeghairisha mambo yako basi muda hausubiri mtu unazidi kwenda mbele. Kibaya ni kuwa muda unaweza …
491;MCHEZO wa NDANI wa MAISHA ( Inner Game of Life ) ndio ngazi unayopaswa kuwa ili ufanikiwe kama wengine walivyoweza kufanikiwa
Dunia inaongozwa katika ngazi 3 za uhalisia ( 3 levels of realities ) na katika ngazi hizi 3. Ngazi ya 1 ndio yenye watu wengi zaidi na jinsi ngazi zinavyoweza kupanda ndivyo watu wanavyozidi kupungua katika hizo ngazi na ifikapo ngazi ya 3 inabaki na watu wachache ambao ndio hufanya makubwa na maisha yao. Ngazi …