490; BARUA ya 5, Siku ukiwa katika kifungo kumbuka una hiki kitu kitakusaidia kuwa huru Katika maisha yetu ya kila siku huwa h

Katika maisha yetu ya kila siku huwa hatuna kinga ya kila kitu ambayo inaweza kuzuia baadhi ya mambo ambayo hutokea na kutupata. Kuna mambo ambayo hutokea na tukajiuliza namna ya kutokea kwake na mwisho kama utaenda kwa kina unaweza kuyaweka katika makundi mawili. Moja ni kuona kama yako katika uwezo wako na kama sio basi …

489; BARUA ya 4, Hii ndio zawadi pekee nayotakiwa kuacha kila siku za maisha yangu

Kuna wakati katika maisha umewahi kupokea zawadi na pale ambapo ulipokea ulijihisi vizuri sana. Zawadi ni ishara ya upendo na akupaye zawadi anaonyesha kujali na kujali ni moja ya mambo ya sifa njema ya watu walio watoaji hata kama si fedha bali hata muda au tabasamu. Zawadi ni nzuri sana na katika zawadi hizo zote …

488; BARUA ya 3, Maisha katika upande wa makali ya upanga

Upanga una makali ukijisahau ukaacha kushika katika pa kushikwa basi utakaposhika ni katika makali utakatwa. Makali ya upanga ni silaha ya vita na hata wapiganao hujitahidi zaidi kuonyesha upande wenye makali maana ndiko ushindi ulipo. Maumivu yake ni makali ya ukali huu wa upanga. Kuachana na hayo nini maana ya maisha katika upande wa makali …

487; BARUA ya 2, Kila kizazi kina nafasi ya kwenda hatua zaidi ya walokwishakuwepo na vivyo hivyo nafasi ya kuharibu zaidi ya walokwishawahi kuishi

Siku moja nikiwa katika pita pita zangu nikaonana na watu walokuwa katika kijiwe jinsi ambavyo walikuwa wakisemea makosa mengi ya watu walokwisha kupita na kulaumu namna gani wamesababisha maisha yao kuwa mabaya. Ukienda haraka haraka unaweza kuona hawa watu wako sahihi asilimia zote na ukaona kweli kabisa walokwisha kuwahi kuishi wamechangia tulipo hasa katika ubaya …

486; Barua ya 1, Usitupe Kalamu yako, SAFARI ya Kilele cha Makala ya 500 toka nianze kuandika.

Rafiki/ndugu upendaye kujifunza kila siku karibu katika safari ya barua ambazo nitakuwa naandika Figa la Ushairi juu ya maisha, uzoefu na yale ambayo nitakuwa najifunza katika maisha na kuyaendea kuchukua hatua. Namshukuru Mungu pale ninapoamini kuwa haba na haba hujaza kibaba na ndivyo ambavyo nilivyoanza kuandika kwa njia ya jukwaa la mtandaoni na sasa kukaribia …

485; Jamii 100, UTALII wa VIWANDA ( Industrial Tourism ) Utalii ni se

Utalii ni sekta yenye tija katika maeneo mengi Duniani. Ni sekta yenye kuingiza mapato makubwa kwa eneo husika au nchi. Utalii ni sehemu ya kujifunza na kuziona fursa ambazo usingeziona kama si kwa njia ya utalii. Utalii ni kazi bora kwa wanahistoria, wafanyabiashara, kila mtu mpenda kujifunza na hata waandishi ili kujifunza na kuhifadhi uzuri …

484; JAMII 100, Falsafa, Asili na Vitabu vya Dini vinajua namna mafanikio makubwa yanahusiana moja kwa moja na moyo ulojaa shukrani hupata zaidi katika maisha.

Rejea ya kitabu; The SCIENCE of GETTING RICH, Attracting Financial Success through Creative Thought by Wallace D Wattles ( Sayansi ya kupata Utajiri, Kuvutia mafanikio ya kifedha kupitia mawazo bunifu ) Moyo wenye shukrani hujaa utoshelevu na furaha siku zote. Moyo wenye shukrani haukosi kupata zaidi katika maisha. Asili ndio mwalimu wa kwanza aonekanaye namna …

483; JAMII 100, Unapoukumbuka mwili na roho usisahau kuwa akili hulishwa kama ilivyo roho na mwili hulishwa

Rejea ya kitabu; The SCIENCE of GETTING RICH by Wallace D. Wattles ( Sayansi ya kupata Utajiri ) Habari rafiki na mpenda kujifunza mambo mapya kila siku. Kama ulikuwa hujatambua kuwa katika maisha yetu ya kila siku tunaenda kujishughulisha katika kazi, vipaji na biashara zetu ili tuweze kuulisha mwili, roho na hata akili zetu. Mbali …

482; JAMII 100, Kitabu hiki kiwe katika moja ya vitabu vyako 100 utakavyokuwa unavisoma kila siku za maisha yako. Kitabu; The Sc

Kitabu; The Science of Getting RICH by Wallace D. Wattles ( Sayansi ya kuwa Tajiri ) Habari Rafiki. Ni siku mpya, mwezi mpya na mwezi wa mwisho kwa mwaka 2018. Huu ni mwezi wenye fursa nyingi na kama watu hawatakaa vizuri ni mwezi wa kupoteza kile ambacho kwa mwaka mzima umekuwa unakipigania. Kuwa hai na …

Design a site like this with WordPress.com
Get started