528; January 31, Changamoto yako ni ndogo kama ungejuwa wanazopitia watu wengine.

Moja ya ahadi ambayo nilokuwa nimejiwekea mwaka huu 2019 ni ya kujisukuma kila siku kuandika katika wakati ambao naona ni wakati mgumu kuandika. Wakati huu unaweza ukawa na sababu za kutosha kabisa kuwa kwanini usipumzike na kisha ungoje siku nyingine ?. Lakini hili nimelikataa na kusema nitakuwa naandika hivyo hivyo na kuona huwa inakuaje kuandika …

527; January 30, Akili imezoea kuzurura idhibiti

Habari Rafiki ni siku nyingine ambayo ni zawadi tumepata kuitumia ili tuweze kupiga hatua kubwa na maisha yetu na wale wanaotuzunguka. Zawadi ya kuwa hai ni zawadi kubwa ambayo kama ingekuwa inanunuliwa basi wengi wangeweza inunua lakini haiko hivyo. Mshukuru Mungu kwa nafasi hii na kuitumia katika kujifunza na kusaidia wengine kwa ulivyojaliwa ni njia …

526; January 29, Kila unachokitaka lazima ulichonacho ukipoteze

Habari Rafiki naamini kila siku kwako unaipa uzito kama vile ni siku ambayo ikipita imepita huwezi kurudia tena kuishi. Kila siku ni fursa ya kujifunza vitu kwa kina na unajiona kadri unavyoendelea kuishi unagundua kumbe vitu ulivyokuwa unavijua kwa undani kumbe hujui kwa kina. Hili linatokea na ndilo ambalo linatupa nafasi ya kuwa hitaji la …

525; January 28; Dhibiti hasira zako ufanye maamuzi sahihi

Hasira ni hisia kali ambayo wengi wanaoshindwa kuidhibiti basi huwapelekea kufanya maamuzi ya ovyo. Kwa kuwa wakati ijapo hasira uwezo wa kufikiri hushuka na hisia huwa juu kufanya maamuzi. Mara zote ambapo hisia huwa juu basi kufikiri huwa chini na hapo maamuzi yote yafanyikayo huwa yana majuto baadaye. Hasira ni kupata kurukwa na akili kwa …

524; January 27, Usipofushwe na mwonekano wa nje wa watu ushindwe kuona uhalisia wa watu ulivyo na maamuzi ya kundi kufanya unavyofikiri kunaweza kukuondoa katika uhalisia.

Rejea ya Maarifa; The LAWS of HUMAN NATURE by Robert Greene ( SHERIA za ASILI ya BINADAMU ) Mara nyingi tumekuwa tunapotea kabisa kuona uhalisia pale ambapo watu wanaoonekana kwa mwonekano nadhifu na tabasamu kuonekana ni watu ambao tunaweka imani kwao haraka zaidi kuliko ambao mwonekano wao si nadhifu. Tumeona wazi wazi vile hata watu …

523; January 26, Unachofikiri ni tatizo sio tatizo ila tatizo kubwa ni wewe

Habari Rafiki naamini unaendelea na hatua zako bora sana. Kila siku tunapoteza sehemu ya maisha yetu, nguvu zetu na kingine umakini wetu. Rasimali kama nguvu ni kuhifadhi sana kwa kuepuka habari hasi na watu wanaokatisha tamaa. Huku umakini unaulinda kwa kuilinda akili yako isitoroke toroke kwa kujua ambacho unakifanya kwa wakati huo. Ukiweza kuhifadhi rasimali …

522; January 25, Utafanikiwa kama utaendelea kuwa mwanafunzi wa maisha

Leo imekuwa siku bora sana nikiwa bado naendelea kujifunza mengi katika safari ya maisha. Moja ni vile ambavyo tuna siku zisizo nyingi za kuishi kwa kuona baadhi ya watu wakiondoka kama majani juu ya mti lakini huu ndio uhalisia ambao haukwepeki na jambo la pili ni juu ya maisha ya maana na bora. Maisha ya …

521; January 24; Jua Vichache ila kwa kina

Habari Rafiki naamini unaendelea vizuri na hatua zako za kila siku. Kujifunza ni hitaji muhimu kwa mafanikio kama vile damu katika mwili basi kujifunza na kufanyia kazi ndio msingi katika safari ya mafanikio. Kadri unapojiwekeza ndani yako kwa maarifa ndivyo na wewe unavyozidi kufupisha njia yako kuelekea hatua kubwa za maendeleo. Ishukuriwe nafasi ya teknolojia …

520; January 20, Kiwango chako cha kufanikiwa kipo katika utatuzi wa matatizo ya jamii.

Habari rafiki naamini kila siku kwako huwa unaipa uzito kama vile ikishapita haitakuja kuwa tena hivyo. Kila siku huja na kupita na muda na nguvu zetu kimoja huwa hatuna siku zote. Nguvu zetu zinaenda zikiisha kila siku na kiwango cha uthubutu wetu huwa hakiwi sawa na vile ambavyo mtu akiwa kijana au alivyokuwa mtoto. Hivyo …

519; January 19, Jamii 100~ KITABU;The Power of Creative Intelligence(Nguvu ya Akili bunifu) by Tony Buzan.

Ubunifu ni uwezo wa kuandaa na kuleta wazo jipya, kutatua matatizo katika namna halisi yenye upekee na kuonekana mbele ya jamii kwa kile unachokifanya. Mwandishi anaelezea namna ubunifu unavyoweza kukufanya ufanikiwe zaidi anatupa mbinu mbalimbali ambazo tukizitumia tutafanya mambo bora Kama alivyofanya Leornado da Vinci ambaye ni mfano bora kabisa kwetu. Mambo ambayo nimejifunza katika …

Design a site like this with WordPress.com
Get started