559; Kitabu mwezi wa 3, Uchambuzi kifupi; The RETAIL DOCTOR’S, A Guide to growing your Business by Bob Phibbs ( Mwongozo wa kukuza Biashara yako )

Rafiki karibu tena katika kitabu chetu cha 3 kwa kina kila tunapokaribia mwezi mpya kuanza. Kwa miezi miwili ilopita Januari na Februari tuligusa vitabu viwili kimoja kiligusa juu ya kukabiliana na kujidhibiti hasira katika maeneo ya kazi na kingine juu ya mtu kama Mfalme wa fikra, roho na mwili wake mwenyewe. Na kitabu cha mwezi …

558; February 28, Maamuzi yote nitakayofanya nikiwa na hasira yatakuwa ya ovyo na kujichelewesha kuchukua hatua nikiwa na hasira ni ukomavu.

Hasira ni nguvu na ikishindwa kudhibitiwa ina uwezo wa kumfanya mtu apate kurukwa na akili kisha akaamua pasipo kufikiri na maamuzi yake mengi huwa ya ovyo na majuto baada ya tukio lilofanywa na hasira. Hasira hukaa kifuani mwa mtu mpumbavu na anayeshindwa kudhibiti hasira ni mtu kushindwa kushika hatamu ya hisia zake na matendo. Matokeo …

557; February 27, Nitakapoweza kuipa uzito kauli ya niishi leo kama siku yangu ya mwisho nitafanya mambo makubwa Duniani.

Moja ya sababu kubwa ya hofu ya kifo ni kuwa maisha yetu hatuishi kitoshelevu na tunaishi kana kwamba kesho zitaendelea kuwepo. Pale ambapo tunaona wengine siku kama hii hawapo na walikuwepo basi ni dhahiri kifo nasi kitabisha hodi siku moja. Kufahamu hili katika uwazi basi latupa himizo la kuishi sasa, la kushughulika na maisha yetu …

556; February 26, Vuta subira mengine unayopitia hujipembua yenyewe kadri muda uendavyo utaelewa sababu ya kutokea kwake.

Kuna mambo yalopita unaweza kuyaelewa sasa kwanini yalitokea na yepi ambayo umejifunza kwayo. Na huenda kwa wakati ule hukuweza kuona hilo sababu binadamu ni hulka yake kuona karibu kuliko kuona mbali na kutamani vya mbali na kuvipuuza vya karibu. Subira ni ukomavu na hutaka utulivu mkubwa hasa katika mambo yagusayo moja kwa moja hisia zetu. …

555; February 25; Msingi wa fedha ni thamani na nguvu ya fedha yapaswa kudhibitiwa lasivyo inaweza kukuharibu

Fedha ni thamani na kila unapokuza na kuongeza thamani kupitia ufanyacho ndivyo unavyoweza kutengeneza fedha zaidi. Pale unapozipata hupati tu fedha kama fedha ila fedha kama nguvu ya kufanya vitu vilivyokuwa kazi kupatikana vipatikane. Fedha ni nguvu na hii nguvu iletwayo na fedha ndio kiini cha mazungumzo yetu leo. Fedha ni nguvu inayokupa uone majibu …

554; February 24, Nitakavyokuwa naweka muda wa kujifahamu kwa kina basi njia ya kufahamu maisha kwa kina itakuwa nyepesi.

Lengo kuu moja kubwa la maisha na siku zote za uhai wetu ni kufahamu jinsi tulivyo na kujua kwa kina umaana wa kuishi kwetu tunaishi kwa sababu gani. Toka utoto hadi siku ya umauti ni katika safari hii ya kugundua mengi yalokuwa ndani yetu ila kwa kadri tuishivyo yanajidhihirisha kidogo kidogo hata kufika utoshelevu. Safari …

553; February 22, Nikitumia mitandao ya kijamii au vyombo vya habari kama rejea ya kupima mambo nimekubali kutopata uhalisia wa mambo ulivyo.

Kile kinachooneshwa au kutangazwa au kuandikwa kupitia vyombo vya habari au mitandao ya kijamii ni sehemu ndogo ya uhalisia wa vitu vilivyo. Na ni makosa makubwa ninapoweka akili kutumia kama rejea ya kujua mambo kwa kina. Kile kinachoonekana si ilivyo nyuma ya hicho kitu na ukitegemea kama kilivyo unaruhusu matatizo na upotevu muda wa kitu …

552; KURASA 10 kila Siku, Uchambuzi wa Kitabu ~ HAPPINESS for HUSBANDS and WIVES by Harold Shryock ( FURAHA kwa WAUME na WAKE )

Kitabu kizima; 272 kurasa Nakala ngumu ( Hard copy ) Kurasa; (17 ~ 29 ) Uchaguzi wa mwenza wa Maisha. Imekuwa inajulikana kuwa moja ya matukio muhimu kwa maisha ya mtu ni kuzaliwa, ndoa na kifo. La kwanza na la mwisho hakuna ambaye huwa ana uwezo nayo kuyazuia au kutaka yawe atakavyo kuliko la pili …

551; February 21, Ili nipate nitakacho lazima nivivuke vikwazo na maumivu kati kati ya mchakato.

Ili tupate chochote kile kizuri na bora huwa tunatenganishwa na vikwazo na maumivu ya jinsi ya kukipata. Tukitaka mwili mzuri lazima tuvuke maumivu ya misuli na tuendelee mbele kati kati ya vikwazo ili miili tutakayo ije. Na hii sio katika mwili pekee hata maisha ya mafanikio lazima kushinda vikwazo na maumivu kati kati ya mchakato. …

550; KURASA 10 kila Siku, Uchambuzi wa Kitabu ~ HAPPINESS for HUSBANDS and WIVES by Harold Shryock ( FURAHA kwa WAUME na WAKE ) Kitabu kizima; 272 kurasa

Kitabu kizima; 272 kurasa Nakala ngumu ( Hard copy ) Kurasa; (5 ~ 16 ) Ndoa ni sehemu ya maisha na ni ngazi ya mahusiano ilo juu zaidi ya ukaribu mkubwa wa kihisia baina ya watu wawili ambao wamejitoa kusafiri pamoja wakiwa na nia ya ujenzi wa taasisi moja kubwa ya mahusiano. Mafanikio na furaha …

Design a site like this with WordPress.com
Get started