Kuongea ni rahisi na kila mtu anaweza kuongea atakavyo lakini si sawa katika kufanya hapo wapo wachache sana. Kufanya ni kazi nzito na yataka ujisukume haswaa na kufanya hakutaki maneno ila matokeo. Bila kufanya hakuna mabadiliko na Dunia haisubiri wenye maneno tupu ila inawapa nafasi watendaji na ambao wako tayari kuziendea hatua juu ya maisha …
Monthly Archives: February 2019
548; February 19, Maisha ni zawadi na kila siku tuamkapo tushukuru kuwa na hii nafasi ya kuwa hai.
Jambo tunalopaswa kutambua kila siku ni kuwa maisha ni zawadi. Uhai ni thamani ya uwepo wetu na hii nafasi ni ya pekee na kama tutakosa shukrani basi tunakosa kutambua kuwa hii nafasi ni ya ukomo na haipo sehemu huuzwa ikishapotea. Kuamka katika kuipokea kwa furaha na shauku ya kuwahudumia watu wanaotuzunguka ndio umaana wa kuwa …
547; February 18, Kila kitu kitabadilika nikibadilika kufikiri na kuanza kuchukua hatua.
Mafanikio ya kweli huanzia ndani na huko ndani yanaenda kugusa mfumo mzima wa kufikiri. Pale kufikiri kukibadilika basi mambo yote nje nayo yanaitikia mabadiliko toka ndani. Vile mawazo chanya nitakavyoruhusu yawe na himaya ndani ya fikra zangu ndivyo urahisi wa mambo yote nayotamani kuona yakibadilika nitayaona wazi wazi. Iwe ni kazi, mahusiano, maisha, kipaji, maono …
546; February 17, Nguvu zako zipo katika utulivu
Jinsi ambavyo Dunia inavyozidi kuwa bora na kuwa kijana ndivyo usumbufu unavyozidi kuongezeka na utulivu kuwa bidhaa adimu kupatikanika. Kila siku watu wako na pirika pirika ambazo zinawanyima hata muda wa kutulia kisha wakapima katika pirika zote hizo je wanapiga hatua ? au wamekwama. Maana si shida kuwa na pirika pirika nyingi ila ufanisi ndicho …
Continue reading “546; February 17, Nguvu zako zipo katika utulivu”
545; February 16, Mafanikio ya kweli sio tukio ni mchakato wa hatua ndogo ndogo za kila siku endelevu
Watu wengi huvutika na matokeo ya kitu na hupofushwa wasione matokeo hayo yamezalishwa na nini. Kuona matokeo pekee hutaweza kuona uhalisia wa mambo na hivyo utakosa maana sahihi ya mafanikio ni nini?. Kwa kuwa matokeo huvutia sana ndo maana wengi waanzapo na maana ya mafanikio kama matokeo waanzapo safari na kisha kuona kisicho huishia njiani …
544; February 15, Kuna adui ndani yako zaidi ya ulimi na huyu ndie anayekukwamisha mambo yako.
Tumekuwa tunasoma na kusikia mengi juu ya nguvu ya ulimi ilivyo na athari zake pale unaposhindwa kudhibitiwa. Licha kuwa ulimi umekuwa umepewa uzito kuwa watu waudhibiti ili waweze kudhibiti maisha yao basi kuna zaidi ya ulimi kile kinachopaswa kudhibitiwa maana ndicho kinachokwamisha wengi wakwame na wasipige hatua na maisha yao. Naona unayo shauku kubwa ya …
543; February 14, Kila eneo utakalo kuwa mgeni tafuta mtu aliye mwenyeji.
Maisha ni sawa na safari ndefu sana yenye kukaribisha mambo mageni yenye kutupa kufahamu juu ya uhalisia wa mambo ulivyo. Ugeni una gharama nyingi ukiangalia kwa kina. Sababu ya ugeni wengine hukosea na hata kufanya mambo ambayo wazi wazi yanaonyesha ugeni wao ulivyo na unaonekana na wengine. Ugeni sio kosa katika safari ya kujifunza mbali …
Continue reading “543; February 14, Kila eneo utakalo kuwa mgeni tafuta mtu aliye mwenyeji.”
542; February 13, Changamoto ifanye kuwa malighafi na ladha ya Maisha ipo katika ugumu.
Just as nature takes every obstacle, every impediment, and works around it — turns it to its purposes, incorporates it into itself — so, too, a rational being can turn each setback into raw material and use it to achieve its goal. – Marcus Aurelius, Meditations Kama ilivyo asili kuweza kubadili vikwazo na kufanya kwa namna yake. Ndivyo ilivyo kwa kiumbe …
541; February 12, Mambo yakikwendea vibaya kumbuka mambo mazuri yanayoendelea katika maisha yako
Ni kawaida na hulka ya watu na hata wewe pale unapoingia katika wakati mgumu katika maisha na ukaona kama kila kitu ni kigumu na hukuwahi kuwa na nafasi nzuri na mambo yalikwendea vizuri wakati fulani. Maisha utapitia magumu lakini si wakati wote kuwa mambo yatakaa hivyo ila ni kama tu u mtu mwenye shukrani. Kumbuka …
540; February 11, Kinachokusumbua wewe na wengine ni tafsiri juu ya matukio ya Maisha
“What disturbs people, these are not things, but the judgements relating to things” ~ Epictetus Jioni ni wasaa mzuri wa kuangalia na kuipima siku yako ulivyoweza kuishi. Ukiangalia kwa ubora basi utajipa nafasi ya kujiuliza jambo lipi bora umefanya, jambo lipi umekosea na tatu mambo yepi unatakiwa kuyaboresha ikiwa kesho itatokea. Ukifanya hivi utayaimarisha maisha …