Zama tuishizo zina masumbufu mengi. Hizi ni zama ambazo watu wanajikuta hawana muda na maisha yao wakayaangalia yalivyo nje ndani. Kwa kuwa katika usumbufu huwezi kupata utulivu wa kutulia na ukayaangalia maisha yako kwa kina. Usumbufu wa mitandao ya kijamii, watu, matukio vyote hupoteza ubora wa muda wako wa kuwa peke yako. Utulivu wako ndio …
Monthly Archives: March 2019
586: March 30, Uwezo wa kwenda zaidi ya tulipofika upo ikiwa tutajisukuma kukabili maumivu katika mchakato
Kila rekodi kubwa inayowekwa Duniani iwe katika michezo, maisha au eneo lolote lile basi watu wanaoweka rekodi hiyo wana jambo moja wanalofanana. Uwezo wa wao kujisukuma zaidi kupita kawaida ndiko kunakozalisha hawa watu na Dunia ikawaweka katika historia. Kujisukuma isivyo kawaida huwa kunaambatana na maumivu hasa katika mchakato. Vile uwezavyo kuwa na ustahimilivu mkubwa ndivyo …
585: March 29, Ukikua kiakili na kiroho kuuzidi mwili utaweza kutatua chochote kitakachoweza kukutokea.Mwili ni dhaifu na ndani ya
Mwili ni dhaifu na ndani ya mwili visivyoshikika vina nguvu kubwa kuushinda mwili. Ukikua zaidi ndani yako kiakili na kiroho mwili hata ukiwa dhaifu bado ndani yako utakuwa imara. Mwili huchoka, mwili huumwa, mwili hudhurika. Ila ukiwa na ustahimilivu wa kiakili na kiroho utaweza kukabiliana na chochote hata kama mwili utachoka. Ukiwa imara ndani ni …
584: March 28, Kama kila mtu utamwona kwa jicho la kuwa hafahamu kila kitu basi itakupa kujishusha zaidi kila siku unavyoendelea kujifunza.
Ufahamu ni somo pana lakini ujinga ni zaidi. Kwa kuweka wazi hili basi jipe siku ya kuitazama siku yako kwa kina. Ianze siku yako kama alivyo mtoto akiwa na shauku ya kujua na hata kujaribu. Utaona namna ambavyo watu hata wenye mamlaka nao ni kama wengine katika kutofahamu mambo mengine. Watajua eneo fulani na eneo …
583: March 27, Vitabu vinavyokufanya ukue katika kuona mambo kwa kina ndivyo unavyopaswa kusoma kuyaelewa maisha.
Kuna ngazi 4 katika usomaji vitabu ambazo ndizo zinazotofautisha watu katika kusoma vitabu. Ngazi ya 3 ambayo ni usomaji wa kina ndio ngazi ambayo inaweza kubadili maisha yako na mtizamo wako juu ya Dunia na maisha ya mwanadamu. Ngazi hii hufaidisha msomaji kwa kuwa na vitabu vizuri ambavyo huibua hekima ndani yake na hata kubadili …
582: March 26, Kila kitu tunachokitafuta kipo ndani ya watu na kadri utakavyoweza kuishi vizuri na watu utapata kujua mengi.
Ujuzi pekee ambao huwa hauchuji zama na zama basi ni ujuzi wa kuhusiana na watu katika ngazi tofauti tofauti. Vile unavyoweza kuishi na watu na kuwaelewa jinsi walivyo katika nafasi zao ndivyo unavyoweza kujua kwa kina kuwa kila unachokitafuta hakipo sehemu yoyote ile ila ndani ya watu. Hivyo kauli ile utajiri mkubwa Duniani basi ni …
581: March 25, Dhibiti nguvu inayopotea uitumie kupiga hatua kubwa na maisha yako.
Maisha yetu hubeba uhai pale ambapo nguvu au nishati inapokuwepo. Nishati ya kwanza ni kutokana na chakula ambacho hutupa nguvu. Nishati ya pili ni maarifa kama chakula cha akili. Hii nishati ya pili ndio yenye nguvu kufanya uweze kupiga hatua za juu zaidi za maisha yako. Hisia hasi au taarifa hasi hunyonya nguvu ya mwili …
580: March 24, Usitarajie chochote kile unapofanya jambo na kwa kufanya hivi utaishi kwa furaha siku zote za maisha yako
Ni hulka yetu sisi binadamu kuwa huwa tunasukumwa kufanya vitu ili baadaye nasi tutarajie kupata mrejesho. Ikitokea matarajio ya kile ambacho tulikifanya hayajafika vile ambavyo tuliwaza basi furaha yetu yote inaweza kupotea na tukaingia katika huzuni. Matarajio sana katika maisha kumefanya watu wengi waipoteze furaha kuliko kuwa na furaha. Pale utakapoishi kwa kufanya vitu na …
579: March 23, Kadri ndani yako unavyokua kiroho ndivyo unavyoweza kustahimili chochote kile kinachoweza kukutokea.
Ulimwengu wa ndani ni ulimwengu usio na kikomo na una utele. Mtu ni kiumbe wa kiroho na kadri maisha yake ya kiroho yanavyozidi kuwa ya kina ndivyo anavyoweza kuwa tayari kukabiliana na chochote kile na kisiweze kumwangusha. Maisha ya kiroho ni zaidi ya mifumo ya dini na ni zaidi ya vile watu wafikirivyo. Maisha ya …
578: March 22, Ni kawaida kuchoka upandapo mlima lakini haimaanishi kuacha kupanda mlima.
Kuchoka ni sehemu ya maisha. Tumekuwa tunaona vitu vikichoka na hata mili yetu huchoka. Kuna kuchoka na mwisho kama ni kitu kushindwa kabisa kufanya kazi. Mbali na hilo unapokuja kuyaangalia maisha kama mpandaji mlima utaona kuchoka kupo lakini hakuna maana kuwa ndio mwisho wa safari. Safari huendelea ili kuweza kufika juu palipokusudiwa kufikika. Kujisukuma kuendelea …