607: April 26, Kila unapotaka kuacha ulichokianzisha kumbuka sababu ya kukianza.

Ni rahisi katika maisha kuanzisha vitu vingi na kumaliza hadi mwisho wanaomaliza hubakia wachache. Kuanza ni kama vile unavyokuwa na hamasa siku ya kwanza ya kitu. Lakini kadri siku zinavyokwenda unajikuta hamasa haina nguvu tena bali kinachobakia ni nidhamu pekee yake. Maisha yanataka uwe na nidhamu ya kumaliza ambacho umekianza. Ushindi na pongezi ni vile …

606: April 24, Swali la kitu unalojiuliza ndilo jibu ukiangalia kwa kina.

Katika safari ya maisha si jambo geni unapofikia wakati ambao unakuwa na maswali mengi juu ya vitu, hali na watu. Unaweza ukawa unajiuliza nifanye nini kuwa na furaha, nifanye nini niwe mtu bora au nifanye nini nipate kuona njia. Ukiangalia haya maswali kwa kina yana majibu kwa kila swali. Kuwa na furaha, kuwa bora na …

605: April 23, Siku ya Vitabu Duniani na zawadi moja kubwa unayoweza kuipata pekee kwa kuvisoma vitabu.

Leo ni siku ilowekwa Duniani kote kwa kuhimiza suala la usomaji na usomaji vitabu ikiwa ni jambo la kwanza, uchapishaji na masuala ya hati miliki za kazi za uandishi. Huenda isiwe siku kubwa kama siku nyingine ambazo huhamasishwa na kukumbukwa Duniani kote. Ila kwa aliye msomaji wa vitabu au chanzo chochote cha maarifa basi siku …

604: April 22, Maisha ni mapya ukiacha kuona vitu vilivyokuwa kawaida si vya kawaida.

Mtu aliyezoea kuona mambo kawaida ataendelea kuyaona kawaida hata ambayo si kawaida. Mazoea huua kuona thamani ya kitu na mwisho huficha nafasi ya ubunifu. George Kneller anasema “Kufikiria kibunifu, ni lazima tuache kuchukulia vya kawaida kutokuwa kawaida”. Na hii ndio siri ya maisha pia. Pale unapoona vitu kwa uzito na si vya kawaida basi unafungua …

603: April 21, Maisha ni zawadi na kila siku ni siku mpya.

Kama ambavyo mtizamo juu ya siku ulivyo hasa kama ni siku za sikukuu na kila kitu kuonekana kama kimebadilika basi ndivyo inavyowezekana kuziona siku nyingine kitofauti. Maisha ni zawadi na kila siku ni siku mpya. Ruhusu kuona upya, mtizamo mpya na hatua mpya za matokeo yatakayokupa msukumo mpya. Ishi sasa na nafasi hii ni moja …

602: April 20, Usihitimishe sababu ya wengi wanavyosema bali na wewe jipe muda kuchimba kwa kina.

Ni kawaida ya watu wengi wakiona jambo ni gumu kuling’amua basi wanaegemea upande wa watu wengi wao wanasemaje. Kusimama kwa sababu ya kundi kubwa limesemea jambo fulani haina maana laweza kuwa sahihi au kweli. Ili na wewe ujue ukweli mwenyewe unapaswa kujipa muda huku ukichimba kwa kina kwa kile ambacho unatamani kuona ukikipatia majibu sahihi. …

601: April 19, Ondoa demokrasia unapotafuta kupiga hatua kubwa katika maisha hasa eneo la mwili wako

Unapotamka unataka kufanikiwa au kubadilika tu basi kikwazo cha kwanza ni mwili wako. Utaanza kukupa kila aina ya sababu ili ifike uache ulichokuwa umesema utafanya. Pale unapokuwa umeruhusu demokrasia dhidi ya mwili wako ndipo unaponyang’anywa ushindi wako. Kuna wakati unahitaji upuuze demokrasia unapojadilina na mwili wako pale unapotaka kwenda hatua kubwa maishani au kutengeneza tabia …

600: April 18, Matokeo bora unayotamani upate yatakugharimu na vingi utavipoteza.

Ubora wowote uonao una gharama ya kulipia. Iwe kuanzia vitu hadi hali mbalimbali zinazovutiwa na watu huwa na gharama kubwa ya kulipa. Iwe utajiri, iwe matokeo makubwa ya kazi basi lazima utagharamika kutengeneza yatokee. Utahitaji muda, nguvu, maarifa na kingine utapoteza chochote kisichofaa. Kupoteza hapo ndipo mtihani kwa wengi kutaka matokeo bora na huku hawataki …

599: April 17, Ushindi wako wa chochote utaivuta Dunia lakini kushindwa kwako utabakia peke yako.

Pale utakapokuwa umeleta matokeo bora ya chochote kile maishani basi Dunia itakuwa rahisi kukutambua. Hii imekuwa inaonekana katika michezo, shule, vipaji mbalimbali na masuala mengi ya kiuongozi. Ushindi unavuta watu wakuone na hata wasokujua wakushangilie. Lakini pale utakapoanguka, umeshindwa na kushuka chini utajikuta umebaki peke yako. Jiimarishe wakati wowote ikitokea uko peke yako uendelee kuwa …

598: April 16, Kujua pekee hakutoshi na hakusaidii kama kulivyo kuchukua hatua.

Ni kweli tunaweza kujua mazoezi ya viungo ni muhimu kwa afya zetu, uvutaji sigara ni hatari kwa afya zetu, kughairisha kunaua ndoto zetu, mahusiano ya watu wetu wa karibu ni muhimu lakini bado huwa hatufanyi kile ambacho tunajua ni cha msingi kwetu. Kujua pekee bila kuchukua hatua hakusaidii. Kujua misingi ya kufanikiwa bila kuiishi hakukufanyi …

Design a site like this with WordPress.com
Get started