Mama hubeba uzao na uzao ndio kiini cha maisha ya kizazi kimoja na kingine. Mama hubeba zawadi ya maono, mawazo, ubunifu na biashara zinazozaliwa na uzao ambao hubeba katika ustahimilivu. Furaha na uzalishaji na mwendelezo wa maisha huambatana na sifa hii. Asili hutusitiri na kubeba rasimali zote kwa ajili ya uendelevu wa maisha, kila kitu …
Monthly Archives: May 2019
611: Mei 11, Endelea kujisukuma ili uweze kuona matokeo unayotamani kupata.
Kuna wakati utaamka na kuona siku kama imekuwa na changamoto hata kabla siku kuanza. Wakati huu wengine husema siku ishakuwa mbaya au imeingiwa mkosi. Ni kweli mwili huchoka na unakuwa ukikupa kila sababu ya wewe kuacha kujisukuma kama mwanzo na kujikuta hakuna kitu unachopiga hatua. Hakuna njia ya mkato ambayo utapita kama utakwepa kujisukuma mwenyewe …
Continue reading “611: Mei 11, Endelea kujisukuma ili uweze kuona matokeo unayotamani kupata.”
610: Mei 09, Mtu wa ndani anavyopambana kuliko mtu wa nje.
Maisha huanza kuwa na uhuru pale ambapo utafika hatua ya kudhibiti mtu aliyeko ndani yako. Mtu aliye ndani ndiye amebeba uhalisia wa mtu mzima. Kinacholeta shida si kilicho nje bali ni kile kilicho ndani. Hisia, mawazo yote husababisha matokeo ya nje ya mtu. Ukosefu wa udhibiti wa mtu wa ndani ndipo penye msingi mbovu wa …
Continue reading “610: Mei 09, Mtu wa ndani anavyopambana kuliko mtu wa nje.”
609: Mei 07, Ni muhimu kujua wakati wako ili usije kuona kama uko nyuma unapojilinganisha na wengine
Siku hii moja ina watu wa rika mbalimbali. Wapo walio katika nafasi ya utoto, ujana, utu uzima na uzee. Kila mmoja yu katika wakati wake. Si eneo hili pekee hutokea hivi wazi wazi pia yapo maeneo mengine yenye kufanana na haya. Kila mmoja hupita wakati wake katika kujifunza, kujizoesha na kupata kujua mambo kwa kina …
608: Mei 06: Kuni zinateketea, ongeza nyingine moto uendelee kuwaka.
Ukiwa jikoni kuna ile hali inayovutia sana ya moto wa kuni unavyokuwa unakolea kila unapokuwa unaongeza kuni. Moto kuwaka kunaleta mwanga na kama ni chakula basi kina uhakika wa kupata joto lenye uhakika wa kuivisha kilicho juu ya moto. Vitendo vyako ni kuni ambazo zinachochea moto wako ( shauku, ndoto, lengo, kipaji nk ) ili …
Continue reading “608: Mei 06: Kuni zinateketea, ongeza nyingine moto uendelee kuwaka.”