644; Vitabu 40 unavyoweza kusoma siku utapoona unao utayari kwa kina zaidi.

Habari rafiki yangu. Naamini unaendelea vizuri na hatua zako za kila siku. Maisha ni darasa la kujifunza kila siku na limejaa fursa ya wazi kuamua kipi unachokitaka na maisha yako. Uchaguzi wa kutafuta maarifa kupitia vitabu ili kusaidia kujua kwa kina maisha ni maamuzi bora ambayo utakuja kujishukuru siku zijazo. Katika kupitia pitia kusoma baadhi …

643; Usidharau mwanzo mdogo wa kitu. Kila uanzapo kitu kifikiri kwa miaka 10 ijayo.

Rafiki habari ya siku mpya tena. Leo ni zawadi ambayo wengine hawajapata lakini wewe umeipata kuwa na shukrani kwa Mungu. Nafasi hii ya kuwa hai ni thamani ya juu zaidi ya kiumbe hai. Uhai ukitoka basi kiumbe hupoteza thamani. Zione changamoto zako toka juu kuwa ni ndogo na tumia nafasi ya kuwa hai kujikumbusha nafasi …

642; Nguvu ya kushukuru katika kuvuta maisha ya utele zaidi. Asante wewe unayeendelea kusoma zawadi hii ya uandishi nilopewa nitumie kwa muda.

Mwaka huu 2019 na miezi hii ya Julai na Agosti unakuwa ni mwaka wangu wa 11 toka nimejitambua ndani kuna uandishi na napaswa kuandika siku zote za maisha yangu. Uandishi huu umekua na sasa kufikia umri wa miaka 11 na huenda ukadumu zaidi kuliko nafasi ya mimi kuendelea kudumu katika zawadi ya maisha. Zawadi hii …

641; Mabadiliko ya Dunia huanza na mtu mmoja anayeanza kubadilika na nishati ya mabadiliko ianzapo kusambaa.

Mwaka 1952 huko nchini Japan utafiti mmoja ulifanyika wa kutafiti mienendo ya Nyani. Na utafiti huu ulihusu ulaji wa viazi vitamu ambavyo walikuwa wakilishwa nyani hao. Siku moja palitokea jambo ambalo lilionyesha watafiti kuvutwa umakini wao pale ambapo nyani mmoja alionyesha mienendo ya kitofauti. Nyani huyu alianza kuosha viazi vitamu kabla ya kuanza kula huku …

640;Je kuwa na maarifa mengi ni kikwazo kufanikiwa?

Kujifahamu wewe kwanza ni jambo muhimu kabla hujaanza kuwa na maarifa toka vyanzo mbalimbali. Kushindwa kujifahamu wewe mwenyewe ni rahisi maarifa kukuharibu zaidi kuliko kukujenga. Elimu ya utambuzi au kujitambua ni muhimu katika kumsaidia mtu kuona maarifa kama mwanga na si kikwazo. Mtu ni mjengo wa umbo lake la nje (mwili), utendaji wake (akili) na …

639:Malenga na falsafa: Wajibu wa kuwapenda binadamu wenzetu

Upendo ni nishati kuu inayofanya maisha yetu yaonekane kuwa na maana. Licha himizo la upendo huu bado sisi kwa sisi kama binadamu tunakabiliana na kupishana kwa mitizamo, wengine kuwekeana chuki na wakati mwingine utulivu wetu unavurugika sababu ya mahusiano ya binadamu wenzetu ambao kwa namna moja tunaendelea tunahusiana. Wakati huu wa kupishana mitizamo, uwepo wa …

638; Njia 20 utakavyoweza kuwa sehemu ya maono haya makubwa kwa jamii.

Habari rafiki yangu. Maisha yetu ni mwangwi wa kile kilichomo ndani yetu. Hivyo unavyoona nje basi ndivyo ndani yako ndivyo ulivyo. Hii ni hatua bora sana kama utaweza kutumia vizuri kubadili hali za nje kwa kubadili unavyoona ndani yako. Uwezo huu ndio unafanya jamii zibadilike Duniani kote kwa kuona kwanza ndani na kisha kutokea kwa …

637; Chimbuko la utele ni nguvu na fedha zinatengenezwa kwa kubadilishana nguvu

Fedha ni alama ya nishati bunifu. Na katika sehemu zote Duniani imekubaliwa itumike alama kama karatasi au sarafu kuelezea kiwango cha nguvu hii ya ubunifu. Fedha unaipata kwa kujua mzunguko wa nishati hii inayohama toka umbo moja hadi lingine. Mabadilishano yote ya thamani na yenye kuzalisha fedha ni kusema kwamba unabadilishana nguvu moja na kuhamishia …

636; Ulimwengu wa nje ni kioo kinachotuonyesha jinsi tulivyo ndani yetu.

Ndani yetu kuna nguvu kubwa ya uumbaji ya kutengeneza uhalisia wa nje. Kile tukionacho kwa nje basi kiini cha kutengenezwa kwake basi huanzia ndani. Mabadiliko yote ambayo mtu atatamani ayaone nje basi inabidi yaanzie ndani. Ni kama kioo cha kujitazamia ambacho huonyesha uhalisia wa kitu kama kilivyo. Sisi binadamu tumepewa zawadi kubwa na ya pekee …

635; Nafasi ya wazee kama chanzo cha maarifa na uzoefu wao kwa kizazi kinachobakia linapewa uzito kiasi gani ?

Wazee ni hazina kubwa ya maarifa kwa jamii yoyote ile inayotoa nafasi ya kuona hilo. Kwa jamii nyingine wazee huheshimika wakiwa kama alama ya fahari ya jamii sababu ndani yao wamejaa uzoefu na maarifa tele walopata kujikusanyia kipindi kirefu cha kuishi kwao. Muda na kufahamu mambo huhusiana sana. Na hii ndio huleta ukaribu mkubwa sana …

Design a site like this with WordPress.com
Get started