Miaka 10 ijayo nitakuwa mbali kama nitaamua kuweka kazi kubwa sasa ! – UTAYARI ndio Ada

Kuweka kazi ni kuweka nguvu, akili, muda katika kufanya lengo ulojiwekea ulifikie. Kuweka kazi ni kuwa tayari kukabiliana na kila aina ya changamoto na kusema changamoto hazitakuzuia kusonga mbele. Kuweka kazi kubwa ni kuhakikisha unajikana kabisa na kila aina ya mambo ambayo yatakuchelewesha kule unakotaka kufika. Miaka 10 kuanzia sasa kama nitaweka kazi kubwa katika …

Chagua kimoja na izamishe akili hapo.

Kila siku naiona ni zawadi nayopewa kuishi kitoshelevu. Uhai ni zawadi ya pekee mno nayoshukuru kwa Mungu kila iitwapo leo. Maisha yangu yanakuwa na maana sababu ya uwepo wa uhai. Hivyo kila siku nina kazi moja kubwa nayo ni kuizamisha akili katika jambo moja kila siku nalo ni UANDISHI. Uandishi ni njia moja ambayo naifurahia …

Alama za kudumu za kuiachia Dunia siku tutakapokufa.

Nikukaribishe tena katika safari ya kujifunza, kuishi na kufurahia zawadi ya kuwa hai. Uhai ni zawadi na inapaswa kutumika vizuri mno kila iitwapo leo. Pili ni furaha na utoshelevu wa pekee unapojua au kufanya kitu kinachokubeba moyo na akili zako zote kukifanya. Uandishi kwangu ni utoshelevu mkubwa ambao ninafurahia kila siku katika hii zawadi ya …

Mambo 28 nilojifunza mwezi Julai 2020

Habari rafiki yangu wa kipindi kirefu katika kufuatilia makala mbalimbali kupitia blogu hii toka mwaka 2017. Wewe umekuwa unanipa deni la mimi nisiache kuandika na nijisukume kukushirikisha mengi nayojifunza na kukutana nayo katika safari ya maisha yangu. Miaka 2 ilopita nilikuwa na utaratibu wa kuandika mambo ambayo kila mwezi nilokuwa najifunza. Lile zoezi lilikuwa bora …

Kila kitu kizuri kitakuhitaji uwekeze muda wa kutosha.

Mwezi huu wa saba nilijiwekea zoezi la kujifunza kila siku juu ya asili na nimefanikisha kwa sehemu kujua mengi kuhusu asili. Somo moja kubwa ambalo nimejifunza katika kipindi cha zaidi ya siku 20 za kujifunza asili nimekuja kugundua na kukumbushwa juu ya “Kila kitu kizuri kinahitaji uwekezaji muda wa kutosha”. Ni kauli nyepesi nyepesi kwa …

Nakosea wapi – Nasoma vitabu vingi ila sioni mabadiliko

Maisha ili yabadilike yanahitaji mambo machache unayoweza kufanyia kazi na kujitengeneza nidhamu ya kutenda zaidi kuliko kuishia jambo kulijengea picha pekee. Unabadilika kwa kutenda maana kwa kila tendo huja matokeo. Usomaji wa vitabu ni tabia kama tabia zingine zinazotengenezwa na mtu mwenyewe. Unavyorudia rudia kufanya kitu ndivyo hicho kitu au hali inavyojipa nguvu ya kuyaongoza …

Unachoendelea kukifanya kitakupa UTAMBULISHO.

Utambulisho wa chochote kile umebeba mchango mkubwa wa kuathiri maisha ya mtu au vitu. Kile kinachomtambulisha mtu kina nguvu ya kuruhusu baadhi ya mambo yatokee au kuzuia kabisa mambo yasitokee. Utambulisho ni sawa na chapa ambayo watu wanakupa iwe kwa vile unavyofanya vitu au wao wanavyokufikiri. Hili limeathiri maisha ya watu wengi, biashara na maeneo …

Maisha ni hadithi zitakazosimuliwa wakati ujao.

Nikiwa katika kutafakari maisha yangu ya nyuma naona ni hadithi na masimulizi ya mambo niliyoyapitia na ndivyo wakati ujao haya ya sasa yatakuwa hadithi kwa watu wa vizazi vijavyo. Ukweli huu unaweza mtu asielewe sasa lakini kadri unavyoishi na uzee unavyobisha hodi ndivyo vipande vingi vya maisha ya mtu huwa kama hadithi. Yaweza kuwa mambo …

Faida 5 za kufungua notibuku yako leo.

Notibuku ni ghala la mawazo Leo ilikuwa siku yangu ya tofauti pale ambapo katika mkusanyiko wa kazi nyingi ziliwahi kuziandika magazetini, notibuku na katika komputa nilitenga muda kuzipitia pitia tena. Nilichokipata ndicho kilichozalisha makala hii unayoisoma sasa. Faida tano nazoenda kukushirikisha ni zile ambazo nimebahatika kuzitafakari na kuamua niandike na kukushirikisha wewe msomaji wangu ili …

Vitabu 7 vinavyogusia kufikiri kitajiri na kuanza safari ya UTAJIRI

Rafiki yangu leo tupo kituo kingine cha safari yetu ya maarifa ambapo tunaenda kujifunza vitabu ambavyo vimegusia maarifa ya safari ya utajiri na watu kuwa matajiri. Utajiri ni hitaji la watu wengi duniani kote maana kupitia utajiri ndipo unapoweza kuyaona maisha kwa utoshelevu. Umaskini unatunyima kuyaona maisha kwa picha kubwa tofauti na ulivyo utajiri. Utajiri …

Design a site like this with WordPress.com
Get started