Ujasiri ni kuinuka tena katika anguko- “Anza upya’’

Zama tunazoishi sasa na matukio tunayopitia maishani si mageni kuwa watu walokuwa kabla yetu hawakupitia. Maisha yao na yetu sasa ni mzunguko wa mambo yale yale yanayoendelea kumkumba mtu katika maisha yake. Hili ndilo linalofanya maisha yahitaji ujasiri na ustahimilivu kuyaendesha na kukabiliana na kila aina ya changamoto mtu atayoweza kupitia. Changamoto zinazomkumba mtu katika …

Hifadhi mambo kimaandishi kadri muda uendavyo mengi utayasahau – “Maandishi yanadumu”

Ni rahisi kuona karibu kuliko kuona mbali. Hili lina maana wakati wa sasa ni mfupi kuliko saa zijazo zilizo na nafasi ya utele kuliko sasa. Muda na nguvu zetu zinaenda zikiwa finyu na ndivyo nao mwili hupunguza ufanisi wake kadri mtu azeekavyo. Kuna mambo sasa unaweza kuona ni mepesi ila muda na umri ukishapita hayatakuwa …

Rudia kadri unavyoweza unapotaka kubobea katika kitu – “Kurudia ni Njia”

Kuna kipindi ambacho nilikuwa najifunza mpira na kuangalia mpira hasa maeneo ya viwanja vya mpira na kujifunza kitu kimoja kikubwa nacho ni mazoezi ya kurudia kitu kile au zoezi fulani. Kama ni wachezaji safu ya ushambuliaji kuwaona wakipiga mpira eneo moja mara kwa mara. Hili ni moja tu katika mengi nilojifunza kuwa maisha nayo ili …

“Jifunze misingi na kanuni za eneo jipya utakaloanza kazi”

Maisha yanakuwa magumu si kwa kukosa maarifa pekee bali hata kutojua umuhimu wa kutambua kanuni au misingi inayoongoza vitu ikoje. Unapokosa kujua misingi au kanuni fulani za kitu au kazi ndivyo hali ya ugumu inavyozaliwa na kuwa kikwazo kuwa na urahisi wa kufanya vitu. Imekuwa si mazoea ya watu wengi kujifunza misingi ya eneo jipya …

Vitabu 28 katika mtizamo wa maisha, uandishi, asili na utele – [Zawadi yangu ya kumbukizi ya kuzaliwa]

Vitabu 28 katika mtizamo wa maisha, uandishi, asili na utele – [Zawadi yangu ya kumbukizi ya kuzaliwa] Karibu msomaji na mfuatiliaji wa blogu hii niipayo anuani ya “ghala ya maarifa kimtazamo wa ndani” itakayobakia siku itakapokuwa mwisho wa uandishi wangu. Nafurahia zawadi hii ya uandishi kwa Mungu. Yamekuwa ni maisha yenye maana kubwa toka mwaka …

Siku ya kumbukizi ya kuzaliwa angalia upya maisha yako- “Badili vipaumbele”

Siku kama hii ifikapo ya tarehe 20.08 kila mwaka nakuwa najipa tafakari ya maisha yangu nilipotoka, nilipo na wapi natakiwa kuelekea. Mbali na hayo maswali muhimu nayojiuliza ila huwa nahesabu nafasi ya kuona siku hii kama kumbukizi ya kuzaliwa kwangu miaka ilopita ni zawadi na deni kubwa la kuyaangalia maisha yangu na kubadili vipaumbele vyangu …

Nianze au nisianze kile nilichopanga – “Muda unazidi kunitupa mkono”

Pesa zinaweza kuja na zikapotea tena ukazipata kwa mfumo ule ule wa mnyororo wa thamani kwa kujua matatizo yepi jamii inayosumbuka nayo au mahitaji yepi jamii inayahitaji. Ila muda ambao umepita wa jambo ukishapita umepita na huna nafasi ambayo mtu anaweza kupata muda tena. Inawezekana ni muda wa ujana au muda wa kujifunza jambo fulani …

Maisha ni matokeo ya maamuzi unayoyafanya– “Amua Usijutie baadaye”

Hatuwezi kukimbia matokeo ya maamuzi tunayofanya kila siku za maisha yetu. Iwe ni kwa udogo au ukubwa kwa kila jambo tunaloamua na kulifanya linatutengenezea matokeo yawezekana ikawa sasa au siku zijazo. Maamuzi yanapofanywa sasa bila kujipa tafakari ya namna athari yake itakavyokuwa baadaye huishia kumfanya mtu aingie katika majuto kuwa angeliona kabla basi asingethubutu kuamua …

Kilicho kigumu kwako usifikirie ni kigumu kwa kila mtu- “Omba msaada kwa walioweza”.

Kwa kuona jambo gumu kwako usifikirie ni gumu kuwezwa na wengine Ni asili yetu sisi binadamu unapojaribu kitu na ukashindwa basi unapata wazo au mawazo ya jumla kuwa hili jambo hakuna analoliweza. Kufikiri kwa mtindo huu kunadumaza watu wengi na watu wanaendelea kuishi maisha ambayo hawayafurahii kabisa sema hawana tu namna ya kuvuka hapo walipo. …

Usiwe mvivu kwa vile vyenye tija na maisha yako- HAKUNA MTU MVIVU DUNIANI

Uvivu wa kufanya mambo yenye tija na maisha yetu ndio unatuchelewesha kufikia mafanikio ambayo tungeyapata kama jitihada ambazo tunaweka katika mambo yaso na faida tungeyabadili mkondo wake. Hakuna mtu mvivu duniani maana kuna mambo mtu huyo hana uvivu nayo. Mtu anaweza kusema anajihisi uvivu kusoma vitabu ila si mvivu katika tabia nyingine ambazo ameamua ziwe …

Design a site like this with WordPress.com
Get started