Utakutana na ugumu unapoamua kuanzisha hatua mpya- VUMILIA

Asili yetu sisi binadamu ni kupata faraja tunapokuwa katika hali zile ambazo tumezizoea na huwa kazi ngumu na safari isofurahisha pale tunapotaka kufanya mambo nje na mazoea yetu ya kila siku. Utaona namna ilivyo ngumu kwa mtu ambaye si mazoea yake kuamka asubuhi ilivyo kazi kwake kuamka asubuhi. Utaona namna ilivyo kazi kwa mtu asiye …

Unaumia kihisia kwa matarajio unayodhania- Uhalisia mambo ni TOFAUTI

Agosti 04- Jua mambo yanaweza kuwa tofauti na unavyodhania Mwezi huu nipo nasafiri katika uwanda wa ngazi nne za uwepo. Ngazi ya hisia, mwili, kiroho na kiakili ikiwa ndio safari kamilifu maishani ya kutembea yenye kuzalisha maisha imara na bora. Unaweza kuwa imara kimwili lakini ukikosa uimara wa hisia, kiroho na kiakili bado unakuwa mtu …

Litapita kama mengine yalivyopita- ni SOMO la USTAHIMILIVU

Agosti 3- Mambo hayana makao ya kudumu maishani. Hili nalo litapita tu kama mengine yalivyopita Maisha ni darasa linalotufunda mengi kila iitwapo leo. Darasa hili lina kila aina ya mitihani na mafunzo kama si mambo yanayokutokea Wewe basi kuna watu unawaona wanapitia mitihani na mafunzo mengi. Licha ya hayo yote yanayotokea kuna muda mambo hupita …

Juhudi ni Rafiki wa Kweli [ 1 N ]

“All growth depends upon activity. There is no development physically or intellectually without effort, and effort means work.” – Calvin Coolidge Ukuaji wowote ule unategemea KAZI. Hakuna maendeleo ya kimwili au kiakili bila juhudi. Juhudi kwa maana ya kazi fulani inahitajika kufanyika. Maneno hayo juu yana nguvu kubwa kwangu napokumbuka mengi kuhusu maisha yangu. Juhudi ndio …

Mwezi Agosti – Kitabu cha kusoma [The Four Levels of Healing by Shakti Gawain ]- Ngazi nne za Uponyaji – Mtu ni ngazi nne za Uwepo

-Imarisha ngazi zote nne maisha yawe KAMILI Binadamu ni uwepo wa mambo makubwa manne; Kiroho, kiakili, kihisia na kimwili. Huu mkusanyiko kwa pamoja ndio unaofanya utimilifu na utoshelevu maishani. Haya maeneo manne ni ya kuendelezwa, kuponywa na kufanywa yawe pamoja ili maisha yaitwayo ya maana yaweze kutokea. Ngazi hizi nne ndizo zinazofanya tuone maisha ya …

Bisha hodi nao mlango utafunguliwa- Safari ya Utambuzi

Hodi!,Hodi!, Hodi!  [Tumezoea kubisha hivyo katika milango majumbani mwetu ila ni muda hatujabisha hodi ndani yetu kujua kilichomo ] – Agosti 1 2020 Kama tungeweza kufungua hazina zilizopo ndani yetu kamwe tusingeweza kupata eneo lingetosha kuzibeba. Hii ni dhahiri namna ndani ya kila mmoja wetu kuna hazina na utajiri ambao mtu akikuza nafasi ya kutambua …

Design a site like this with WordPress.com
Get started