Pandisha bei ila fanya jambo hili

Kila mtu yupo tayari kununua kitu anachokipenda au alichokipa kipaumbele kuwa ni kitu au hitaji lenye umuhimu kwake. Bei ya kitu, bidhaa au huduma inaweza kuwakwamisha baadhi ya wateja au kufanya wengine wanunue bila kujali bei ila wamesukumwa na nini wanakipata wakishanunua hicho kitu. Thamani ndio kipimo kikubwa ambacho mteja awe mteja wa bidhaa chache …

Wasaidie wengine kwanza kupata- “Ni sheria ngumu ila ina faida”

Sheria moja kubwa ya mafanikio ni kuwasaidia wengine kufanikiwa kabla hujafanikiwa wewe. Huenda ni ngumu kueleweka kwa juu juu ila ukiangalia kwa kina ina maana kubwa sana. Huwezi jua una nini ndani yako mpaka pale ambapo unapopata fursa ya kushirikisha kwa wengine nao wakakupa utambulisho fulani. Inawezekana ujuzi, kipaji, bidhaa, biashara au maarifa unavyo ila …

Usikimbie mazoezi- “Mazoezi ni maandalizi”

Tafiti zinasema kuwa wakati ambao akili imetulia ndipo penye mazingira mazuri ya mtu kupata mawazo bunifu au ufahamu wa kitu wa kumwacha aah aah kumbe!, au kupata maono ya jambo. Utulivu huu ni ule wa akili inapokuwa inafikiria sasa. Imetokea leo wakati sijui nitaandika jambo gani kama nilivyojipa ahadi kuhakikisha naandika kila siku iwe siku …

Endeleza kipaji chako- “Tayari unao Mtaji”

Kila kona ukitembea utakutana na watu wengi walofanikiwa kutokana na vipaji vyao. Wengine ni vipaji vya kucheza mpira, kuandika, kuchora, kuimba, mahesabu, utoaji ushauri na kadhalika. Mbali na machapisho mengi na vitabu kugusia kuwa mtu ana vipaji zaidi ya 08 bado kuna kundi kubwa la watu ambalo limekosa kutambua kuwa ndani ya kila mtu pana …

Uvumilivu, Ustahimilivu na Utulivu – “Maisha yenye Uimara”

Maisha ni darasa pana ambalo kila siku halituachi kutufundisha mambo mengi. Masomo makubwa katika maisha ambayo yanaweza kufanya maisha kuwa bora na imara ni kuwa mvumilivu, kuwa mtulivu na kuwa na ustahimilivu. Hivi vyote katika umoja vinayapa maisha kuwa na msingi imara. Uvumilivu ni pale ambapo unapokuwa tayari kuvuta subira katika unachokifanya ukiwa na imani …

Wakati mzuri wa Kufanya kazi – “Ni unapokuwa na Nguvu”

Kitu pekee ambacho kinazidi kupungua kila iitwapo leo kwa mtu basi ni nguvu. Rasimali muda inaweza kupatikana ila nguvu hupungua kadri umri unavyoongezeka na hatuwezi kuwa na nguvu zile zile ambazo wakati wa ujana zilikuwepo. Rasimali hii ni muhimu sana kuitumia kwa umakini tukijua haitupi nafasi ya kuwa nayo kadri tuongezakavyo umri. Nguvu za mwili …

Umuhimu wa kuwa na mtu aliyekutangulia- “Jifunze Kupitia Viatu Vyao”

“Tunahitaji miongozo kutoka kwa wale ambao wametutangulia. Tunahitaji walezi hawa”. Ni moja ya nukuu za mwanafalsafa Marcus Aurelius. Walotutangulia wana mambo makubwa mawili yanayoweza kuwa msaada kwetu. Mosi wanafahamu njia na pili wana mtaji mkubwa wa uzoefu. Uzoefu na kujua njia maishani ndivyo vitu vikubwa ambavyo kila mmoja ndani yake anapambana kuvijua. Ukiwa na uzoefu …

Maandishi Huishi: My Life, My Purpose by Benjamin W Mkapa (Somo – “Kwa nini na kwa namna gani ?” )

Ukitembelea na kusoma ukurasa wa 11 aya ya pili unakutana na maneno “Kwa nini na kwa namna gani?” Msingi wa makala hii utaenda kujikita eneo hili. Uandishi wa tawasifu au masimulizi yanayoandikwa na mwandishi mwenyewe yana uzito mkubwa sana ikiwa ataandika katika ukweli na uwazi. Ukweli na uwazi wa mwandishi unampa msomaji kuhisi kabisa sauti …

Chaji Betri lako- “Kupumzika baada ya kazi ni muhimu”

Ukiwa unapita pita kila kona siku hizi basi sitilii shaka utaonana na mtu au watu wakiwa na uhitaji wa simu zao zipate kuchajiwa mara baada ya betri kuwa chini {battery is low]. Huenda betri linapochajiwa kuwa lina asilimia 100% ila kadri muda uendavyo na unavyoendelea kuitumia simu ndivyo asilimia zinavyopungua hadi kufikia simu kuzima kabisa. …

Mtu akikutukana huwa unafanya nini ?

Hebu fikiria mtu anakupigia simu, unapokea na katika maongezi anakiri kukosea namba ila baada ya muda anapiga tena na Wewe unamwambia kuwa nambari upigayo umekosea. Mwitikio wake unakuwa ni kukutusi tena matusi makubwa makubwa. Ukiangalia unaona hujatendewa haki kutukwana na huna kosa ulofanya ila kuhoji tu. Je utamtukana ?, utazima simu au utafanya kitu gani …

Design a site like this with WordPress.com
Get started