ANZA 14; Tafuta Kitu Kimoja Hata Ukikata Kabisa Tamaa Utaendelea Kukifanya

Nimechagua kuandika hata kama nitapitia changamoto ngumu basi nitaweza kujisukuma niendelee kuandika na kushirikisha maarifa. Kuandika kunanipa msukumo mkubwa kuhakikisha yale nayoyafahamu naweza kuandika na kushirikisha wengine katika nyakati zote. Kuandika kupitia mitandao ya kijamii nimeanza toka mwaka 2017 ambapo nimekuwa najisukuma kuandika na kushirikisha yale nayoyafahamu, nilowahi yapitia na yale ninayojifunza kila siku.   …

ANZA 13; Ulichokianzisha Lazima Upimwe Kama Una Msimamo Kweli au Laah

Utapimwa katika chochote unachokianzisha ikiwa kweli umejitoa kweli au umefanya miguu nje au ndani. Utaleta wazo fulani kwa watu ila linaweza lisipokelewe vile ulitegemea wangelipokea au kuunga mkono. Usipokuwa imara hapa basi utapuuza namna unaona wazo lako lina kitu fulani cha kuchangia jamii yako. Unachopimwa siku zote ni msimamo juu ya kitu unachokifanya kama kweli …

ANZA 12; Tetea Ulichokianzisha Usikubali Kiishie Njiani

Tunaishi katika zama ambazo unahitaji ujitoe mzima mzima katika kitu unachotaka kufanikiwa kwacho. Vikwazo na kukatishwa tamaa kuko kila kona na ukiwa huna ujasiri basi chochote utakachokuwa unakianzisha au kukitambulisha utaishia njiani. Wengi wameishia njiani baada ya kukatishwa tamaa au kukutana na vikwazo. Uhalisia hakuna mambo utayapata kirahisi bila kutetea hadi uyaone yakitimia. Lazima ujitume …

ANZA 11; Umepoteza Kabisa Hamasa Basi Angalia Ulokwisha Fanikisha Siku Za Nyuma

Tunahimizwa sana kuwa watu wa shukrani kila tunalopitia maishani. Watu ambao wana maisha ya kujifunza kushukuru kila siku wanapata faida moja kubwa ya kuwa watu wenye hamasa katika kuchukua hatua kuliko wale ambao hawajali wala hawaoni uzito wa kushukuru hatua ambazo wamekwisha kufanya au kusaidiwa. Hamasa huwa haidumu katika maisha ni sawa na kula huli …

ANZA 10; Bahati Itakukuta Wakati Unaendelea Kuchukua Hatua Kila Siku

Tunaishi katika zama ambazo kupata chochote unachokihitaji lazima uweze kujituma na kujitoa kweli kuwa umedhamiria haswaa. Usipokuwa imara, mstahimilivu, king’ang’anizi huwezi kupata unachotaka kukipata. Maisha halisi yanataka uwe kama mpambanaji na mtafutaji asiyechoka. Maisha hayatakupa vitu kirahisi rahisi au kwa bahati bila kuwa ulishajiwekea mazingira ya maandalizi ya kutokea vyote unavyotaka vijitokeze. Nafasi ya mafanikio …

ANZA 9; Msukumo wa Ndani Ndo Chanzo cha Matokeo Yote Tunayotamani Yatokee

Mwanzo wa kutokea kitu huanza na msukumo na huu msukumo ni ule utokao ndani yetu. Msukumo huu unaweza kuwa katika mfumo wa mawazo, picha au hisia. Hisia, mawazo au picha katika akili hutengeneza msukumo wa kutamani kuona kilicho ndani kinakuwa halisi. Laweza kuwa wazo la bidhaa au biashara mtu analo ndani yake na anapata msukumo …

ANZA 8; Shangilia Ushindi wa Hatua ndogo ndogo ila Usibweteke Bali Ongeza Mwendo

Ushindi wa jambo lolote lile hutia hamasa ndani ya mtu. Hali nzuri unayopitia unapokuwa umeshinda kitu au kufanikiwa kitu inaweza kukulewesha ukasahau bado safari ya kule uendako bado ni mbali. Unaposhinda au kufanikiwa hatua ndogo ndogo ndani ya ubongo hutolewa kemikali moja ya zawadi “dopamini” ambayo inampa mtu hali ya kujisikia vizuri baada ya kufanikiwa …

Design a site like this with WordPress.com
Get started