554; February 24, Nitakavyokuwa naweka muda wa kujifahamu kwa kina basi njia ya kufahamu maisha kwa kina itakuwa nyepesi.

Lengo kuu moja kubwa la maisha na siku zote za uhai wetu ni kufahamu jinsi tulivyo na kujua kwa kina umaana wa kuishi kwetu tunaishi kwa sababu gani. Toka utoto hadi siku ya umauti ni katika safari hii ya kugundua mengi yalokuwa ndani yetu ila kwa kadri tuishivyo yanajidhihirisha kidogo kidogo hata kufika utoshelevu. Safari …

553; February 22, Nikitumia mitandao ya kijamii au vyombo vya habari kama rejea ya kupima mambo nimekubali kutopata uhalisia wa mambo ulivyo.

Kile kinachooneshwa au kutangazwa au kuandikwa kupitia vyombo vya habari au mitandao ya kijamii ni sehemu ndogo ya uhalisia wa vitu vilivyo. Na ni makosa makubwa ninapoweka akili kutumia kama rejea ya kujua mambo kwa kina. Kile kinachoonekana si ilivyo nyuma ya hicho kitu na ukitegemea kama kilivyo unaruhusu matatizo na upotevu muda wa kitu …

552; KURASA 10 kila Siku, Uchambuzi wa Kitabu ~ HAPPINESS for HUSBANDS and WIVES by Harold Shryock ( FURAHA kwa WAUME na WAKE )

Kitabu kizima; 272 kurasa Nakala ngumu ( Hard copy ) Kurasa; (17 ~ 29 ) Uchaguzi wa mwenza wa Maisha. Imekuwa inajulikana kuwa moja ya matukio muhimu kwa maisha ya mtu ni kuzaliwa, ndoa na kifo. La kwanza na la mwisho hakuna ambaye huwa ana uwezo nayo kuyazuia au kutaka yawe atakavyo kuliko la pili …

551; February 21, Ili nipate nitakacho lazima nivivuke vikwazo na maumivu kati kati ya mchakato.

Ili tupate chochote kile kizuri na bora huwa tunatenganishwa na vikwazo na maumivu ya jinsi ya kukipata. Tukitaka mwili mzuri lazima tuvuke maumivu ya misuli na tuendelee mbele kati kati ya vikwazo ili miili tutakayo ije. Na hii sio katika mwili pekee hata maisha ya mafanikio lazima kushinda vikwazo na maumivu kati kati ya mchakato. …

550; KURASA 10 kila Siku, Uchambuzi wa Kitabu ~ HAPPINESS for HUSBANDS and WIVES by Harold Shryock ( FURAHA kwa WAUME na WAKE ) Kitabu kizima; 272 kurasa

Kitabu kizima; 272 kurasa Nakala ngumu ( Hard copy ) Kurasa; (5 ~ 16 ) Ndoa ni sehemu ya maisha na ni ngazi ya mahusiano ilo juu zaidi ya ukaribu mkubwa wa kihisia baina ya watu wawili ambao wamejitoa kusafiri pamoja wakiwa na nia ya ujenzi wa taasisi moja kubwa ya mahusiano. Mafanikio na furaha …

549; February 20, Sio ninachokisema kitabadili hatua zangu ila kile ninachokifanya kitanipa matokeo.

Kuongea ni rahisi na kila mtu anaweza kuongea atakavyo lakini si sawa katika kufanya hapo wapo wachache sana. Kufanya ni kazi nzito na yataka ujisukume haswaa na kufanya hakutaki maneno ila matokeo. Bila kufanya hakuna mabadiliko na Dunia haisubiri wenye maneno tupu ila inawapa nafasi watendaji na ambao wako tayari kuziendea hatua juu ya maisha …

548; February 19, Maisha ni zawadi na kila siku tuamkapo tushukuru kuwa na hii nafasi ya kuwa hai.

Jambo tunalopaswa kutambua kila siku ni kuwa maisha ni zawadi. Uhai ni thamani ya uwepo wetu na hii nafasi ni ya pekee na kama tutakosa shukrani basi tunakosa kutambua kuwa hii nafasi ni ya ukomo na haipo sehemu huuzwa ikishapotea. Kuamka katika kuipokea kwa furaha na shauku ya kuwahudumia watu wanaotuzunguka ndio umaana wa kuwa …

547; February 18, Kila kitu kitabadilika nikibadilika kufikiri na kuanza kuchukua hatua.

Mafanikio ya kweli huanzia ndani na huko ndani yanaenda kugusa mfumo mzima wa kufikiri. Pale kufikiri kukibadilika basi mambo yote nje nayo yanaitikia mabadiliko toka ndani. Vile mawazo chanya nitakavyoruhusu yawe na himaya ndani ya fikra zangu ndivyo urahisi wa mambo yote nayotamani kuona yakibadilika nitayaona wazi wazi. Iwe ni kazi, mahusiano, maisha, kipaji, maono …

546; February 17, Nguvu zako zipo katika utulivu

Jinsi ambavyo Dunia inavyozidi kuwa bora na kuwa kijana ndivyo usumbufu unavyozidi kuongezeka na utulivu kuwa bidhaa adimu kupatikanika. Kila siku watu wako na pirika pirika ambazo zinawanyima hata muda wa kutulia kisha wakapima katika pirika zote hizo je wanapiga hatua ? au wamekwama. Maana si shida kuwa na pirika pirika nyingi ila ufanisi ndicho …

545; February 16, Mafanikio ya kweli sio tukio ni mchakato wa hatua ndogo ndogo za kila siku endelevu

Watu wengi huvutika na matokeo ya kitu na hupofushwa wasione matokeo hayo yamezalishwa na nini. Kuona matokeo pekee hutaweza kuona uhalisia wa mambo na hivyo utakosa maana sahihi ya mafanikio ni nini?. Kwa kuwa matokeo huvutia sana ndo maana wengi waanzapo na maana ya mafanikio kama matokeo waanzapo safari na kisha kuona kisicho huishia njiani …

Design a site like this with WordPress.com
Get started