Uvumilivu, Ustahimilivu na Utulivu – “Maisha yenye Uimara”

Maisha ni darasa pana ambalo kila siku halituachi kutufundisha mambo mengi. Masomo makubwa katika maisha ambayo yanaweza kufanya maisha kuwa bora na imara ni kuwa mvumilivu, kuwa mtulivu na kuwa na ustahimilivu. Hivi vyote katika umoja vinayapa maisha kuwa na msingi imara. Uvumilivu ni pale ambapo unapokuwa tayari kuvuta subira katika unachokifanya ukiwa na imani …

Wakati mzuri wa Kufanya kazi – “Ni unapokuwa na Nguvu”

Kitu pekee ambacho kinazidi kupungua kila iitwapo leo kwa mtu basi ni nguvu. Rasimali muda inaweza kupatikana ila nguvu hupungua kadri umri unavyoongezeka na hatuwezi kuwa na nguvu zile zile ambazo wakati wa ujana zilikuwepo. Rasimali hii ni muhimu sana kuitumia kwa umakini tukijua haitupi nafasi ya kuwa nayo kadri tuongezakavyo umri. Nguvu za mwili …

Umuhimu wa kuwa na mtu aliyekutangulia- “Jifunze Kupitia Viatu Vyao”

“Tunahitaji miongozo kutoka kwa wale ambao wametutangulia. Tunahitaji walezi hawa”. Ni moja ya nukuu za mwanafalsafa Marcus Aurelius. Walotutangulia wana mambo makubwa mawili yanayoweza kuwa msaada kwetu. Mosi wanafahamu njia na pili wana mtaji mkubwa wa uzoefu. Uzoefu na kujua njia maishani ndivyo vitu vikubwa ambavyo kila mmoja ndani yake anapambana kuvijua. Ukiwa na uzoefu …

Maandishi Huishi: My Life, My Purpose by Benjamin W Mkapa (Somo – “Kwa nini na kwa namna gani ?” )

Ukitembelea na kusoma ukurasa wa 11 aya ya pili unakutana na maneno “Kwa nini na kwa namna gani?” Msingi wa makala hii utaenda kujikita eneo hili. Uandishi wa tawasifu au masimulizi yanayoandikwa na mwandishi mwenyewe yana uzito mkubwa sana ikiwa ataandika katika ukweli na uwazi. Ukweli na uwazi wa mwandishi unampa msomaji kuhisi kabisa sauti …

Chaji Betri lako- “Kupumzika baada ya kazi ni muhimu”

Ukiwa unapita pita kila kona siku hizi basi sitilii shaka utaonana na mtu au watu wakiwa na uhitaji wa simu zao zipate kuchajiwa mara baada ya betri kuwa chini {battery is low]. Huenda betri linapochajiwa kuwa lina asilimia 100% ila kadri muda uendavyo na unavyoendelea kuitumia simu ndivyo asilimia zinavyopungua hadi kufikia simu kuzima kabisa. …

Mtu akikutukana huwa unafanya nini ?

Hebu fikiria mtu anakupigia simu, unapokea na katika maongezi anakiri kukosea namba ila baada ya muda anapiga tena na Wewe unamwambia kuwa nambari upigayo umekosea. Mwitikio wake unakuwa ni kukutusi tena matusi makubwa makubwa. Ukiangalia unaona hujatendewa haki kutukwana na huna kosa ulofanya ila kuhoji tu. Je utamtukana ?, utazima simu au utafanya kitu gani …

Ninatazama Mlima – “Natakiwa nipande na kufika juu kileleni”

Kughairisha ni mlima, uvivu ni mlima, kutothubutu ni mlima. Mlima una vikwazo na kufika juu ya mlima basi lazima upande na kutoruhusu vikwazo vikufanye usifike juu kileleni. Maisha yetu ni mikusanyiko ya vilima mbalimbali ambavyo bila kuwa tayari au kuwa watu jasiri hatuwezi kupata ushindi wowote mkubwa maishani. Kughairisha ni kikwazo kikubwa sana ambacho kinatuchelewesha …

Mwonekano unaweza kukudanganya- “Kisogelee hicho kitu karibu”

Mwonekano wa vitu na bila kufikiri kwa kina umefanya tuingie katika matatizo mengi ambayo yangeepukika endapo tungejipa muda wa kukisogelea hicho kitu kwa karibu. Inawezekana mtu ukavutika na mwonekano wa kitu na ulipokisogelea na kuona kumbe mwonekano ulikuwa ni juu juu tu na si vile kilivyo ulivyokiona. Jambo moja kubwa ni mafanikio ya jambo lolote …

Ukomavu wa juu wa maisha- “Kujisimamia bila kusukumwa”

Maisha tulonayo sasa ni matokeo ya karibu asimilia 80 za yale tunayoyafanya kuliko tunayoyaongea. Hili ndilo linatupa maisha tulonayo sasa na kutoka hapa tulipo ni kuamua kufanya kwa utofauti kuliko tulivyokuwa tunaendelea kufanya. Maisha ni wajibu wetu bila kuwa na mtu wa kutusukuma sukuma tufanye tunayopaswa kufanya. Ngazi ya Wewe mwenyewe kuweza kujisimamia bila msukumo …

Ukipenda unachokifanya kitakufikisha mbali- “Upendo una NGUVU”

Wanasema katika maisha kuna nguvu kubwa mbili zinazoyaongoza maisha yetu. Mosi ni nguvu ya “HOFU” na pili ni nguvu ya “UPENDO”. Watu wanafanya vitu katika msukumo wa hizi nguvu ukiangalia kwa kina. Mtu asipoongozwa na upendo basi hofu itachukua nafasi ya kumwongoza. Nguvu ya hofu inawadidimiza watu kupata vitu vingi bora maishani na watu wanajawa …

Design a site like this with WordPress.com
Get started