IVUKE HOFU ANZA KUTENDA

Habari ya siku nyingine mpya, imekuwa ni neema tena kuiona hii inatupa nguvu kuwa leo ni kama ukurasa safi wa karatasi unaotakiwa kuandikwa kwa uzuri. Siku inaanza kuonekana vizuri asubuhi kwa kuwa na vipaumbele vitakavyokusogeza mbele katika mafanikio yako iwe ni elimu, kiroho, kiuchumi hata kijamii kwa ujumla. Leo tujikumbushe kwa Habari ya namna ya …

MAANA BINADAMU TUNAYO KAWAIDA KUSAHAU

Tusije kusahau jambo hili, maana binadamu tunayo kawaida ya kusahau Usijesahau mtoto akikua atakuwa mtu mzima, na huenda alichokibeba huwezi jua atazaa kitu gani ? Usijesahau aliyekuwa na afya huenda akawa mgonjwa mtarajiwa licha kujua taratibu zote za afya Usijesahau kuwa leo itaisha na itapita na siku nyingine itakuja na mambo yake Usijesahau kuwa kuna …

KESHO UNA LAKO JAMBO

Utendi: Kesho Una Lako Jambo Kesho U lugha za fumbo Umeniacha kikumbo Niige watu mkumbo Niahirishe na mambo Kesho nakutafuta miaka sijakupata Hadi mvi nimepata Ngozi nayo yajivuta Nguvu zikaniondoka Kesho nikidhani shaka Nikajua itafika Ningali nguvu hakika Kauli hii ya kesho Kwangu imekuwa mwasho Lini utakuwa mwisho Kesho aje hitimisho ? Uliniahidi kesho Uvivu …

USIMSEME MTU, JISEMESHE MWENYEWE

SHAIRI: NAJISEMESHA MWENYEWE Najisemesha mwenyewe, huwa zingo aisema Kujitathimini wewe, ukajijua vyema Jukumu ni lako wewe, sipofanya utakwama Mtu na asilaumiwe, kuzipeleka lawama. Jitambue jikague, kwa kujisemesha wewe Jichambue ujijue, faida yako mwenyewe Na Jione jipimee, kioo chako nakiwe kukumbuka jichague, kichwani ujielewe Usiseme ya jirani, kwanza jione machoni Na uyajue ya ndani,yako yaliyo sirini …

Design a site like this with WordPress.com
Get started