Kinachotofautisha watu maishani ni mambo mawili au matatu. Jambo la kwanza ambalo nimeona kwa kutazama na kuishi kwangu ni juu ya uzoefu. Ukiwa na uzoefu wa jambo unakuwa mtu huru, jasiri na mwenye furaha. Mtu asiye na uzoefu katika eneo fulani huwa ni mtu asiye na ujasiri, mashaka na hofu. Tenga muda na wekeza kufanya …
Nyakati ngumu endelea kuwa imara.
Kuna wakati ambao unakutana na ugumu kiasi kwamba unapata sababu za kukata tamaa pale unapoona watu wengi ulokuwa unajua wana nguvu na ni watu imara nao nyakati ngumu ziliwaondoa ujasiri wao na nguvu zao nao kuwa watu dhaifu na wenye kuhitaji nguvu ya kusonga mbele. Nyakati ngumu ni nzuri kwa lengo moja kubwa la ukuaji …
Kuchukua hatua mapema kunazuia gharama kubwa baadaye.
Kughairisha mambo ni tatizo kubwa linalonyima fursa nyingi kufunguka kwa watu wengi. Pale unapoghairisha vitu au kufanya jambo kwa kufikiri huenda baadaye utafanikiwa kulifanya kumesababisha majuto makubwa siku zijazo. Imekuwa kawaida kughairisha mambo kwa kufanya siku moja na baadaye kughairisha inakuwa tabia inayosababisha mambo mengi yasiwezekane kutokea. Hili linaonekana dhahiri pale ambapo mwaka mpya unapoanza …
Continue reading "Kuchukua hatua mapema kunazuia gharama kubwa baadaye."
Somo la maisha yangu yalopita- LEO NI NYEPESI ILA SIO KESHO
Napenda kuandika, najisikia utoshelevu kuandika, sitaacha kuandika. Kuandika kunanirudisha katika kina cha mawazo, kunanipa nguvu nisiyoweza kuelezea. Uandishi ni alama ambayo itabaki na kunipita miaka mingi kuishi zama hadi zama. Vile tusomavyo leo maandishi ya watu waloishi miaka zaidi ya 2000 basi ndivyo ilivyo alama ya uandishi hudumu vizazi hadi vizazi. Nami nashukuru kuwa katika …
Continue reading "Somo la maisha yangu yalopita- LEO NI NYEPESI ILA SIO KESHO"
Makala ya uchambuzi wa kitabu; Embracing Life After Loss by Allen Klein (Maisha baada ya kuondokewa)
Maisha ni zawadi pale ambapo watu huendelea kuishi. Ila wanapoondoka na kuwa mbali nasi kwa njia ya kifo na kutokuwa na matumaini ya kuwaona tena ndipo maisha hugeuka na kuonekana ni mateso na maumivu yasoweza kuelezeka. Ila kupoteza watu wetu wa karibu ni jambo lisiloweza kukwepeka maishani. Maana hata sisi siku moja tutaondoka na kuwaacha …
Mahojiano; Sam Vidambu kutoka Kenya
Karibu tujifunze pamoja rafiki, Dunia inakua haraka tofauti na miaka 500 ilopita. Uwepo wa ukuaji wa mitandao ya kijamii kumeleta manufaa makubwa ya kujenga mtandao wa marafiki, walimu, menta kupitia mitandao ya kijamii hasa majukwaa ya mtandaoni kama “Whatsapp”. Mwaka huu nilikutana na ndugu Sam Vidambu kwa kuunganishwa na rafiki yangu Deviano ambaye naye tulionana …
Muziki na ucheshi huibua chemchemi ya furaha ndani yetu.
Habari rafiki yangu unayeendelea kujifunza kila siku bila kuacha. Uwekezaji unaojiwekea sasa wa kujielimisha ni akiba na marejesho yatakayokuwa na faida kwako siku zijazo. Endelea kuupenda ubongo na akili yako kwa kulisha maarifa na taarifa zenye kukufanya uwe bora kila siku. Liwe lengo lako mama kwa mwaka unaoenda kuanza 2020 kuwa utajielimisha zaidi na kuwekeza …
Continue reading "Muziki na ucheshi huibua chemchemi ya furaha ndani yetu."
Kuishi unachokisema ni kazi ngumu. Ila izoe hivyo hivyo.
Je ungoje kuweza kuishi unachokisema kabla ya kusema ?. Je useme kisha uende kuchukua hatua kuishi ulichokisema?. Ni maswali magumu ambayo unaweza kujiuliza wewe au watu wengine kuwauliza wanaoandika au kusema kitu kwa wengine. Kuishi ni zoezi gumu na linataka uanze kuwa muwazi kwako mwenyewe kabla ya watu wengine kuwa tayari kukuona u muwazi. Ni …
Continue reading "Kuishi unachokisema ni kazi ngumu. Ila izoe hivyo hivyo."
MATATIZO YA JAMII
Mawasiliano; +255 676 559 211 Malenga wa Ubena +255 654 993 263 Jane David ( Sms tu ). Jane ni mshairi mwenye tatizo la usikivu na ana shida ya miguu. Ila ni mpambanaji sana na unaweza usijue kama ana changamoto hizo katika maisha yake. Raymond N Mgeni. Natafuta matatizo, niweze kuyatatua Ndio kazi ya mjazo, …
NIFUNZE KUWA MUUZAJI
Marko Kinyafu Muumini wa kweli, +255 (0) 714 129 520 Kinyafumarcos@gmail.com Kitunda, Dar es salaam, Tanzania Dr.Raymond Mgeni Malenga wa Ubena, +255 (0) 676 559 211 Raymondpoet@yahoo.com Mbeya, Tanzania Kinyafu Marko; Mwalimu wangu mwalimu, naanza nayo dawia Leo nimetia timu, hapa kwako kukujia Ninalo jambo muhimu, nataka kulitambua Ati miye nifanyaje, niwe muuzaji bora? Dr.Raymond …