Mwaka 2018 nilipata fursa ya pekee ya kusoma kitabu cha “The ASSIGNMENT” kilichoandikwa na Mike Mudrock. Kitabu hiki nilipewa zawadi na ndugu yangu mmoja ambaye tulionana katika duka la vitabu “HOUSE OF WISDOM” maeneo ya Posta. Huyu ndugu alikuwa akinitafuta na wakati mwingine tunatafutana ili anipe hiyo zawadi ambayo hadi leo hii nabaki kuona kama …
Kuwa na fikra za utele na fikiri kitajiri.
Fikra za utele zinakufanya uone maisha yana wingi wa vitu kuliko vile ambavyo una fikra za uhaba. Unapoweka fikra zako katika kuwa na kitu ndivyo shauku kubwa ya kuumbika kwa hicho kitu hutokea. Hili liko wazi sababu mawazo ni nguvu na ni nguvu ambayo wakati wote hujitafuta ijitokeze katika umbo. Unaweza kuona hili halina nguvu …
Continue reading "Kuwa na fikra za utele na fikiri kitajiri."
Hujachelewa kuanza kusoma vitabu.
Habari rafiki yangu. Naamini unaendelea vizuri na hatua zako za kila siku. Nafasi uliyonayo sasa kuwa hai ni zawadi ya pekee sana. Itumie kujiboresha kila inapoitwa leo bila kukata tamaa. Kuna wakati utajaribu utaanguka ila usife moyo kuendelea kujaribu na kujiboresha wewe kila siku. Jua kuwa hakuna kitu kinakuwa bora kwa siku moja bila majaribio …
647; Ukiona mtu yupo mbali ujue alipotoka ni mbali.
Leo hebu tulia na vuta picha ya kila mtu unayejifunza kitu kutoka kwake na ona nyuma ya pazia kabla ya huyo mtu kufanikiwa alipitia changamoto zipi. Ukiangalia kwa kina utaona safari ya yeye kuwa hapo alipofika ilichukua muda mrefu kufika hapo. Unaweza kuvutika na mtu alivyoweza kuwa na utajiri na kujenga jina kubwa kibiashara au …
Continue reading "647; Ukiona mtu yupo mbali ujue alipotoka ni mbali."
646; Kuna njia nyingi za kufanya kitu chochote. Jisukume kufikiri zaidi ya unavyofikiri
Kama leo utasema uende mkoa mmoja hadi mwingine unaweza kutumia njia nyingi za usafiri. Unaweza kutumia usafiri wa anga, barabarani na majini. Hata usafiri wa barabarani unaweza kutembea kwa miguu, baiskeli, pikipiki au gari. Kinachotofautisha ni gharama ambayo utaingia katika kutumia njia za usafiri kufika eneo lingine. Ila njia za kufanya kitu bado zinaendelea kuwa …
645; Mwonekano unakudanganya jipe muda utajua uhalisia.
Habari rafiki yangu. Ni muda sasa sijakuandikia kitu kupitia blogu hii kwa kipindi cha mwezi mmoja sasa umepita. Nimerejea tuendelee na safari ya kujifunza hadi pale ambapo tutafika ukomo wa maisha yetu. Mwezi wa nane ulopita nilimpoteza rafiki yangu na mtu muhimu sana katika maisha yangu. Baba yangu mzazi alimaliza safari yake ya zawadi ya …
Continue reading "645; Mwonekano unakudanganya jipe muda utajua uhalisia."
Uchambuzi wa kitabu; Hii zawadi yangu siku ya kumbukizi ya kuzaliwa kwangu- “A HAPPY POCKET FULL of MONEY by David Gikandi”. Ikiwa na maana ya kifurushi cha furaha ya Fedha.
Hiki kitabu nimechagua nichambue kwa siku hii inayonipa tafakari ya uwepo wangu Duniani. Uwepo wetu una maana kama tuna nafasi ya kuchangia kuifanya Dunia iwe bora. Nami siku hii nakualika katika kifurushi hiki cha furaha ya fedha ujifunze namna utambuzi huu utakupa maisha ya furaha na utajua sababu ya kuishi kwako. Nakukaribisha kujifunza kuanzia Dunia …
Makala; Nguvu ya 100, mambo 100 na kama fedha, mtandao wa kutosha wa watu unavyoweza kuisaidia jamii miaka 100 ijayo.
Makala hii ni moja ya zoezi ambalo nimejipa mwenyewe katika kutii ushauri wa mwandishi Brian Tracy namna fedha ni muhimu ikiwa utapata namna bora ya kuitumia kuisaidia jamii. Hivyo akawa kapendekeza kuandika mambo 100 unayoweza kufanya kwa kutumia fedha, mtandao wa watu kuisaidia jamii ikapiga hatua za juu. Name sikuchelea kuandika yale ambayo nimeona yanaweza …
Makala- Utulivu una mitetemo ya juu. Penye utulivu pana nguvu
Zama tuishizo zina usumbufu mwingi kuanzia watu ambao wanatuzunguka, maeneo ya kazi hadi katika mitandao ya kijamii. Watu wamekosa ule utulivu hata wa kusikia sauti ndani yao. Hili ni hatari ambapo watu wanakosa muda wa utulivu wa kuwa wao kama wao. Usumbufu huu umefanya watu wakose ufanisi katika kazi zao na hata matokeo kuwa madogo. …
Continue reading "Makala- Utulivu una mitetemo ya juu. Penye utulivu pana nguvu"
Unaposaidia wengine unajisaidia wewe mwenyewe
Maisha ni mwangwi wa kila unachokifanya. Kile unachokiona nje yako ndivyo ulivyo ndani yako hupishani sana na wewe wa nje na wa ndani. Ukibadili ndani yako kuona kitu, kufikiri kitu au kuhisi ndivyo nje yako utaona sawa na ulivyoona ndani yako. Kile kinachoonekana nje ni kuakisi tu yale yalo ndani ya mtu. Hii ni siri …
Continue reading "Unaposaidia wengine unajisaidia wewe mwenyewe"