624; Hatua ndogo ndogo hazitakuchosha ila siku zitakupa matokeo makubwa.

Habari ya asubuhi rafiki. Leo ni siku mpya tena na zawadi ya maisha kwetu kushukuru nafasi ya kuwa hai na pili kuendelea kuishi kile ambacho kitakuwa daraja kwa watu wengine. Ni leo siku ya kujisukuma kuchukua hatua na kupata matokeo yawe makubwa au madogo madogo. Tunahimizwa na pengine wengine wanatuhamasisha juu ya kuwa na maono …

623; Mtu ni kazi inayoendelea haijakamilika. Usijisikie vibaya kuwa katika matengenezo

Habari ya siku mpya rafiki. Kila siku ni siku mpya unapaswa kuwa mpya kuanzia kifikra na ukijisukuma basi hatua zako ziwe bora kuliko jana. Siku kama hii imekuwa ni zawadi maana si wote wameipata ila wewe na mimi tumepata hii zawadi itumie vizuri na kuwa na shukrani. Maisha yetu ni hadithi inayoendelea kusimuliwa kila siku …

622; Uchambuzi wa kitabu, MAXIMUM INFLUENCE- The 12 Universal Laws of Power Persuasion by Kurt W. Mortensen ( Ushawishi wa Juu~ Sheria 12 za Asili za ushawishi wenye nguvu ).

Ushawishi ni kiungo muhimu katika mafanikio makubwa kwa kitu chochote kile Duniani. Matangazo mengi utaona wanawekeza fedha nyingi lengo kufikisha nguvu ya ushawishi kwa watu juu ya vitu wanavyofanya. Viongozi, biashara zote zinatafuta kuongeza nguvu ya ushawishi mkubwa. Kila siku hata katika mitandao ya kijamii tunakutana na jumbe au picha au tangazo katika kutushawishi kufanya …

621: Una kitu unachomiliki kinakumiliki; Ukikosa udhibiti kitakuangusha

Leo ni siku mpya na haifanani na jana. Jana ilipita imebakia kumbukumbu ambalo liko katika akili zetu na tena cha kushangaza unachokumbuka ni picha picha tu. Leo iko mikononi mwako sasa na haikai nayo itaondoka na kuwa jana ifikapo kesho. Maisha yetu ya nje yalivyo ni zao la ndani kulivyo. Kile kinachoonekana na mtu kama …

620: Mobile Chambuzi 25#; Uchambuzi wa kitabu- Matrix of Mind Reality; Discover the Greatest Secrets of the Mind and Reality to get anything you desire, Always like a magic by Noctis Enoch.

Habari Rafiki. Naamini siku yako imekuwa bora sana na unaendelea kujifunza kila siku pasipo kukoma. Maarifa ndio njia bora ya kutufanya tupige hatua kila siku kwa kutupa mtizamo wa kina wa mambo kila iitwapo leo. Na ndio chakula halisi cha Akili na ukomavu wa fikra zetu. Fikra zetu na sheria za asili zimebeba siri kubwa …

619: Mobile Chambuzi 25#, Kitabu~ The PARABLE of DOLLAR; Proven Strategies for Financial Success by Sam Adeyemi ( Mikakati ya Mafanikio ya Kiuchumi )

Habari Rafiki, Karibu katika safari ya maarifa kusafiri pamoja siku hadi siku. Tunajifunza kubadili tulichokuwa tunakijua na tunabadili kutenda kwetu na matokeo tupatayo huwa tofauti. Hivyo ili kufanikiwa kwa chochote lazima safari ianzie ndani ( mfumo wa kufikiri ) kisha hatua ya kutenda mpya na mwisho ni kicheko cha matokeo bora. Kila mmoja anapenda kuona …

618: Jiandae kwa lolote endapo ulichotegemea kisipokuwa hicho ili kubaki na utulivu wako.

Masomo mengi ya kuhamasisha yamekuwa yanafundisha sana upande chanya wa mambo, upande mzuri wa mambo. Hili ni jambo zuri sana kuifanya akili iwaze chanya na mambo bora. Lakini kuna wakati mambo huenda kinyume na matarajio ambayo yametegemewa na kama mtu hakuwa kajiandaa kwa hilo basi litamvuruga na kumnyima hatua ya juu zaidi. Kuna wakati unaweka …

617: Uchambuzi wa Kitabu, THE FIVE SECRETS YOU MUST DISCOVER BEFORE YOU DIE by John Izzo ( Siri 5 za Kugundua kabla hujafa )

Hakuna uhakika ulio wazi kama uhakika wa uwepo wa kifo. Watu wanaposikia habari za kifo huogopa na pengine hawataki kuzungumza zaidi kuhusu kifo na siku ya kufa. Hata waonapo vitabu juu ya masuala ya kifo huwa hawavutiki kuvisoma. Ila ni ukweli uliopo kuwa tumekuwa tukiona watu wakifa na ukweli mgumu kwetu kuwa nasi siku moja …

616: Hamasa yako ya siku ya kwanza iendeleze

Habari rafiki yangu. Siku mpya ya kuendelea na hatua zetu. Maisha ni zawadi na namna bora ya kuheshimu zawadi hii ni kuwa daraja kwa wengine kadri uwezavyo kila siku. Sisi binadamu tuna kawaida ya kuwa na shauku kubwa pale ambapo kitu bado hatujakipata. Utaona namna ambavyo watu wanakuwa na hamasa nacho isivyo kawaida. Lakini mtu …

615: Asili inapendeza na fursa ya kutalii ni njia ya kurejesha utulivu wa ndani wa maisha yetu.

Maisha ni zawadi. Mazingira yanayotuzunguka yanabeba uzuri wa maisha yetu yakichangiwa na uzuri wa viumbe hai mbalimbali vinavyofanya maisha kutegemeana. Ukianza kutafuta utulivu katika asili basi asili inao utajiri wa utulivu huu. Ukiona maeneo ya milima, maeneo ya vyanzo vya maji, maeneo ya misitu utaona namna utulivu ni sehemu ya asili. Ifikapo usiku hata anga …

Design a site like this with WordPress.com
Get started