594: April 11, Njia ya mkato ulokuja nayo siku unazaliwa ni uwezo ulio ndani yako.

Dunia kadri inavyozidi kukua ndivyo inavyozidi kuwa tele na utupu wake unazidi kujifichua utajiri wake. Kila kiumbe kina kitu ndani yake kwa ajili ya kuchangia kuondoa utupu uliopo na kudhihirisha kuwa katika utupu kuna utele. Kipaji, vipawa, uwezo wa kufikiri, kujenga taswira ni mazingira ambayo mtu huzaliwa nayo kuelekea mafanikio makubwa. Kadri mtu atajua na …

593: April 09, Wana hofu ukijifahamu ulivyo na uwezo mkubwa ndio maana wanakuzuia usipate nafasi ya kutulia na wewe wa ndani.

Si hofu kubwa katika tusoyajua ila ni hofu ile ya jinsi tulivyo na uwezo mkubwa ndani yetu. Unapojua ndani kuna uwezo mkubwa wa kufanya vitu basi wengine wanaanza kuona hofu namna utakavyoweza kufanya makubwa na hutaweza kusumbuliwa na wengine. Hii ndio hofu ambao wengine wana hofu na njia pekee ya wewe ushindwe kujua hili ni …

592: April 08, Nyanyuka tena kuanza safari maana bado safari inaendelea.

Maisha katika sura ya riadha huenda yakaeleweka kiwepesi zaidi. Riadha hutufunza masomo mapana kuhusu maisha hasa wakati ambao ni mgumu, kuchoka na kupoteza tumaini. Uzuri wa riadha uko pale ambapo ushindi na tuzo zinapotolewa. Huu ni wakati ambao mwanariadha husahau wakati ule ambao alikuwa amechoka, aliona kushindwa na kingine tumaini lilizima la kufikia taji na …

591: April 06, Utele unatokea popote pale utakapofungua fikra zako kuwa huru na moyo ulojaa shukrani

Utoshelevu wa maisha unafikika pale tu unapokuwa umefika hali ya kuona maisha yakiwa katika utele. Utele unapokuwepo na ndipo utoshelevu wa juu kabisa wa maisha nao hujitokeza. Utoshelevu na uhaba havikai pamoja. Utele ni kuona uwezekano wa mambo mazuri kutokea popote pale na hii kuonyesha kuwa Dunia haijapungukiwa ila ina utajiri uonwao kwa kufikiri chanya …

590: April 05, Watu hawakujali wewe wanajijali wao na matatizo yao.

Matatizo ndipo ilipo fursa ya kutoa thamani kwa maisha ya watu na huo ndio msingi wa fedha umejengwa na unapojengwa. Je huduma, ujuzi, kipaji au maono au bidhaa yako inasaidia kutatua tatizo/matatizo kwa maisha ya watu ?. Maana watu wanafanya vitu vingi kwa kujijali wao na eneo moja kubwa la kujijali wao ni kuona wanapata …

589: Makala: Ushairi, mshairi na jamii

Na; Malenga wa Ubena Hifadhi: Kijiji cha Ushairi Ninapokumbuka safari yangu ya ushairi siachi kukumbuka washairi kama wakina Shabaan Bin Robert, Kandoro wa Saadani, Amri Abeid Kaluta mshairi aliyeipaisha Kigoma wakati wake na mwingine bila kusahau basi ni Mshairi Mnyampala Eugene Mathias aliyeibeba Dodoma wakati wake. Haya majina yote yalisifika enzi zao na hata sasa …

588: April 1, Umia kwa muda ili uwe huru baadaye maana kadri unapokwepa maumivu kuyapitia unapishana na mafanikio

Kila mmoja anavutika na mafanikio yanapotajwa. Kuvutika huku kwa wengi ni yale matokeo ya mafanikio na si vile matokeo yalivyoweza kuzalishwa. Kinachozalisha matokeo ndipo ulipo mzizi wa mafanikio. Matokeo hayapo bila mchakato kuwepo na hii iko katika kila kitu na huwekwa mizizi na kanuni ya kupanda na kuvuna. Kazi ya kupanda ni ngumu kuliko sherehe …

587: March 31, Muda wako wa utulivu ndio muda pekee unaoweza kutafakari kwa kina juu ya maisha yako.

Zama tuishizo zina masumbufu mengi. Hizi ni zama ambazo watu wanajikuta hawana muda na maisha yao wakayaangalia yalivyo nje ndani. Kwa kuwa katika usumbufu huwezi kupata utulivu wa kutulia na ukayaangalia maisha yako kwa kina. Usumbufu wa mitandao ya kijamii, watu, matukio vyote hupoteza ubora wa muda wako wa kuwa peke yako. Utulivu wako ndio …

586: March 30, Uwezo wa kwenda zaidi ya tulipofika upo ikiwa tutajisukuma kukabili maumivu katika mchakato

Kila rekodi kubwa inayowekwa Duniani iwe katika michezo, maisha au eneo lolote lile basi watu wanaoweka rekodi hiyo wana jambo moja wanalofanana. Uwezo wa wao kujisukuma zaidi kupita kawaida ndiko kunakozalisha hawa watu na Dunia ikawaweka katika historia. Kujisukuma isivyo kawaida huwa kunaambatana na maumivu hasa katika mchakato. Vile uwezavyo kuwa na ustahimilivu mkubwa ndivyo …

585: March 29, Ukikua kiakili na kiroho kuuzidi mwili utaweza kutatua chochote kitakachoweza kukutokea.Mwili ni dhaifu na ndani ya

Mwili ni dhaifu na ndani ya mwili visivyoshikika vina nguvu kubwa kuushinda mwili. Ukikua zaidi ndani yako kiakili na kiroho mwili hata ukiwa dhaifu bado ndani yako utakuwa imara. Mwili huchoka, mwili huumwa, mwili hudhurika. Ila ukiwa na ustahimilivu wa kiakili na kiroho utaweza kukabiliana na chochote hata kama mwili utachoka. Ukiwa imara ndani ni …

Design a site like this with WordPress.com
Get started