ANZA 5; Usikate Tamaa, Ukikata Tamaa Walio Nyuma Yako Watakwama.

Unajua ni kwa namna gani ndoto ya mtu mmoja inaposhindwa kutimizwa si inamnyima mtu fursa ya kuifikia bali inawakwamisha maelfu ya watu ambao huenda maisha yao yangekuwa bora kwa mtu mmoja kuweza kutimiza maono au ndoto yake. Mtu anapokata tamaa kuendelea na kile alichokianzisha anafunga njia kwa maelfu ya watu nyuma yake. Kukata tamaa ni …

ANZA 4; Endelea Kutafuta Majibu ya Matatizo Yanayoisumbua Jamii

Jamii tunayoishi ina bahari ya matatizo ambayo kamwe hayawezi kuisha. Mafanikio yanapojitokeza basi na matatizo yanakuja kwa namna nyingine. Hivyo ukiweka nguvu hili eneo la kutafuta majibu juu ya matatizo yanayoisumbua jamii basi unaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maisha ya watu, ukafanikiwa na kuisaidia jamii kupiga hatua. Magunduzi yote ambayo tunayaona ni watu waliokuja …

ANZA 3; Anza Kutafuta Maarifa yahusuyo Unachokifanya

Hatua ya kuanzisha kitu ni ngumu ila inaweza kuwa nyepesi pale ambapo unaanza kuwa na mwanga kuhusu hicho kitu. Mwanga au nuru ya kitu haiji tu ghafla ila isipokuwa kuamka kimaarifa na kiufahamu. Ndo maana lipo himizo la utafute maarifa, ufanye tafiti na uulize walokutangulia ili upate hatua za kwenda. Watu wengi wameingia katika kushindwa, …

ANZA 2; Mwanzoni ni Pagumu Ila Usighairishe Ulichokianzisha

Safari ya chochote unachokianza ambacho hukuwahi kuanza ni lazima utakutana na kikwazo au changamoto kwa kukiona kigumu mwanzoni. Hili lipo kwa kuanzisha tabia mpya, kuacha tabia fulani, kujenga nidhamu fulani au kuanzisha mfumo fulani mpya. Akili zetu zinapenda mazoea yaliyo ya faraja “Comfort zones”. Sasa kinachotokea unapoanzisha kitu kipya ni kulazimisha akili itoke katika hali …

ANZA 1; Anzia Ulipo na Utarekebisha Mambo Mbele ya Safari

Tumejichelewesha sana kuanzisha vitu kwa kutafuta tuwe na kila kitu. Hili limefanya wengine hadi wafe na mawazo yao kwa kusema nitaanza nikiwa na hiki na hiki. Nani aliye na uhakika wa kuwa kesho itakuwa yake tena ?. Anza hapo hapo ulipo na kadri muda unavyoenda utajua wapi pa kurekebisha. Kungoja uwe na kila kitu utajichelewesha …

Unapenda Kusoma Vitabu?, twende Pamoja 2021.

Kila mwaka huwa ninaandaa orodha ya vitabu navyosoma mwaka unaoanza ingawa huwa naanza mwaka wangu mpya kila ifikapo mwezi wa 11 wa kila mwaka. Hili nimekuwa nafanya sasa kwa miaka mitatu baada ya kujifunza mengi kupitia Kisima cha Maarifa, kundi ambalo lipo chini ya usimamizi wa Kocha Dkt. Makirita Amani. Toka nimeanza kufanya hivyo imekuwa …

Orodha ya Vitabu 50; 2020 Katika Mwaka Wenye Changamoto Nyingi. # Maarifa ni Njia#

Mwaka huu nilijiwekea lengo la kusoma vitabu vichache "vitabu 22" tu ili niweze kuvidadavua kwa kina kitabu kimoja hadi kingine, lakini haikutokea hivyo kufuatana mwaka huu 2020 kuwa na mabadiliko mengi ya mambo. Hivyo nikajikuta nasoma vitabu vingi vingi kujifunza mambo mengi zaidi kuliko wakati mwingine wowote ule. Nimejaribu tu kuangalia katika baadhi ya vitabu …

Mambo haya 5 Yanakimbiza Wateja katika Biashara yako.

Biashara ni kiungo muhimu katika safari nzima ya kufikia mafanikio ya kiuchumi sehemu zote Duniani. Biashara inahusisha ubadilishanaji wa thamani kupitia bidhaa au huduma katika mfumo wa uuzaji na ununuaji. Wateja ndio injini ya biashara iendelee kuwepo au kufa. Wateja wanakuja katika biashara kwa msukumo wa mambo mawili; Mosi ni kutafuta kukidhi mahitaji fulani fulani …

Kupata Pesa dhidi ya Kutunza Pesa ?

Katika pita pita yangu nimekutana na mjadala mzito wa watu kuhusu mambo makubwa mawili kuhusu pesa. Kundi la kupata pesa na kundi la kutunza pesa. Ukiingia ndani kwa kina utaona haya maneno mawili yana tofauti kubwa. Kupata na kutunza. Unaweza kupata na usitunze. Huu udadisi ukanifanya nikutane na kitabu kimoja mtandaoni kiitwacho "The Psychology of …

Uchambuzi wa Kitabu -Persuasive Copywriting Using Psychology to Influence, Engage and Sell by Andy Maslen [Saikolojia Katika Ushawishi na Uuzaji wa Maudhui]

Dunia inakua kila siku hasa eneo la mawasiliano na majukwaa ya mtandaoni. Uwepo na ukuaji wa mitandao ya kijamii unaipeleka Dunia kuwa na ongezeko la watu hadi kufikia watu zaidi ya bilioni 5 kufikia 2040 watakaokuwa katika mitandao ya kijamii (Digital World). Hii ni dhahiri namna Dunia itakuwa zaidi ya kijiji kwa wakati huo.  Mapinduzi …

Design a site like this with WordPress.com
Get started