Ufahamu ni somo pana lakini ujinga ni zaidi. Kwa kuweka wazi hili basi jipe siku ya kuitazama siku yako kwa kina. Ianze siku yako kama alivyo mtoto akiwa na shauku ya kujua na hata kujaribu. Utaona namna ambavyo watu hata wenye mamlaka nao ni kama wengine katika kutofahamu mambo mengine. Watajua eneo fulani na eneo …
583: March 27, Vitabu vinavyokufanya ukue katika kuona mambo kwa kina ndivyo unavyopaswa kusoma kuyaelewa maisha.
Kuna ngazi 4 katika usomaji vitabu ambazo ndizo zinazotofautisha watu katika kusoma vitabu. Ngazi ya 3 ambayo ni usomaji wa kina ndio ngazi ambayo inaweza kubadili maisha yako na mtizamo wako juu ya Dunia na maisha ya mwanadamu. Ngazi hii hufaidisha msomaji kwa kuwa na vitabu vizuri ambavyo huibua hekima ndani yake na hata kubadili …
582: March 26, Kila kitu tunachokitafuta kipo ndani ya watu na kadri utakavyoweza kuishi vizuri na watu utapata kujua mengi.
Ujuzi pekee ambao huwa hauchuji zama na zama basi ni ujuzi wa kuhusiana na watu katika ngazi tofauti tofauti. Vile unavyoweza kuishi na watu na kuwaelewa jinsi walivyo katika nafasi zao ndivyo unavyoweza kujua kwa kina kuwa kila unachokitafuta hakipo sehemu yoyote ile ila ndani ya watu. Hivyo kauli ile utajiri mkubwa Duniani basi ni …
581: March 25, Dhibiti nguvu inayopotea uitumie kupiga hatua kubwa na maisha yako.
Maisha yetu hubeba uhai pale ambapo nguvu au nishati inapokuwepo. Nishati ya kwanza ni kutokana na chakula ambacho hutupa nguvu. Nishati ya pili ni maarifa kama chakula cha akili. Hii nishati ya pili ndio yenye nguvu kufanya uweze kupiga hatua za juu zaidi za maisha yako. Hisia hasi au taarifa hasi hunyonya nguvu ya mwili …
580: March 24, Usitarajie chochote kile unapofanya jambo na kwa kufanya hivi utaishi kwa furaha siku zote za maisha yako
Ni hulka yetu sisi binadamu kuwa huwa tunasukumwa kufanya vitu ili baadaye nasi tutarajie kupata mrejesho. Ikitokea matarajio ya kile ambacho tulikifanya hayajafika vile ambavyo tuliwaza basi furaha yetu yote inaweza kupotea na tukaingia katika huzuni. Matarajio sana katika maisha kumefanya watu wengi waipoteze furaha kuliko kuwa na furaha. Pale utakapoishi kwa kufanya vitu na …
579: March 23, Kadri ndani yako unavyokua kiroho ndivyo unavyoweza kustahimili chochote kile kinachoweza kukutokea.
Ulimwengu wa ndani ni ulimwengu usio na kikomo na una utele. Mtu ni kiumbe wa kiroho na kadri maisha yake ya kiroho yanavyozidi kuwa ya kina ndivyo anavyoweza kuwa tayari kukabiliana na chochote kile na kisiweze kumwangusha. Maisha ya kiroho ni zaidi ya mifumo ya dini na ni zaidi ya vile watu wafikirivyo. Maisha ya …
578: March 22, Ni kawaida kuchoka upandapo mlima lakini haimaanishi kuacha kupanda mlima.
Kuchoka ni sehemu ya maisha. Tumekuwa tunaona vitu vikichoka na hata mili yetu huchoka. Kuna kuchoka na mwisho kama ni kitu kushindwa kabisa kufanya kazi. Mbali na hilo unapokuja kuyaangalia maisha kama mpandaji mlima utaona kuchoka kupo lakini hakuna maana kuwa ndio mwisho wa safari. Safari huendelea ili kuweza kufika juu palipokusudiwa kufikika. Kujisukuma kuendelea …
577: March 21( jana ), Jipe dakika 5 hadi 20 za kushukuru kwa kila mambo mazuri yanayoendelea katika maisha yako.
Wengine siku inapoisha sababu ya vile alivyoitafsiri siku anaona siku nzima hakuna hata jambo zuri ambalo anaweza kuhesabu kuwa kalipata au analo. Ni rahisi sana kusahau uzuri pale ubaya unapokuwa umeingia. Lakini hii haimaanishi usahihi kuwa hakuna uzuri au hakuna mambo mazuri yanayoendelea iwe kwa mtu au Dunia kwa ujumla. Kuna mambo mazuri yanayoendelea katika …
576: March 20, Unapotaka kupiga hatua kubwa hesabu kila siku kama siku inayojitegemea
Utapata kuona ukifanya makubwa na maisha yako pale ambapo utaichukulia leo kama siku inayojitegemea na kama vile umesahau yalopita nyuma na yajayo huna hakika nayo. Hivyo akili na nguvu zako zote unajikuta ukiziweka sasa na kwa njia hiyo ufanisi unakua mkubwa na siku inaisha ikiwa na ujazo. Mbali na hapo leo unapohusianisha na jana au …
575: March 19, Kila siku tafuta kitu cha kukiendea kukijua kwa kina na ndivyo utakavyoweza kuyaelewa mengine yanayoendelea katika maisha yako.
Kuna kitu kimoja ambacho kilifanyiwa tafiti kwa kuona uhalisia kuwa jinsi watu wafanyavyo kitu kimoja ndivyo ilivyo ufanyaji wa vitu vingine hautofautiana na jinsi afanyavyo kitu kimoja. Kama mtu wa kupuuzia baadhi ya vitu basi upuuziaji huo unaweza ukatokea hata kupuuzia mambo makubwa ambayo yanaweza kuathiri kabisa maisha. Hivyo ili kuzuia hili tafuta kitu kimoja …