Moja uwe na mtizamo sahihi wa kukiona kitu kilivyo, pili kuchukua hatua na tatu ni mapenzi ya msukumo kufanya mtizamo na kuchukua hatua viende pamoja. Hatua hizi 3 hazitakuwa nyepesi hata kidogo na utakaposhindwa kuzifuata hutaona changamoto ikiwa kama njia kwako. Wewe sio wa kwanza kupitia changamoto kama ilivyokuwa zaidi kwa wakati ule wa kale …
573: March 17, Ufahamu wenye manufaa ni ule utakaopata kwa kuingia kukifanya hicho kitu mbali na hapo unajua nadharia tu. Hutaweza kujua maana ya kitu kwa k
Hutaweza kujua maana ya kitu kwa kusikia au kuambiwa hadi pale ambapo utaweza kukipitia hicho kitu ndipo ufahamu wako wa hicho kitu unaweza kuwa wa kina zaidi. Nadharia juu ya kitu hazina nguvu kama ilivyo nguvu ya hali ambazo utapitia kitu ambacho umekisikia au kuambiwa tu. Matokeo ya maisha na kweli ya maisha ipo katika …
572: March 16, Unavyoiishi jifunze namna bora ya kuishi bila kuchoka hadi siku ambayo ni nafasi yako ya mwisho ya kuishi.
Moja ya swali ambalo linaendelea kujibiwa hadi siku tunayoondoka Duniani ni namna gani bora ya kuishi. Maisha bora ni aina gani ya maisha ?. Hili ni swali lenye uzito wa juu kuzidi yale kama unaishi kwa kusudi gani na nini maana ya maisha. Namna bora ya kuishi wakati tunaishi ni swali ambalo limekuwa likiendelea kutafutiwa …
571; March 15, Uwezo wa kubadili kila changamoto iwe fursa ya mabadiliko unaanzia kubadilika unavyofikiri mambo wakati huo huo.
Msemo wa badili kila changamoto kuwa njia au fursa inawezekana usiweze kueleweka na wengi na kuonekana ni nadharia na hakuna uhalisia wowote ule. Ila kuna matokeo bora sana ya kuyapitia ukaona ni jambo lisilokungoja kwa kila changamoto kuikabili kwa kubadili kuifikiri kama ndio fursa ya kukupa mafanikio makubwa. Ni mpaka ubadili kufikiri juu ya uionavyo …
570: March 14, Ni muhimu kutambua upya kuwa kila jambo hubeba wakati wake na ukitambua mapema ni faida kwako kuliko hasara
Kuna mambo huwa yanaeleweka yenyewe na kirahisi pale ambapo hupita na kisha ukiangalia nyuma unagundua vile ulivyokuwa na nafasi nzuri sana ya kufanya vitu. Pale unaposema nitafanya siku zijazo na hujaona leo kuna uwezekano zifikapo siku zijazo utakumbuka nyakati kama hizi zilikuwa na nafasi ya wazi ya kuchukua hatua. Kugundua mapema kuwa huu ndio wakati …
569: March 13, Akili inayozurura haiwezi kufanya makubwa katika siku.
Zama tuishizo licha kuwepo kwa maarifa tele lakini bado watu wengi wanasita kuchukua hatua. Akili zimekuwa zinazurura bila kutulia sehemu moja na kazi ikafanyika hadi mwisho. Utaona vile miili yetu inavyoona kupungukiwa pale unapofanya kazi na huku simu ikiingiza taarifa toka katika mitandao ya kijamii. Akili imekosa utulivu na kama tungeweza kuona ikashikika basi ingekuwa …
Continue reading "569: March 13, Akili inayozurura haiwezi kufanya makubwa katika siku."
568; March 12, Unavyoviona na kufikiri ni vitu vidogo ndivyo kazi kuvidhibiti na kuvisimamia.
Mfano umejiambia utakimbia kila siku ili uimarishe afya yako na huenda ukaona ni jambo rahisi. Siku ya kwanza ukaanza kwa hamasa hadi siku ya 3 mwili ukaanza kukupa sababu na ukajikuta umeacha na imepita miezi sasa hukimbii tena. Huu mfano mmoja ila kuna maeneo mengi katika maisha yetu tunaweza ona rahisi mwanzoni lakini nidhamu ya …
567; March 10, Sema unaweza na utafanya hata kama jambo ni gumu.
Ili mafanikio yaje lazima ujifunze kufanya vitu vinavyoonekana vigumu kuwezekanika. Lazima ujenge nidhamu ambazo hukuwahi kuzifanya ili uvute mafanikio. Haitaishia hapo utahitaji ujenge tabia ambazo hazitakuwa rahisi kwako kuzijenga ili ushawishi na uwe na sifa za mtu ambaye atafanikiwa. Lazima ukubali ugumu sasa ili mambo yawe rahisi ijayo yako. Lazima ukubali kushinda changamoto katika maisha …
Continue reading "567; March 10, Sema unaweza na utafanya hata kama jambo ni gumu."
566: March 09, Kuna utoshelevu mkubwa utaupata ukimaliza kazi ulopanga umalize kwa siku husika
Kazi ni uhai na katika kazi ndipo ulipo utoshelevu. Matokeo ya kazi yana raha yake kubwa na moja ni utoshelevu mkubwa unaokuja baada ya kumaliza kazi husika. Katika kazi zote ambazo utazifanya jua kuwa hakuna kazi nzuri kama ya kuwa daraja kwa wengine. Hata kama haitakupa kile ulichotamani ukipate lakini maisha yanayofanyika daraja kwa watu …
565: March 08, Mwili utaharibika lakini kitokacho ndani ya mwili kabla ya kuharibika hudumu miaka mingi.
Mawazo, ubunifu, uandishi ni zao la ndani la mtu lililo katika mfumo wa kufikiri na nafasi ya kiroho ya maisha ya mtu. Tulipo sasa bado tunakumbuka kazi za watu ambao miili yao hutaweza ipata sasa lakini kile walichokitoa kwa ajili ya Dunia bado kinaishi hadi sasa. Vilivyo ndani yetu tunapovipanda siku za uhai wetu huendelea …