564: March 07, Usishangazwe na kuondoka kwa vitu maana kila tulichonacho tumeazimwa kwa muda

Hatuna tunachokimiliki milele katika maisha yetu. Kila tulichonacho sasa tunacho kwa muda hapa ni pamoja na uhai wetu. Kila kitu ni kama tumepewa kwa muda tuwe navyo kisha ufikapo muda viwe mbali nasi. Maisha yetu, nguvu zetu, watu wetu wa karibu wote kwa ujumla wao wapo kwa muda na siku vitatutoka viwe mbali nasi. Inawezekana …

563: March 04, Unachokipenda kina nguvu pande mbili iwe ni kukupa mafanikio makubwa au kukuingiza katika mateso makubwa

Upendo ni nguvu yenye upekee inayofanya ushawishi ambao pengine hata fedha au mambo mengine yoyote yale yashindwe kufanikisha kushinda upendo. Upendo ni msukumo wa ndani ambao una nguvu ya kumsukuma mtu kufanya kitu. Iwe katika kupenda kilicho bora kufungua mafanikio au upendo huo huo ukafungua njia ya mateso kwa mtu huyo. Sababu ya upendo watu …

562; Marchi 03: Maisha ni safari nikianguka napaswa kunyanyuka tena kwa kusonga mbele na safari.

Maisha ni riadha. Jinsi zilivyo mbio fupi na ndefu mkiambiaji akianguka hunyanyuka tena kwendelea mbele kufikiri hatma ya mchezo wake. Ushujaa na ukomavu wake huwa katika kunyanyuka tena na kuchukua hatua ya kusonga mbele. Hivi ndivyo maisha kwa walio na ustahimilivu huwa siku zote. Watakutana na vikwazo na vitawaangusha lakini watakuwa na nguvu za kunyanyuka …

561; March 02, Usishindane na matukio ya maisha hayataisha ila wewe utapoteza nguvu ukitaka mashindano

Maisha kila siku yamebeba matukio na visa na imekuwa hivi zama zote sisi si wa kwanza kuwa na hali kama hizi. Utapoteza nguvu na muda kusema ushindane na matukio yanayotokea katika maisha unapotaka kuyafuatilia yote na kutaka kujua kiundani. Utachoka wewe na utashindwa wewe ukitaka upambane nayo na kufuatilia yote. Achana nayo kama wataka kupiga …

560; March 01, Ninapoona hakuna njia nitumie hicho hicho kikwazo kiwe njia ya kufungua mlango wa kutokea

Mambo yanapokuwa mazuri ni hulka ya binadamu kutofikiri kuwa kuna wakati mambo yanaweza kwenda tofauti na hapo ndipo vikwazo hubeba nguvu na watu hukwama kutoka hapo. Changamoto au vikwazo vyaweza kuziba njia usione pakupita lakini kwa watu ambao wamedhamiria kupiga hatua na maisha yao hizo hizo changamoto huzigeuza na kuwa njia au mlango wa kutokea. …

559; Kitabu mwezi wa 3, Uchambuzi kifupi; The RETAIL DOCTOR’S, A Guide to growing your Business by Bob Phibbs ( Mwongozo wa kukuza Biashara yako )

Rafiki karibu tena katika kitabu chetu cha 3 kwa kina kila tunapokaribia mwezi mpya kuanza. Kwa miezi miwili ilopita Januari na Februari tuligusa vitabu viwili kimoja kiligusa juu ya kukabiliana na kujidhibiti hasira katika maeneo ya kazi na kingine juu ya mtu kama Mfalme wa fikra, roho na mwili wake mwenyewe. Na kitabu cha mwezi …

558; February 28, Maamuzi yote nitakayofanya nikiwa na hasira yatakuwa ya ovyo na kujichelewesha kuchukua hatua nikiwa na hasira ni ukomavu.

Hasira ni nguvu na ikishindwa kudhibitiwa ina uwezo wa kumfanya mtu apate kurukwa na akili kisha akaamua pasipo kufikiri na maamuzi yake mengi huwa ya ovyo na majuto baada ya tukio lilofanywa na hasira. Hasira hukaa kifuani mwa mtu mpumbavu na anayeshindwa kudhibiti hasira ni mtu kushindwa kushika hatamu ya hisia zake na matendo. Matokeo …

557; February 27, Nitakapoweza kuipa uzito kauli ya niishi leo kama siku yangu ya mwisho nitafanya mambo makubwa Duniani.

Moja ya sababu kubwa ya hofu ya kifo ni kuwa maisha yetu hatuishi kitoshelevu na tunaishi kana kwamba kesho zitaendelea kuwepo. Pale ambapo tunaona wengine siku kama hii hawapo na walikuwepo basi ni dhahiri kifo nasi kitabisha hodi siku moja. Kufahamu hili katika uwazi basi latupa himizo la kuishi sasa, la kushughulika na maisha yetu …

556; February 26, Vuta subira mengine unayopitia hujipembua yenyewe kadri muda uendavyo utaelewa sababu ya kutokea kwake.

Kuna mambo yalopita unaweza kuyaelewa sasa kwanini yalitokea na yepi ambayo umejifunza kwayo. Na huenda kwa wakati ule hukuweza kuona hilo sababu binadamu ni hulka yake kuona karibu kuliko kuona mbali na kutamani vya mbali na kuvipuuza vya karibu. Subira ni ukomavu na hutaka utulivu mkubwa hasa katika mambo yagusayo moja kwa moja hisia zetu. …

555; February 25; Msingi wa fedha ni thamani na nguvu ya fedha yapaswa kudhibitiwa lasivyo inaweza kukuharibu

Fedha ni thamani na kila unapokuza na kuongeza thamani kupitia ufanyacho ndivyo unavyoweza kutengeneza fedha zaidi. Pale unapozipata hupati tu fedha kama fedha ila fedha kama nguvu ya kufanya vitu vilivyokuwa kazi kupatikana vipatikane. Fedha ni nguvu na hii nguvu iletwayo na fedha ndio kiini cha mazungumzo yetu leo. Fedha ni nguvu inayokupa uone majibu …

Design a site like this with WordPress.com
Get started