534; February 06, Anayekutusi mchukulie aliyefanya tendo hilo ni vile afanyavyo mtoto.

Mtoto hufanya vitu au mambo pasipo ufahamu wa kina wa mambo kwanini kafanya hicho kitu. Ndo maana wakati mwingine viboko hutumika kuonyesha ni namna gani baadhi ya mambo afanyayo hayafai kufanywa aachane nayo afwate njia nyoofu. Lakini jambo ambalo anafanya mtoto huwa linaeleweka sababu ya utoto wake hivyo anachukuliwa jinsi alivyo kuwa yeye ni mtoto …

533; February 05, Unapofanya kitu kiwe endelevu asili hukipa jina hicho kitu.

Tupo darasani kila siku hasa darasa la maisha. Pale unapoamka asubuhi ukitegemea siku iwe nyoofu kama vile ambavyo ulitaka iwe lakini mambo yanakwenda vile yapendavyo yenyewe. Hivi ndivyo maisha hujipa kuwa darasa linalodumu kwa viumbe wake hasa viumbe wenye upevu mkubwa kama binadamu. Mimi na wewe kila siku kuna nafasi ya kujifunza katika yale ambayo …

532; February 04, Usihangaike kutolea maoni kila kitu vingine viache kama vilivyo.

Msingi mkuu wa maisha yenye furaha ni maisha ambayo yamejaa utulivu wa ndani. Utulivu ni kama ngome isoweza kutikiswa na chochote toka nje. Umewahi ona jinsi maji yaliyo matulivu yalivyo ? na umewahi onana na watu wenye utulivu walivyo ?. Kama umewahi kuona na kuwaona utakubaliana nami namna ni watu wenye nguvu na kama ni …

530; February 2; Unaenda wapi ulipo pana kila kitu.

Mtu ni hulka yake kutamani na kupuuza alichonacho. Ni hali ambayo humnyemelea siku zote katika mambo yake kuona alichonacho hakina maana hadi kipotee. Ni rahisi kuona vya mbali kuliko vilivyo karibu yake. Maisha haya yanaweza kumkosesha mengi, kuzipoteza fursa nyingi na kingine atafutacho hakipo mbali na yeye bali hujitaabisha kutafuta kisha huja kugundua atafutacho anacho …

529; Kitabu cha February 01; Uchambuzi wa kitabu; MAN: King of Mind, Body and Circumstance by James Allen ( Mtu: Mfalme wa Fikra, Mwili na hali zimzungukazo )

Tatizo kubwa la maisha liko katika kujifunza namna gani ya kuishi. Kama ilivyo mtihani mkubwa kwa mwanafunzi wa awali katika kujua kutoa na kuongeza. Ndivyo ilivyo katika maisha mtihani wa nini utoe au kuongeza katika maisha ni swali gumu ambalo halijibiki kirahisi. Lakini ifikapo ubobezi na kujua vitu kujapo magumu hujiondoa yenyewe. Mbali na kutokujua …

528; January 31, Changamoto yako ni ndogo kama ungejuwa wanazopitia watu wengine.

Moja ya ahadi ambayo nilokuwa nimejiwekea mwaka huu 2019 ni ya kujisukuma kila siku kuandika katika wakati ambao naona ni wakati mgumu kuandika. Wakati huu unaweza ukawa na sababu za kutosha kabisa kuwa kwanini usipumzike na kisha ungoje siku nyingine ?. Lakini hili nimelikataa na kusema nitakuwa naandika hivyo hivyo na kuona huwa inakuaje kuandika …

527; January 30, Akili imezoea kuzurura idhibiti

Habari Rafiki ni siku nyingine ambayo ni zawadi tumepata kuitumia ili tuweze kupiga hatua kubwa na maisha yetu na wale wanaotuzunguka. Zawadi ya kuwa hai ni zawadi kubwa ambayo kama ingekuwa inanunuliwa basi wengi wangeweza inunua lakini haiko hivyo. Mshukuru Mungu kwa nafasi hii na kuitumia katika kujifunza na kusaidia wengine kwa ulivyojaliwa ni njia …

526; January 29, Kila unachokitaka lazima ulichonacho ukipoteze

Habari Rafiki naamini kila siku kwako unaipa uzito kama vile ni siku ambayo ikipita imepita huwezi kurudia tena kuishi. Kila siku ni fursa ya kujifunza vitu kwa kina na unajiona kadri unavyoendelea kuishi unagundua kumbe vitu ulivyokuwa unavijua kwa undani kumbe hujui kwa kina. Hili linatokea na ndilo ambalo linatupa nafasi ya kuwa hitaji la …

525; January 28; Dhibiti hasira zako ufanye maamuzi sahihi

Hasira ni hisia kali ambayo wengi wanaoshindwa kuidhibiti basi huwapelekea kufanya maamuzi ya ovyo. Kwa kuwa wakati ijapo hasira uwezo wa kufikiri hushuka na hisia huwa juu kufanya maamuzi. Mara zote ambapo hisia huwa juu basi kufikiri huwa chini na hapo maamuzi yote yafanyikayo huwa yana majuto baadaye. Hasira ni kupata kurukwa na akili kwa …

524; January 27, Usipofushwe na mwonekano wa nje wa watu ushindwe kuona uhalisia wa watu ulivyo na maamuzi ya kundi kufanya unavyofikiri kunaweza kukuondoa katika uhalisia.

Rejea ya Maarifa; The LAWS of HUMAN NATURE by Robert Greene ( SHERIA za ASILI ya BINADAMU ) Mara nyingi tumekuwa tunapotea kabisa kuona uhalisia pale ambapo watu wanaoonekana kwa mwonekano nadhifu na tabasamu kuonekana ni watu ambao tunaweka imani kwao haraka zaidi kuliko ambao mwonekano wao si nadhifu. Tumeona wazi wazi vile hata watu …

Design a site like this with WordPress.com
Get started