523; January 26, Unachofikiri ni tatizo sio tatizo ila tatizo kubwa ni wewe

Habari Rafiki naamini unaendelea na hatua zako bora sana. Kila siku tunapoteza sehemu ya maisha yetu, nguvu zetu na kingine umakini wetu. Rasimali kama nguvu ni kuhifadhi sana kwa kuepuka habari hasi na watu wanaokatisha tamaa. Huku umakini unaulinda kwa kuilinda akili yako isitoroke toroke kwa kujua ambacho unakifanya kwa wakati huo. Ukiweza kuhifadhi rasimali …

522; January 25, Utafanikiwa kama utaendelea kuwa mwanafunzi wa maisha

Leo imekuwa siku bora sana nikiwa bado naendelea kujifunza mengi katika safari ya maisha. Moja ni vile ambavyo tuna siku zisizo nyingi za kuishi kwa kuona baadhi ya watu wakiondoka kama majani juu ya mti lakini huu ndio uhalisia ambao haukwepeki na jambo la pili ni juu ya maisha ya maana na bora. Maisha ya …

521; January 24; Jua Vichache ila kwa kina

Habari Rafiki naamini unaendelea vizuri na hatua zako za kila siku. Kujifunza ni hitaji muhimu kwa mafanikio kama vile damu katika mwili basi kujifunza na kufanyia kazi ndio msingi katika safari ya mafanikio. Kadri unapojiwekeza ndani yako kwa maarifa ndivyo na wewe unavyozidi kufupisha njia yako kuelekea hatua kubwa za maendeleo. Ishukuriwe nafasi ya teknolojia …

520; January 20, Kiwango chako cha kufanikiwa kipo katika utatuzi wa matatizo ya jamii.

Habari rafiki naamini kila siku kwako huwa unaipa uzito kama vile ikishapita haitakuja kuwa tena hivyo. Kila siku huja na kupita na muda na nguvu zetu kimoja huwa hatuna siku zote. Nguvu zetu zinaenda zikiisha kila siku na kiwango cha uthubutu wetu huwa hakiwi sawa na vile ambavyo mtu akiwa kijana au alivyokuwa mtoto. Hivyo …

519; January 19, Jamii 100~ KITABU;The Power of Creative Intelligence(Nguvu ya Akili bunifu) by Tony Buzan.

Ubunifu ni uwezo wa kuandaa na kuleta wazo jipya, kutatua matatizo katika namna halisi yenye upekee na kuonekana mbele ya jamii kwa kile unachokifanya. Mwandishi anaelezea namna ubunifu unavyoweza kukufanya ufanikiwe zaidi anatupa mbinu mbalimbali ambazo tukizitumia tutafanya mambo bora Kama alivyofanya Leornado da Vinci ambaye ni mfano bora kabisa kwetu. Mambo ambayo nimejifunza katika …

518; January 18, RUDI KUWA WEWE

Habari Rafiki ni siku nyingine tena ya kuangalia maisha yetu yalipo na wapi tuendako. Siku kama hii ni fursa kubwa ya kuchukua hatua na kuanza vitu tukiwa na nguvu bado lakini tukiwa na nafasi ya kuwa hai. Maisha yetu yanaisha kila siku na inakuwa hatari sana pale yanapoisha na tukiangalia nyuma hakuna hatua kubwa ambazo …

517; January 17, SOTE TUNA VIBANZI SHUGHULIKA NA CHA KWAKO

Rejea ya Maarifa; Hoja za Karugendo, Gazeti Mwananchi Na. 6739 Ukurasa wa 18. Habari ya siku mpya Rafiki ni leo ambayo kwa wakati wa jana ulisema ikifika basi utaanza au kuchukua hatua. Kila siku ni nafasi ya wazi ili tujiboreshe na tuongezeke kifikra ili tuweze kukua na kupata maendeleo. Hakuna maendeleo katika fikra ambazo zinakwepa …

516; January 16, Nyuma ya pazia ndipo penye siri sio ukionacho sasa

Habari Rafiki siku inapoisha huwa ni jambo gani kwako unalikumbuka ?. Kama unakumbuka ni jinsi gani siku yako ulivyoipoteza pasipo kufanya jambo lenye kugusa maisha basi jionee huruma sana na ujiadhibu kabisa kwanini unapoteza sehemu ya maisha yako. Kila siku ni kama tunakufa kidogo kidogo kabla ya kifo halisi siku kuwa kati kati yetu. Je …

515; January 15, Kusikiliza hupelekea kuwa na hekima

Habari Rafiki kila siku katika maisha yetu huja kama zawadi na wenye kuifungua ni sisi wenyewe kwa maana ya kujimimina katika vilivyo ndani yetu ( ujuzi, uzoefu, kipaji, maono, mawazo ) katika kusaidia wengine wapige hatua. Maisha yako yakikosa kugusa maisha ya watu wengi basi kuna kiwango chako cha ndani hujakitumia ipasavyo na muhimu kujiona …

514; January 14, Fedha itakufuata ukishaweka mazingira ya yenyewe kuja kwako

Maisha ni kanuni na kadri unavyokwepa kanuni za maisha kuna mambo ambayo ulitakiwa upate kirahisi utalazimika kuingia gharama kubwa zaidi na gharama hiyo ni upotevu wa muda na nguvu. Kuna matokeo bora sana kila wasaa ambao utakuwa unafuata kanuni hasa kanuni za maisha ambazo zimekuwa zinatoa majibu sawa na vile watumiavyo wengine. Fedha ni eneo …

Design a site like this with WordPress.com
Get started