513; January 13, Mambo hayakai yakadumu hufika wakati hupita.

Habari Rafiki ambaye huachi kujifunza kila siku ukijua wazi kuwa bila kujifunza hakuna ukuaji na ukikosekana ukuaji hakuna maendeleo. Hongera kwa hii hatua nzuri ambayo unajisukuma kupiga hatua zaidi ya ulipokuwa jana. Karibu katika kujifunza tena katika yale ambayo yanatutokea, tunayaona na yalikwisha kutokea. Unapokuwa katika wakati mgumu au wakati wenye wingi wa changamoto utaona …

512;January 12, Itachukua muda vuta Subira

Maisha na asili ni walimu walio wazuri katika kuishi kwetu siku zote hapa Duniani. Masomo mapana na ya kina yapo katika haya maeneo mawili ya kuishi kwetu maisha na asili. Kuna mengi ambayo yamefichwa ndani ya maisha na ndani ya asili yasoweza kuwa rahisi kupatikanika kwa watu ambao wanachelea kujifunza. Asili inatufundisha juu ya kungoja …

511; January 11, Ushindi mkubwa ni kuzishinda hisia na kutawala mawazo yako

Habari Rafiki kila siku ni siku ambayo inatupa nafasi ya kujifunza maisha kwa kina ikiwa tutakuwa tayari kujifunza. Tukikosa tu kujifunza basi tunakaribisha maisha ambayo hayafai kuishiwa. Safari ya kujifunza ina faida nyingi kuliko hasara za kutojifunza. Kujifunza kila siku ni kujiweka kuwa imara na maisha yako yanakuwa bora kila siku zaidi ya siku ya …

510; January 10~PIGO MOJA la NYUNDO HALITOSHI KUPASUA MWAMBA

Maisha ya wadudu yanaweza kutupa somo kubwa sana na moja ya somo kubwa la hekima ni katika hawa wadudu wawili ambao nimekuwa najifunza mengi ikiwa ni kwa zaidi ya miaka 20 sasa ni juu ya uendelevu wa kila siku na hatua ndogo ndogo zao kufanya mambo makubwa. Ukimtazama mchwa utaona jinsi ukubwa wa vichuguu vyao …

509; January 09, Zawadi pekee ya kujipa ukiwa peke yako ni kufikiri juu ya maisha yako

Maisha yetu yanaweza kuwa bora sana endapo tutajipa wasaa wa kuyaangalia kwa kina maisha yetu na wapi tulipokuwa mwanzo, tulipo na kule tuendako. Tafakari ya kina kama hii ni wasaa wa maisha bora sana ambayo si wote wanaweza kupata. Jinsi ambavyo ratiba na mambo mengi yamewabana sana wasiweze kufikiri juu ya maisha kunazidi kuwa na …

508; January 8, AMA ULIPE SASA GHARAMA au ULIPE BAADAYE ZAIDI ?

Maisha ni mchezo wenye hatari kubwa sana na hatari huanza siku ya kwanza ya kuzaliwa na huendelea hadi siku ambapo mtu hufa. Maisha yamejaa mambo mengi na katika mambo mengi kuna nafasi ya maisha kuwa na uhalisia. Uhalisia huu huwezi kuutenga na gharama. Gharama hii ulipe sasa au baadaye lakini kulipa utalipia wakati ukifika. Pengine …

507; January 7, Walofanikiwa hufanya mambo magumu ili mafanikio yawe rahisi na ambao hawafanikiwi hufanya mambo mepesi na mafanikio kwao huwa magumu.

Habari Rafiki ni siku mpya tena na ya pekee sana. Siku kama hii kuna wengine hawajaiona na wengine ambao walitutoka zamani walitamani zama kama hizi wangeona yale ambayo walitamani yawakute kabla ya kufa kwao. Hivyo mimi na wewe kuiona siku hii ni nafasi adhimu kumshukuru Mungu na pili kuitumia kitoshelevu maana nasi siku itakuja hatutapata …

506; January 6, NI KWELI NI BURE lakini Gharama ya Kuchukulia kwa uzito ni Kubwa.

When information is cheap attention becomes expensive ~ James Gleick Habari Rafiki wiki ya kwanza ya mwaka 2019 imeshaondoka hiyo na hivi ndivyo maisha yetu yanavyosogea na hata nguvu zetu zinaenda zikipungua na kama tunakosa kujifunza hili basi siku za mbele yetu tutajutia sana nafasi hii ya sasa kuwa tungelitumia kwa utoshelevu zaidi. Mbali na …

505; Januari 5, Muda na ukweli ni Pacha. Hutaweza kushindana na Muda.

Time discovers truth ~ Seneca Habari Rafiki naamini siku yako imeanza vizuri na hata ikiwa haiko vizuri jaribu kubadili kufikiri na kuyaona mambo na kisha utaona sio tukio la nje lenye hatari bali ni wewe ulivyotoa tafsiri. Leo ni fursa ya pekee ambayo kwa wengine haijawa hivyo ila kwako hadi kusoma hapa ni wazi u …

504; Januari 4, UKIKOSA HAMASA angalia ambayo tayari umeshayafanya.

Maisha yetu wakati wote si sawa utakutana na mambo yakaenda tofauti kabisa na ambavyo ungetazamia yawe. Kuna siku ambayo utaamka na kuona hamasa huna ya kufanya kazi na hata ukashawishika kabisa uache na siku ipite tu. Wakati huu usipojua hatua ya kuchukua basi ni wakati ambao unaweza kukupotezea muda na nguvu wa kufanya mambo yaweze …

Design a site like this with WordPress.com
Get started