503; Januari 3, UNAVYOWEZA kuwa SALAMA kwa neno HAPANA.

It's only by saying No that you can concentrate on the things that are really important ~ Steve Jobs. Habari Rafiki. Kila siku ni siku mpya kwetu ya kwenda kupiga hatua kubwa. Masaa ambayo tunayo leo ni zawadi muhimu sana kuitumia kupiga hatua na kugusa maisha ya watu wengine. Ulipo hapo kuna matokeo mengi mabaya …

502; Januari 2, MAARIFA yatafupisha SAFARI ya MAFANIKIO yako.

Habari ya wakati huu. Kila siku ni siku ya kuanza jambo na fursa ya kugusa maisha ya watu wengine kwa kile unachokifanya. Na chaguo la kuyapenda maarifa litakuwa chaguo na zawadi bora ambayo unajipa itakusaidia maisha yako yote hapa Duniani. Safari ya mafanikio si nyepesi na kama ingekuwa nyepesi ungeona kila mmoja kafanikiwa. Safari ya …

501; Januari 1, USIRUHUSU KUJIKWAMISHA MWENYEWE

Rejea ya Maarifa; FIKRA PEVU DARASA Hamasa ya siku ya kwanza ya mwaka huwa ina nguvu na huwa si sawa na siku itakayofuata ambapo watu hurudi katika maisha yale yale ya mazoea. Huwezi kupata matokeo tofauti kwa njia zile zile siku zote na hii ndio ambayo inawafanya watu wengi waone hawapigi hatua licha kuwa siku …

500; Ushindi katika ugumu makala ya 500 na 2019 nataka kwenda kuandika wakati ambao sijikii kabisa kuandika na niandike wakati changamoto ziko nyingi na usumbufu na safari nyingine ya siku 365 za MALENGA MENTAL MODEL na Falsafa ya Hatua ndogo ndogo.

Rafiki leo ni makala yangu ya 500 toka nimeanza kuandika na kuwa na utaratibu mzuri wa kuandika. Asante kuwa rafiki yangu maana wewe ndiwe umenipa sababu ya kuandika na nisiache kuandika hadi siku utakaposikia sipo. Kuandika ni kazi ngumu lakini huwa nyepesi ikiwa wafanya kama sehemu ya maisha yako na siku utakapoondoka waje wafaidike wengine …

499; Jamii 100, Tabia pekee ambayo unaweza kuijenga kwa mwaka 2019 itakayokupa hatua kubwa basi ni USOMAJI VITABU na kufanyia kazi.

Rejea ya kitabu; WISDOM by Elijah Mwape ( HEKIMA ) Habari Rafiki naamini siku yako imekuwa bora na mwaka ndio waishia hivyo na ikiwa nafasi nyingine itatokea basi kuamka kwa siku nyingine basi itakuwa ni mwaka 2019 na si huu mwaka tena. Kuwa hai ni fursa maana ukitazama nyuma ni wengi hawapo ila wewe upo …

498; NJIA ya KUTOKA, Kama unamiliki simu janja una kila sababu ya kupiga hatua labda kama huoni fursa.

Maandishi haya ni muktadha wa nchi yetu zaidi ( sisitizo ) Habari Rafiki ikiwa katika siku chache kabisa za kumaliza mwaka ni wasaa mzuri sana wa kuangalia ulikuwa wapi na upo wapi na wapi uendako. Maisha yanaenda kwa kasi sana na vile unasema kesho utafanya unakuta mwaka umeisha kama hivi. Kama u hai bado nafasi …

497; Falsafa 100, Ustahimilivu wa akili na mwili kama silaha katika nyakati ngumu za maisha na kuyaendea mafanikio.

Kila siku maisha yanatupa nafasi mbalimbali za kujifunza katika sisi wenyewe, mazingira na hata wengine. Kama si ugumu ambao tunapitia sisi basi kuna wengine wanapitia magumu na kupitia wao tunaweza kujifunza mengi kabla kuwa zamu yetu kama wao. Ustahimilivu ni silaha katika maisha ambayo tunaishi iwe katika nyumba, jamii, taifa hadi Dunia kwa ujumla wake. …

496; Falsafa 100, Maisha yetu katika sura ya MKOPO na Maarifa yatakuwa ngao kwako katika siku za kuishi kwako Duniani.

Rejea ya kitabu; STOICISM, Ultimate Handbook to Stoic Philosophy, Wisdom and Way of Life by Thomas Beckett. ( USTOA, Kitabu cha Falsafa ya Kistoa, Hekima na Njia ya Maisha ) Uwepo wetu wa kuishi Duniani ni wa muda mchache kuliko urefu wa asili iliopo ambayo imekuwa tangu kale. Asili na vilivyomo vimekuwa na urefu wa …

495; ZAMA TUISHIZO,Teknolojia ni fursa ya kukuza uchumi kwa muda mfupi ikiwa kila mmoja ataona hivyo. Rejea ya kitabu

Rejea ya kitabu; THE ENTREPRENEUR MIND by Kelvin Johnson ( FIKRA za MJASIRIAMALI ) Teknolojia hasa ya mawasiliano imefanya maisha yawe rahisi zaidi kuliko zama nyingine zote ambazo binadamu kawahi kupitia na huenda zikawa zama pekee ambazo zitafanya biashara nyingine zikue haraka na nyingine zife kabisa. Mbali na nguvu ya teknolojia ya mawasiliano ilivyo katika …

494; TAFAKURI ya MAISHA, Kila wakati tunahimizwa kufanya mambo kama ndio nafasi pekee ikipita hatutapata tena kuifanya.

Habari Rafiki yangu, siku zinaenda na kama majira ya saa ni saa zaenda dakika lala salama. Mwaka unaishia na wakati huo huo nayo maisha yanapungua na kuongezeka kila siku. Nguvu zetu za miaka ya nyuma huenda zisiwe sawa na huko tuendako na hivyo hitaji la kutunza nguvu na muda ni la msingi sana kwa maisha …

Design a site like this with WordPress.com
Get started