463; TAFAKARI ya ASUBUHI, Dunia yenye kelele nyingi nje na ndani kwa kukaa kimya na kufanya kazi ndio njia unayopaswa kuisimamia siku zote za maisha yako

Rafiki ni siku angavu tena, ni siku nzuri na hata asili yaonyesha uzuri wake, ni wakati hata anga lavutia na zawadi ya uzuri wa asili unaonyesha namna ambavyo Muumbaji ni wa ajabu na ajabu za kazi zake. Leo ni fursa ya pekee ya kuanza pale ulivyosema jana kuwa leo ikifika utaanza, leo ni zawadi ya …

462; NJIA NGUMU, Kurasa 12 kitabu cha kwanza cha mwaka mpya HATUA kubwa 2018/19

Kitabu; WAR of SELF, The 7 Weapons of Self Mastery by Ramman Sheehan Turner ( Vita ya Binafsi, Silaha 7 za Ubobezi binafsi ) 1 ~ 12 Kituo cha KUSIMAMA; Chukua hatua juu ya maisha yako. Hakuna ambaye yuko tayari kuishi maisha yako kama si wewe utajitoa kuishi maisha yako. Rafiki karibu tena katika mwendelezo …

461; Tafakari ya asubuhi, USIJITENGE na maongezi ya wazee ikiwa wataka ufahamu wa mambo katika maisha.

Rafiki ni siku nyingine mpya, ni siku ya kuanza kama bado wasita kuanza kuishi ndoto zako na leo ni siku ya pekee ya kuishi kama ndio siku yetu ya mwisho ambayo ikipita haitakuwepo kama leo. Nafasi ya kuwa hai si kuwa itadumu milele kuna siku tutaipoteza na hatutakuwa nayo wakati huo. Je leo unaenda kuiishi …

460; Tafakari ya jioni, Mizizi ya mafanikio makubwa yamejifichwa ndani kuliko inavyoonekana nje.

Rafiki, jioni ni wakati mzuri sana wa kupima namna ya siku yako ilivyokwenda na kuona ni kwa namna gani leo tumeongeza kitu katika maisha yetu au ndo tumepoteza kabisa. Jizoeshe kila siku jioni ifikapo kujiuliza maswali namna gani umefanikiwa katika malengo yako ya siku na pia kama umeshindwa shida ilikuwa wapi. Kwa njia ya kujiuliza …

459; Mwaka 2018/19, Hizi ndizo programu 12 ambazo nitakushirikisha rafiki yangu upendaye maarifa na unayejua gharama ya hatua kubwa kwa kipindi cha mwaka mzima 2018/19.

Rafiki bila shaka u mzima kabisa wa afya. Kama afya yako haiko sawa nakutakia kuimarika kwako na urejee tena katika majukumu yako ya kila siku. Afya ni mtaji wetu wa kwanza ambao wengi huwa hawaoni kama ndio wenye thamani mpaka siku wapotezapo afya zao. Pili kuwa hai ni nafasi ya pekee sana ya kumshukuru Mungu …

458; MAISHA na Ubobezi, Ungana na wanamafanikio wote Duniani kila ifikapo saa 11 asubuhi kwa kuanza maisha ya kufanya haya mambo 5 kila siku.

Habari Rafiki, naamini unaendelea vizuri Leo ni siku ya 30 ya mwezi Oktoba mwaka 2018. Tarehe kama hii na mwezi itajirudia lakini si mwaka huu tena. Hivyo kama bado unaona wakati upo jitafakari tena juu ya muda na nguvu zako kuwa hazitaendelea kuwepo siku zote ?. Kila siku huja kama fursa kwetu na sisi huwa …

457; Uchambuzi wa kitabu, WHAT YOUNG INDIA WANTS by Chetan Bhagat ( Nini wanakitaka Vijana wa India ?)

(Nini wanakitaka Vijana wa Tanzania ( Kwetu libakie swali hili ) Habari Moninga (Rafiki), nukuu moja ya mwanafalsafa wa Kigiriki aliyefia katika kusimamia misimamo ya kufundisha jamii kufikiri, kuhoji na kujua kweli, Socrates isemayo "The right way to begin is to pay attention to the young, and make them just as good as possible" ikiwa …

456; Mwaka 2018; Mambo 10 niliyojifunza siku 27 za Mwezi Oktoba, Nafasi 100 za UNIVERSITY of SUCCESS 100 na kama unajiuliza uanzaje kusoma vitabu basi soma makala hii mpaka mwisho.

Rafiki siku zinaenda kwa kasi sana, leo huwezi amini namna ambavyo mwaka umeenda kasi na ukiangalia maisha unajikuta muda umepita tu lakini hatua ambazo umepiga ni ndogo ukilinganisha na muda ambao ulikuwa umepata. Mbali na muda ambao umepita kama u bado hai ni zawadi ya pekee sana kumshukuru Mungu. Kila siku usipojua kuwa ni fursa …

455; Kilele cha Siku 100; Ushindi wa siku 100 na mambo 10 niliyojifunza siku 100, Nafasi 100 pekee za UNIVERSITY OF SUCCESS 100 ( CHUO KIKUU cha MAFANIKIO ) na zawadi ya Uchambuzi wa Kitabu kwa maisha bora utoke ulipo

Ukikosa kupongezwa nafasi pekee unayobaki nayo ni kujipongeza mwenyewe. Hongera Malenga wa Ubena kwa ushindi huu ambao umefika najifunza toka kwako Malenga kuwa safari ya maarifa si rahisi lakini umefanikiwa kufika kilele cha siku 100 ulizojipangia na umefika. Mungu akubariki sana na uzoefu ambao umepata wa mbio za siku 100, siku 100 zikupe sababu ya …

454; Uchambuzi wa Kitabu, “YOU CAN SELL”, Results are rewarded, efforts are not” ( UNAWEZA KUUZA ) by SHIV KHERA

WASIFU WA MWANDISHI SHIV KHERA ~ Ni muasisi wa kampuni ya "OUALIFEID LEARNING SYSTEM INC" huko Marekani akiwa ni raia wa India, ni mwandishi wa kimataifa, mwalimu na mshauri wa masuala ya biashara, mjasiriamali mwenye mafanikio makubwa, mhamasishaji ambaye amekuwa akigusa maisha ya watu wengi sana kupitia nafasi yake ya kuwa msemaji maalumu katika uhamasishaji …

Design a site like this with WordPress.com
Get started