Wakati unapongoja mambo yabadilike, hayabadiliki hadi uwajibike.

Maisha ni wajibu mkuu wa kila mtu aliye mtashi kukubaliana na ukweli kuwa "maisha ni matokeo ya uwajibikaji wetu kwa namna fulani". Wajibu huu unatupa kutualika kwa kila matokeo ambayo tunakutana nayo maishani basi kwa sehemu tumechangia kuwa hivyo iwe twajua ama hatujui. Mambo hayabadiliki hadi pale sisi tunapobadilika kuyaona yalivyo. Himizo la kubadilika kwanza …

Ulivyonavyo anza kushukuru mbali na usivyonavyo.

Katika darasa la maisha huwa tunasahau kuona ni utajiri upi mkubwa ambao tunao pale ambapo tunasahau tulivyonavyo na kuhangaika na tusivyonavyo. Tunasahau namna ni rasimali ngapi tulizonazo ambazo zingeweza kutusaidia kuvuka hatua fulani kubwa maishani. Wiki hii nilifanya zoezi la kuangalia au kushukuru mambo ambayo ninayo kuliko yale nisiyonayo. Zoezi hili nilifanya kwa kuchukua notibuku …

Kufundisha ni kuivusha jamii – “Asante mwalimu wangu, Wewe ni Daraja”

Leo ni siku ya walimu Duniani kote. Siku hii ni kutambua na kufanya tafakari ya kina ni kwa vipi uwepo wa walimu umeleta matokeo chanya na kuisaidia Dunia kustawi vizazi hadi vizazi. Nafasi ya walimu ni kubwa sana unapokuja kuelezea maendeleo ya mtu mmoja mmoja hadi jamii nzima. Majitoleo yao ya muda, maarifa na maisha …

Matokeo ya malengo hayaji mpaka pale unapoweka kazi kubwa na maarifa sahihi.

Kuna mambo mawili ambayo mtu anaweza kulalamika kuwa mbona sipati matokeo ninayoyataka katika nipangayo?. Moja utakuta mtu huyo hakuweka kazi ya kutosha au juhudi za kutosha katika anachokitaka. Pili ni maarifa sahihi katika kile anachokipigania. Haya mambo mawili yanaathiri mno katika matokeo ya jambo lolote lile. Huwezi kupata kitu bila kufanya kazi fulani na kama …

Mambo mazuri ni magumu kuyafanya – ‘Jitoe kuyafanya yana Tija”

Nikiwa katika tafakari nazozifanya kila siku ya maisha yangu, huwa nafikirishwa na pande mbili za mambo. Mambo mazuri na mabaya, Mambo mazuri tunayotamani kuyafanya maishani hutupa taabu kuyafanya ingawa yamebeba manufaa na wakati huo huo mambo mabaya huja kiwepesi na kukaa nasi iwe kazi kuyaacha. Tafakari hii inayaakisi maisha yangu na maisha ya watu wengine …

Vikubwa vyote hukua toka vidogo

Haba na haba hujaza kibaba ni moja ya methali yenye kubeba uzito mkubwa wa umuhimu wa kupiga hatua ndogo ndogo maishani kufikia vitu vikubwa. Hakuna kitu kidogo ambacho kikifanywa kwa uendelevu kikakosa kuwa na nguvu au kuzalisha matokeo makubwa. Iwe ni kitu kizuri au kibaya kikifanywa katika uendelevu huleta athari baada ya muda. Hili ndilo …

Pandisha bei ila fanya jambo hili

Kila mtu yupo tayari kununua kitu anachokipenda au alichokipa kipaumbele kuwa ni kitu au hitaji lenye umuhimu kwake. Bei ya kitu, bidhaa au huduma inaweza kuwakwamisha baadhi ya wateja au kufanya wengine wanunue bila kujali bei ila wamesukumwa na nini wanakipata wakishanunua hicho kitu. Thamani ndio kipimo kikubwa ambacho mteja awe mteja wa bidhaa chache …

Wasaidie wengine kwanza kupata- “Ni sheria ngumu ila ina faida”

Sheria moja kubwa ya mafanikio ni kuwasaidia wengine kufanikiwa kabla hujafanikiwa wewe. Huenda ni ngumu kueleweka kwa juu juu ila ukiangalia kwa kina ina maana kubwa sana. Huwezi jua una nini ndani yako mpaka pale ambapo unapopata fursa ya kushirikisha kwa wengine nao wakakupa utambulisho fulani. Inawezekana ujuzi, kipaji, bidhaa, biashara au maarifa unavyo ila …

Usikimbie mazoezi- “Mazoezi ni maandalizi”

Tafiti zinasema kuwa wakati ambao akili imetulia ndipo penye mazingira mazuri ya mtu kupata mawazo bunifu au ufahamu wa kitu wa kumwacha aah aah kumbe!, au kupata maono ya jambo. Utulivu huu ni ule wa akili inapokuwa inafikiria sasa. Imetokea leo wakati sijui nitaandika jambo gani kama nilivyojipa ahadi kuhakikisha naandika kila siku iwe siku …

Endeleza kipaji chako- “Tayari unao Mtaji”

Kila kona ukitembea utakutana na watu wengi walofanikiwa kutokana na vipaji vyao. Wengine ni vipaji vya kucheza mpira, kuandika, kuchora, kuimba, mahesabu, utoaji ushauri na kadhalika. Mbali na machapisho mengi na vitabu kugusia kuwa mtu ana vipaji zaidi ya 08 bado kuna kundi kubwa la watu ambalo limekosa kutambua kuwa ndani ya kila mtu pana …

Design a site like this with WordPress.com
Get started