Unapoitazama siku kama siku ya mwisho- “Leo imejitosheleza”

Kuna mambo mengi tunayaghairisha katika maisha yetu hili tunalifanya kwa kuona huenda bado muda tunao. Ila tumekuwa mashahidi kwa kuona namna wengi ambao tulokuwa nao miaka 5 ilopita hawapo sasa. Hili linatukumbusha namna ambavyo kila siku tuwapo na nafasi ya uzima ni mwaliko wa kuitumia siku hiyo kama ni siku ya mwisho na hatuna nafasi …

Safari ya maisha itakupitisha katika mengi- “Jifunze kukaza moyo”

Ukweli wa maisha ni kuwa tutaendelea kupitia changamoto siku zote za maisha yetu. Utakaposema kuwa umemaliza changamoto moja basi itatokea nyingine. Hata kufanikiwa nako hakuachi kutokuwa na changamoto sawa sawa na mafanikio apatayo mtu. Kujua kweli hii inakusaidia kuwa mtu imara na kukubali uhalisia wa maisha ni uwepo wa kuvuka vihunzi vya changamoto kila siku …

Tunakua kupitia vile visivyotupa furaha au matokeo sasa – “Maumivu hutukomaza”

Maumivu ya msuli baada ya zoezi kufanyika ndio mwanzo wa kuimarika kwa misuli ya mtu. Kuumia kimwili pale unapofanya hatua ya kuamka mapema kila siku ndivyo unavyojipa nafasi ya kukomaa kitabia kwa kuendelea kuamka asubuhi na mapema bila shida. Mwanzo wa jambo hasa yaliyo na matokeo mazuri baadaye huwa yafanyikapo sasa hayatupi furaha bali huwa …

Asili ina funzo la uendelevu- “Kuchomoza na kuzama kwa Jua”

Asili ni utele wa mambo yote tuonayo na pengine wakati mwingine tusoyaona au kuyashika ila yapo mfano hewa, upepo, sauti, mwanga na kadhalika.  Asili inatupa picha nzima ya kuendelea kwa vitu na hili linaonekana pale ambapo tunajifunza maisha ya mbegu ilivyo. Mbegu yoyote ile imebeba nguvu ya uzao ndani yake. Tunaona namna mbegu moja ya …

Unachokirudia kinakupa kukitawala au kitakutawala.

Fundi mzoefu anapata sifa moja kubwa ya kuitawala kazi yake na humpa watu wengi wamfahamu kwa ustadi wake au ufundi wake. Unapochunguza kwa kina unakuja kuona ufundi wake unatokana na marudio marudio ya kukifanya kitu kwa muda mrefu. Kiasili ni hali ya kawaida kuwa kile unachokirudia muda mrefu unakipatia uzoefu na kukibobea na wakati huo …

Wakati wa sasa ni mtaji wa kuanza kufanya kitu- “Ijayo haitabiriki”

Sijui kama Dunia ilikuwa inajua kama mwaka 2020 ungekuwa mwaka wa tofauti kwa matukio yenye kutikisa Dunia kama mlipuko wa “CORONA” ungebadili mambo mengi na kuathiri hata mifumo ya kibiashara kimataifa. Yote ni angalizo la namna maisha yetu wakati pekee mzuri wa kujiandaa au kuanza kufanya kitu ni sasa. Wakati unaofikiri baadaye utafanya huenda usipate …

Mwaliko wa kushukuru kila iitwapo leo- “Uhai ni Zawadi”

Matatizo yanayotokea kwa mtu huficha uzuri wa mambo mengi ambayo mtu anaendelea kuwa nayo. Ni kweli mtu kaingia katika matatizo ya madeni au kapoteza kazi ila ni mzima wa mwili, yupo hai na ana watu wanaomzunguka. Ila akipitia katika hayo magumu basi anasahau uzuri wa maisha na fursa nyingine ambazo bado hajazipoteza. Hatupaswi kuzibwa macho …

Utapata ugumu mwanzoni tu – “Jikaze umalize ulichokianza”

Uendelevu katika kufanya mambo maishani ni hali ngumu kwa watu wengi sio wewe peke yako unayepitia. Kuanza kitu kunaweza kuwa kwepesi na kazi ikaanza pale unapotakiwa ulichokianzisha ukiendeleze kila siku. Nimeona hili katika maisha yangu, nimejifunza katika mazingira yanayonizunguka na nimejifunza kwa watu pia. Mfano rahisi ni pale unapoona nyumba nyingi mtu kaanzisha msingi ila …

Ukuaji wa maisha ni katika kuvuka vitu navyohofia kuvifanya- Jenga UTHUBUTU.

Wakati naanza kuandika mitandaoni siku za mwanzo mwanzo nilikuwa sijajua kuwa namna vile nilivyohofia ndivyo vilivyofungua njia ya kufanya makubwa zaidi. Nilianza kama mwandishi wa makala fupi fupi tu na mashairi. Ila muda ulivyosogea nilianza kuchambua vitabu na kuwashirikisha watu na kufikia zaidi ya idadi ya vitabu vipatavyo 60 na zaidi nilivyovifanyia uchambuzi na kuwashirikisha …

Ujasiri ni kuinuka tena katika anguko- “Anza upya’’

Zama tunazoishi sasa na matukio tunayopitia maishani si mageni kuwa watu walokuwa kabla yetu hawakupitia. Maisha yao na yetu sasa ni mzunguko wa mambo yale yale yanayoendelea kumkumba mtu katika maisha yake. Hili ndilo linalofanya maisha yahitaji ujasiri na ustahimilivu kuyaendesha na kukabiliana na kila aina ya changamoto mtu atayoweza kupitia. Changamoto zinazomkumba mtu katika …

Design a site like this with WordPress.com
Get started