Habari ya siku nyingine mpya, imekuwa ni neema tena kuiona hii inatupa nguvu kuwa leo ni kama ukurasa safi wa karatasi unaotakiwa kuandikwa kwa uzuri. Siku inaanza kuonekana vizuri asubuhi kwa kuwa na vipaumbele vitakavyokusogeza mbele katika mafanikio yako iwe ni elimu, kiroho, kiuchumi hata kijamii kwa ujumla. Leo tujikumbushe kwa Habari ya namna ya …
LEO NI PISHI LA KESHO
Habari ya siku mpya ndugu msomaji wa blog hii. Ni jambo jema na shukurani kwa Muumba anayetupa nafasi na kuona siku mpya na nguvu mpya Dunia imekuwa inabadilika kila siku, kiwango cha kubadilika kwake Ni cha kasi zaidi kuliko namna ambavyo mwitikio Wa watu unakua. Sayansi inakua zaidi na hata kuhatarisha maisha ya watu licha …
MAANA BINADAMU TUNAYO KAWAIDA KUSAHAU
Tusije kusahau jambo hili, maana binadamu tunayo kawaida ya kusahau Usijesahau mtoto akikua atakuwa mtu mzima, na huenda alichokibeba huwezi jua atazaa kitu gani ? Usijesahau aliyekuwa na afya huenda akawa mgonjwa mtarajiwa licha kujua taratibu zote za afya Usijesahau kuwa leo itaisha na itapita na siku nyingine itakuja na mambo yake Usijesahau kuwa kuna …
KESHO UNA LAKO JAMBO
Utendi: Kesho Una Lako Jambo Kesho U lugha za fumbo Umeniacha kikumbo Niige watu mkumbo Niahirishe na mambo Kesho nakutafuta miaka sijakupata Hadi mvi nimepata Ngozi nayo yajivuta Nguvu zikaniondoka Kesho nikidhani shaka Nikajua itafika Ningali nguvu hakika Kauli hii ya kesho Kwangu imekuwa mwasho Lini utakuwa mwisho Kesho aje hitimisho ? Uliniahidi kesho Uvivu …
MACHO ANGALIA MBELE
UTENZI : MACHO ANGALIA MBELE Ulikuja peke yako Na hazina ndani yako Ulikuja jinsi yako Ulete mabadiliko Kutimiza lengo lako Siku za uhai wako Iweke juhudi yako Kuishi maisha yako Pambana kwa nguvu zako Ukimwomba Mungu wako Uwe mbea maisha yako Timiza wajibu wako Ushike kilicho chako Macho mbele nia yako Sikia sauti yako Moyoni …
USIMSEME MTU, JISEMESHE MWENYEWE
SHAIRI: NAJISEMESHA MWENYEWE Najisemesha mwenyewe, huwa zingo aisema Kujitathimini wewe, ukajijua vyema Jukumu ni lako wewe, sipofanya utakwama Mtu na asilaumiwe, kuzipeleka lawama. Jitambue jikague, kwa kujisemesha wewe Jichambue ujijue, faida yako mwenyewe Na Jione jipimee, kioo chako nakiwe kukumbuka jichague, kichwani ujielewe Usiseme ya jirani, kwanza jione machoni Na uyajue ya ndani,yako yaliyo sirini …
Karibu Kwenye FIGA LA USHAIRI.
FIGA LA USHAIRI Ni Blog itakayokuwa na hazina za jumla za kimaandishi hasa hasa urithi wa tanzu ya ushairi, shairi na tenzi kwa ajili ya kutunza, kuelimisha, kukuza lugha ya kiswahili na zaidi kuhifadhi utajiri wa lugha yetu. Pia itaibua wigo mpana kwa washairi wachanga na wakongwe wasiopata nafasi kuonyesha Kazi zao lengo kuenzi na …