Fanya kila kitu kana kwamba hutaipata hiyo nafasi tena

Mara ngapi katika maisha yako umekuwa unakutana na matukio ambayo ungetamani kwamba ungepewa nafasi tena basi ungeitumia vizuri zaidi maana toka hiyo nafasi ipite huna tena marudio ya kuifanya tena. Inawezekana ni nafasi ulikuwa nayo ya kuzungumza na mtu, kutamani kusikia uambiwe kitu na mtu ila ulipoteza nafasi hiyo kwa mtu huyo kufariki ukifikiri ungepata …

Maandalizi yafanye mambo yakiwa shwari – [Shughulika na mambo yakiwa machanga]

Maisha yetu yanaingia katika ugumu kutokana na ukosefu wa maandalizi. Huwa mambo mengi yanatokea yakitukuta tulikuwa hatuna maandalizi na hili huwa linatuadhibu kweli kweli kiakili hadi kihisia. Hivi hujaona namna umeingia katika changamoto za ulipaji gharama za afya iwe kwako binafsi au watu wako wa karibu na hamkuwahi kuwa na akiba yoyote ile au bima …

Magumu unayopitia yanakuandaa – Uimara una GHARAMA

Magumu tunayopitia katika maisha huenda katika upungufu wetu wa ufahamu wa jambo tulopitia au huenda ni kuguswa au kuumizwa katika hisia zetu au pengine ni ukomo wetu wa kuyaona mambo nje ya mwonekano wake. Magumu yoyote yale ambayo tumepitia na huenda tutaendelea kuyapitia ni njia ya maandalizi katika maisha bora na maisha ya uimara. Uimara …

Leo hii ni mbegu- Kuwa na moyo wa Subira

Subira ni ukomavu mkubwa katika maisha. Usipokuwa na subira mambo mengi katika maisha una nafasi kubwa ya kuyakosa. Subira inaumiza hasa pale ambapo una haraka ya kupata kitu kwa wakati huo. Subira inachosha pale ambapo unatamani matokeo ya mambo yaje yaje haraka haraka. Hata hivyo huwezi kupata matokeo bora unapokosa kukomaa katika subira ya kitu, …

Furaha ya maisha ipo katika utambuzi wa mambo– Washa Mshumaa

Kinachokuzuia kuona Utele katika maisha ni ngazi uliopo ya utambuzi wa mambo na kujitambua. Watu wote waloanza kufanya vitu vikubwa maishani iwe ubunifu, ugunduzi, mapinduzi ya mambo na hata kugusa maelfu ya watu kwa maisha yao ni matokeo ya wao kujitambua na kuwa na utambuzi wa mambo. Kujitambua ni kuamka na kuanza kuona ulivyonavyo, kuanza …

Ikamate akili yako inayozurura– Jifunze kuwa SASA

Maumivu unayopitia ya mambo yanachangiwa sana na kukosa udhibiti wa akili katika kuangalia SASA. Akili yako inapokuwa sasa na isiwe na hali ya kuhama hama utaweza kudhibiti hisia na mwili. Uwezo huu wa kudhibiti akili na mwili kwa akili kuwa sasa kunakupa utulivu mkubwa ndani yako na nafasi ya kutatua matatizo mengi maishani. Mwili unaingia …

Mwili ni CHOMBO tu!

Maisha yana darasa pana. Hili limeniwazisha namna kitu kidogo kwako unavyofikiri ila sivyo katika uhalisia wake. Tarehe 06 mwezi huu Agosti niliandika katika kiunganishi kifuatacho na mwalimu wangu naye akanijibu kupitia utungo. SOMA ZAIDI https://figalaushairi.home.blog/2020/08/06/mwili-ni-njia-ya-utokeaji-wa-hisia-akili-na-nguvu-ya-kiroho-mwili-ni-chombo/ Akanitungia mrejesho wa utungo baada ya kusoma makala ya hapo juu katika kiunganishi. Utungo si kazi ndogo ni zoezi la …

Kisichokuwa na mwendo kinakufa taratibu – Maisha ni MWENDO

Leo wakati naendelea na safari ya kujifunza kuhusu mtu na maisha ndipo nilipokuja na sentensi ya maneno matatu “Maisha ni Mwendo”. Hii imekuja kwa kuangalia yale yanayonizunguka na kunifungua kuwa kinachokosa mwendo hufa. Hii nimekuwa naona pale ambapo watu wanaishia njiani kuendelea na vitu walivyoanzisha [ kuvipa mwendo ] vinavyopotea badala ya muda. Si hilo …

Mwili ni njia ya utokeaji wa hisia, akili na nguvu ya kiroho- MWILI ni CHOMBO

Leo wakati naendelea kutafakari juu ya ngazi za uwepo za mtu nilishangazwa na namna mwili unavyofanya kazi kubwa na utupao thamani kubwa maishani. Tuachane na vile ambavyo tunauchukulia mwili kwa mtizamo hasi bali mwili unapotazamwa kwa nafasi nzuri ni moja ya ngazi ya mwonekano wetu kiumbo unaotupa kuona au njia ya utokeaji wa ngazi nyingine …

Utakutana na ugumu unapoamua kuanzisha hatua mpya- VUMILIA

Asili yetu sisi binadamu ni kupata faraja tunapokuwa katika hali zile ambazo tumezizoea na huwa kazi ngumu na safari isofurahisha pale tunapotaka kufanya mambo nje na mazoea yetu ya kila siku. Utaona namna ilivyo ngumu kwa mtu ambaye si mazoea yake kuamka asubuhi ilivyo kazi kwake kuamka asubuhi. Utaona namna ilivyo kazi kwa mtu asiye …

Design a site like this with WordPress.com
Get started