Ngozi ngumu; Wakatishaji tamaa ni wengi

Marcus Aurelius anasema “Kila siku unayoamka jua unaenda kukutana na watu wasumbufu, wakorofi, wasio na shukrani, wakatishaji tamaa, wasiojua kupongeza, wasiojua mazuri na wenye chuki na hatua unazopiga siku hadi siku”. Ukija kwa kina wanaokukatisha tamaa kuna mambo mawili au matatu yanawasumbua. Moja ni wao kushindwa kufanya kitu unachokifanya hivyo wanajilinganisha na wanaona wewe mbona …

Ongeza thamani na fedha zitakufuata. Fedha huvutwa kwa kutoa thamani na kujua sayansi ya utoaji inavyofanya kazi.

Fedha ni hitaji la muhimu sana kwa zama tunazoishi. Mtu anayekwambia fedha si muhimu basi huenda anazo tele. Fedha ni muhimu mno kwa mifano mingi ambayo wewe mwenyewe umekuwa shahidi pale ambapo hitaji lako lingeweza au linaweza kujibiwa dakika chache tu kama ungekuwa na fedha. Fedha ni alama ya thamani ya kitu au bidhaa au …

Usisubiri hadi mwaka mpya upange malengo. Kila asubuhi ni siku mpya katika maisha na hujui yatakayozaliwa siku ijayo.

Ni mtu kipofu yule asiyeweza kuona alichonacho na kuhangaika na asichonacho. Hili linatokea pale mtu anaposubiri kuanza maisha mapya kila ifikapo mwaka mpya na siku nyingine 300 zinaenda tu pasipo kuziishi kitoshelevu. Maisha ni sasa na asubuhi ifikapo ni maisha mengine mapya huendelea nayo huendelea kuwa sasa. Iwe ni mwaka mpya bado itakuja kuwa sasa. …

Unachokiona kigumu sasa ni sababu u mgeni kufanya kitu hicho. Jipe muda utajua kama wanavyojua wengine.

Maisha ni ngazi. Ngazi ina sehemu ya chini na sehemu ya juu. Huwezi rukia juu pasipo kuanza chini hatua hadi hatua. Hili lipo katika safari ya kujifunza mambo mapya maishani. Hatua za mwanzo za kujifunza kitu huwa kinaonekana kigumu kweli ila muda unapopita kama utajitoa kujifunza basi ule ugumu wa awali huanza kupotea siku hadi …

Uzoefu ni mtaji. Tafuta uzoefu uwe huru

Kinachotofautisha watu maishani ni mambo mawili au matatu. Jambo la kwanza ambalo nimeona kwa kutazama na kuishi kwangu ni juu ya uzoefu. Ukiwa na uzoefu wa jambo unakuwa mtu huru, jasiri na mwenye furaha. Mtu asiye na uzoefu katika eneo fulani huwa ni mtu asiye na ujasiri, mashaka na hofu. Tenga muda na wekeza kufanya …

Nyakati ngumu endelea kuwa imara.

Kuna wakati ambao unakutana na ugumu kiasi kwamba unapata sababu za kukata tamaa pale unapoona watu wengi ulokuwa unajua wana nguvu na ni watu imara nao nyakati ngumu ziliwaondoa ujasiri wao na nguvu zao nao kuwa watu dhaifu na wenye kuhitaji nguvu ya kusonga mbele. Nyakati ngumu ni nzuri kwa lengo moja kubwa la ukuaji …

Kuchukua hatua mapema kunazuia gharama kubwa baadaye.

Kughairisha mambo ni tatizo kubwa linalonyima fursa nyingi kufunguka kwa watu wengi. Pale unapoghairisha vitu au kufanya jambo kwa kufikiri huenda baadaye utafanikiwa kulifanya kumesababisha majuto makubwa siku zijazo. Imekuwa kawaida kughairisha mambo kwa kufanya siku moja na baadaye kughairisha inakuwa tabia inayosababisha mambo mengi yasiwezekane kutokea. Hili linaonekana dhahiri pale ambapo mwaka mpya unapoanza …

Design a site like this with WordPress.com
Get started