Vitabu 4 vinavyofundisha namna mafanikio makubwa ni matokeo ya kuzingatia vitu vidogo vidogo.

Nimerejea kukusanyia kazi zangu nyingi ambazo nilikuwa nazituma kupitia mitandao ya kijamii bila kuzihifadhi katika blogu hii ya figa la ushairi. Nimerejea uendelee kujifunza mengi kupitia hizi makala ambazo zitaendelea kudumu miaka mingi kuanzia sasa. Endelea…………. Nukuu yoyote ni matokeo ya uzoefu fulani wa mambo wa mtu. Hii ndilo linatupa nukuu ya kumbukizi ya Mother …

Safari ya Muziki [01]; Mdomo wa bata na pumzi

Uzuri wa muziki una mambo makubwa mawili nifahamuyo. Moja ni uzuri wa upigwaji wa chombo husika na pili ni ustadi wa mwanamuziki mwenyewe katika anachokiimba au anachokipiga. Ninapenda kujifunza mengi katika ulimwengu wa muziki na vyombo vya muziki. Leo nikukaribishe katika safari ya chombo ninachokihusudu sana kiitwacho "SAXOPHONE" au kwa lugha ya mtaani wanakiita mdomo …

Kuanza mapema ni kujitengenezea nafasi nzuri baadaye

Jioni ni muda mzuri sana wa kufanya tafakari. Jioni hurejeza akili namna siku ilivyokwenda na yale ambayo umejifunza kupitia siku husika. Napenda kuangalia maisha yalivyoenda na hii inajenga hatua bora inayofuata. Maisha ni kuanza mapema kabla muda hujapita. Wale ambao leo tunawaona wamefika mbali katika maeneo mbalimbali maishani ni wao kuanza mapema kufanya vitu. Wakati …

Safari ya ndani ya mabadiliko ni ndefu

Muda pekee wenye thamani katika maisha yetu ni sasa. Muda huu tulionao sasa ndio wenye kubeba hatma ya maisha yetu. Unaporuhusu mawazo yako kwenda eneo lingine ni wazi unaruhusu kupoteza muda tulionao sasa. Hivyo kwa kulijua hilo la muhimu basi ni mwaliko wa sasa wa kurejea na kujiuliza je kuna aina ya safari tunayoalikwa kila …

Matukio maishani yapo tu. Jali mambo yako

Kila siku unapoamka kuna mambo hutokea na huwa hayana dalili kuwa siku yataisha. Kupambana na matukio yanayotokea kila siku ni njia ya uhakika ya kupoteza muda wako na maisha yaliyo katika ukomo. Watu wengi wanayapoteza maisha yao pasipo kujua kadri unavyojipa umakini katika matukio yanayotokea iwe katika jamii, taifa au Duniani ndivyo mambo yako yasivyoweza …

Kaza moyo na ivumilie safari ya mafanikio

Habari rafiki yangu. Ni kipindi kirefu cha zaidi ya miezi 2 sijakuandikia chochote kile. Nimerejea kuendelea kuandika na hii ndio habari bora ninayokuambia muda huu ambao umefungua blogu hii na kuanza kuendelea kusoma. Maisha ni darasa na ni safari inayohitaji kujitoa kweli kweli bila kujibakiza. Hili ndilo linatufanya tuwe ni watu tunaohitaji kukaza moyo huku …

Ngozi ngumu; Wakatishaji tamaa ni wengi

Marcus Aurelius anasema “Kila siku unayoamka jua unaenda kukutana na watu wasumbufu, wakorofi, wasio na shukrani, wakatishaji tamaa, wasiojua kupongeza, wasiojua mazuri na wenye chuki na hatua unazopiga siku hadi siku”. Ukija kwa kina wanaokukatisha tamaa kuna mambo mawili au matatu yanawasumbua. Moja ni wao kushindwa kufanya kitu unachokifanya hivyo wanajilinganisha na wanaona wewe mbona …

Ongeza thamani na fedha zitakufuata. Fedha huvutwa kwa kutoa thamani na kujua sayansi ya utoaji inavyofanya kazi.

Fedha ni hitaji la muhimu sana kwa zama tunazoishi. Mtu anayekwambia fedha si muhimu basi huenda anazo tele. Fedha ni muhimu mno kwa mifano mingi ambayo wewe mwenyewe umekuwa shahidi pale ambapo hitaji lako lingeweza au linaweza kujibiwa dakika chache tu kama ungekuwa na fedha. Fedha ni alama ya thamani ya kitu au bidhaa au …

Usisubiri hadi mwaka mpya upange malengo. Kila asubuhi ni siku mpya katika maisha na hujui yatakayozaliwa siku ijayo.

Ni mtu kipofu yule asiyeweza kuona alichonacho na kuhangaika na asichonacho. Hili linatokea pale mtu anaposubiri kuanza maisha mapya kila ifikapo mwaka mpya na siku nyingine 300 zinaenda tu pasipo kuziishi kitoshelevu. Maisha ni sasa na asubuhi ifikapo ni maisha mengine mapya huendelea nayo huendelea kuwa sasa. Iwe ni mwaka mpya bado itakuja kuwa sasa. …

Unachokiona kigumu sasa ni sababu u mgeni kufanya kitu hicho. Jipe muda utajua kama wanavyojua wengine.

Maisha ni ngazi. Ngazi ina sehemu ya chini na sehemu ya juu. Huwezi rukia juu pasipo kuanza chini hatua hadi hatua. Hili lipo katika safari ya kujifunza mambo mapya maishani. Hatua za mwanzo za kujifunza kitu huwa kinaonekana kigumu kweli ila muda unapopita kama utajitoa kujifunza basi ule ugumu wa awali huanza kupotea siku hadi …

Design a site like this with WordPress.com
Get started